Wanawake na kupenda wanaume wenye hela...

Siku hizi naona kupewa gari na wanaume imekuwa issue kubwa.......kiasi kwamba kuna wakati hoja inajadiliwa mtu labda ana tatizo...mtu anaweka comment za ajabu kwamba wasichana wa siku hizi mnafuata hela na mnadanganywa na magari sijui nyumba na vitu kama hivyo.........ndo maana mnateseka............Au mtu umepata mwanaume mwenye uwezo watu wanakukatisha tamaa,mara hawajatulia,atakudharau mara sijui nini.......

Na wasichana tumekuwa tukijaribu kubisha hilo au kusema si wote.........

Nafikiri wote tunapenda maisha mazuri,hayaletwi na hela bali hela ni sehemu tu ya kuwa na maisha bora na yenye furaha.....

Nikiangalia dunia ya sasa,na hasa jamii inayonizunguka siioni tofauti ya kimatendo na kimaadili ya mwanaume mwenye hela na maskini......wanaume asilimia kubwa ni waongo na wanatoka nje ya ndoa na wengine wanashindwa hata kutimiza wajibu wao kama baba na kama mume.........mimi siamini kwamba ukiwa na hela kiasi au usipokuwa nazo inakufanya wewe uwe mwema sana au mwenye upendo wa kweli....

Nafikiri maisha ni kuchagua na bahati, mwanamke ukipata mwanaume mwenye hela nyingi manake hata mwenye mia mbili atasema anazo.... kama UNAMPENDA, mchunguze, chukua muda tafuta ufahamu wa kile anachokifanya kumpatia kipato...... ukimuona anakufaa nenda,ishi maisha yako,Sali,lea watoto wako na kuwa mvumilivu,zaidi jitahidi kuwa wa manufaa kwa jamii yako na wenye shida.

Ukiwezeshwa nawe kaza buti,jijenge,fanya kazi usiwe tegemezi.......na zaidi kuwa msaada kwa mumeo na furaha yake ili aendelee kufanikiwa zaidi na zaidi mkumbushe kuwasaidia wasio na uwezo.

Samahani Michelle,
Kama hutojali unaweza kunijibu hapa hapa upenuni, ukiona noma fanya ze needful, Umeolewa dada yangu?
 
pesa ni matokeo na wadada hawana budi kukaa chini na kuhangaikia kutafuta pesa zao , lakini embu tazama mazungumzo meni ya kina dada,yanaegemea wapi .....pesa pesa hata wale wenye vipato siku izi mawazo yao ni kuchuna tu ...hawa wanaume unafikiri hawasikii wala kuelewa wanahitaji kupendwa nao lakini wengi wamekuwa na wasiwasi wakiamini inayopendwa ni mifuko yao

kina dada wanahitaji kubadilika na kujifunza kujitegemea sio ooh kila mara vocha,umeona gagulo zuri,mama anaumwa,offer ya bia na kitimoto hiyo mizinga ndio inayoponza

Asante kwa mawazo yako.....naona ume-generalize sana kuwa ni mazungumzo yote ya wadada yanaelekea kuchuna tu....labda unaozungumza nao....wengi siku hizi wameamka,ni wachache sana wanakalisha makalio kusubiri wanaume wa kuchuna na hata kupata mwenye hela ni matokeo pia....anaweza asije ukapata asiye nazo..... ni vizuri kujitegemea na kufanya kazi kwa bidii kwa wale ambao hawafanyi hivyo......

Wanaume wanapaswa kujua si kila mwanamke anawapendea hela zako,wengi wamejiwekea kuwa wanapendewa hela zao hata kama ninachopenda ni utu wako na ulivyo...wajiamini,wachukue muda kuangalia kama mapenzi ni genuine si kukaa na kusema tunawapendea hela...na wao pia wawe na bidii hakuna anayetaka mzigo wa mume na baba watoto....
 
no comment for 2day...ila nahisi kuanza kuku-fuatilia kujua "UMEPATA WAPI" uwezo huu adimu sana kwa wanawake wengi hasa wa dunia ya tatu kama tanzania kuja na hoja +ve na ya-kujenga jamii kama hii... be blezd

AMEN, Be blessed too my brother!!!
 
sio wote ndio maana hata wewe umeweza kuleta hii post hapa lakini bado kuna kundi kubwa la kina dada wanaishi maisha ya kuchuna ,wengine ni wake wa ndoa kabisa lakini pesa yake yake ya mume ya wote na huo tunaita nini mume akikosa balaa kubwa huoni kama wanaume wantuona wachunaji hasa wale waliobahatika kuwa na kipato kikubwa hembu tusubiri mawazo yao.

Mzeiya u are lost bana tokea mwaka huu uanze sijakuona hapa au ndio tunapishana otherwise hope u are good
 
Embu nielekeze namna ya kutoa thanks si unajua mambo ya technologia kule kwetu yamekaa kushoto nikupe shukrani zako za dhati
I think you have to log in first. Once you do it, below every post there are links of "Reply, Reply with Quote" on the right and "Thanks, Posted via Mobile" on the left.
Hope you find it useful.
 
Kuna msemo kutoka dini nyingi na kwa wanafalsafa unaosema hivi: "Tajiri si yule aliye na vingi bali yule anayetosheka na vichache". Wako wanaume wenye uwezo mkubwa na wametulia na familia zao, pia wapo wanaume masikini ambao ni viwembe. Zipo ndoa za masikini watupu lakini wameridhika na hali zao. Zipo ndoa za wanawake walioolewa na wenye uwezo na bado wanatoka nje. Kwa ufupi, dunia ina watu wa kila aina.
Ushauri wako dada Michelle ni mzuri sana - Turidhike na tulichonacho, mali usiyoitokea jasho haina baraka. Tujitume, tusali, tuombe, tulee ili tuwe mfano mzuri kwa watoto wetu. Tukumbuke, "Mtoto hufuata kisogo cha mzazi (mlezi) wake".
 
sio wote ndio maana hata wewe umeweza kuleta hii post hapa lakini bado kuna kundi kubwa la kina dada wanaishi maisha ya kuchuna ,wengine ni wake wa ndoa kabisa lakini pesa yake yake ya mume ya wote na huo tunaita nini mume akikosa balaa kubwa huoni kama wanaume wantuona wachunaji hasa wale waliobahatika kuwa na kipato kikubwa hembu tusubiri mawazo yao.

Ni kweli kwa sababu moja au nyingine simlaumu mwanamume anaposema wanawake ni wachunaji kwa kuwa wapo wanaofanya hivyo na wapo ambao hata elimu waliyonayo haijawasaidia kuondokana na fikra kuwa anapaswa kujitegemea na kuacha kutegemea wanaume.....ninayo imani maisha yanaendelea kubadilika na hali tu inavyozidi kuwa ngumu watabadilika,manake itafika wakati lazima nawe ufanye kazi ili familia isogee.....kwa kuwa wote si wachunaji,ni wajibu wa mwanaume kumchunguza yule anayempenda akiona anachunwa akimbie au azidi kumpenda ni uamuzi wake....lakini si wote tunachuna,na kwa kweli kuna wakati tunahitaji msaada wa hapa na pale,wasiache kutusaidia kwa fikra kuwa tunawachuna....thanks Chauro,i got your point.
 
ha ha ha ha, bado sijampata mume wa kunioa.....Mungu akipenda!!!

Una mawazo very constructive, kama wadada mkiendelea kuwa na mawazo ya namna hii basi huko mbele ya safari hakutakuwa na mambo ya kutuumiza vichwa.
Manake siku hizi ukitafuta gf au mke unaumiza kichwa, utampataje mkweli, manake wengi siku hizi wako kikazi zaidi.

Muombe Mungu aliyehai akupatie mume bora ili akusaidie kutimiza ndoto zako, manake unaonekana unajua unachokitaka.
 
hi akina MICHELLE,HASHYCOOL,THE FINEST,BIGIRITA EMT, BACHA and PAULINA!!!

ntarudi baadae kwa hii sred.
 
Kuna msemo kutoka dini nyingi na kwa wanafalsafa unaosema hivi: "Tajiri si yule aliye na vingi bali yule anayetosheka na vichache". Wako wanaume wenye uwezo mkubwa na wametulia na familia zao, pia wapo wanaume masikini ambao ni viwembe. Zipo ndoa za masikini watupu lakini wameridhika na hali zao. Zipo ndoa za wanawake walioolewa na wenye uwezo na bado wanatoka nje. Kwa ufupi, dunia ina watu wa kila aina.
Ushauri wako dada Michelle ni mzuri sana - Turidhike na tulichonacho, mali usiyoitokea jasho haina baraka. Tujitume, tusali, tuombe, tulee ili tuwe mfano mzuri kwa watoto wetu. Tukumbuke, "Mtoto hufuata kisogo cha mzazi (mlezi) wake".

Asante sana dada yangu,mawazo mazuri sana na yenye hekima....
 
Ni kweli kwa sababu moja au nyingine simlaumu mwanamume anaposema wanawake ni wachunaji kwa kuwa wapo wanaofanya hivyo na wapo ambao hata elimu waliyonayo haijawasaidia kuondokana na fikra kuwa anapaswa kujitegemea na kuacha kutegemea wanaume.....ninayo imani maisha yanaendelea kubadilika na hali tu inavyozidi kuwa ngumu watabadilika,manake itafika wakati lazima nawe ufanye kazi ili familia isogee.....kwa kuwa wote si wachunaji,ni wajibu wa mwanaume kumchunguza yule anayempenda akiona anachunwa akimbie au azidi kumpenda ni uamuzi wake....lakini si wote tunachuna,na kwa kweli kuna wakati tunahitaji msaada wa hapa na pale,wasiache kutusaidia kwa fikra kuwa tunawachuna....thanks Chauro,i got your point.

Tatizo kubwa linalotukabili wanaume wengi ni kumtambua mwanamke anayekupenda kwa dhati ya moyo wake.

Kuna wanawake wamefuzu chuo cha sanaa, yaani wanajua kujivika ngozi za kondoo huwezi amini, anakuwa mpoleee lakini akitaka kuvuna anajua tu atakukamatia wapi. wanawake wako tayari kuficha tabia zao halisi hata kwa miaka kadhaa ilimuradi watimize malengo. mwingine atakupeleka mpaka utamuoa akijua kwamba kwakuwa umemuoa basi utakuwa umeridhika kwamba anakupenda. Akishatimiza malengo yake hapo sasa anaanza kuchomoa makucha yake.
 
Ni kweli kabisa,najua si rahisi Mwita na tunafanya maamuzi bila kujua ukweli kuhusu wenzi wetu kwakuwa wanaficha makucha au ni wasanii....ni kujitahidi tu,kuchukua muda wa kutosha kuwafahamu na zaidi kumuomba Mungu aonaye sirini....
 
Back
Top Bottom