Wanawake na kaburi la mapema.....! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wanawake na kaburi la mapema.....!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by MziziMkavu, Aug 28, 2012.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Aug 28, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,612
  Trophy Points: 280
  [​IMG]

  Hivi karibuni nimesoma utafiti katika makabrasha yangu kuhusiana na maradhi mbalimbali yanayowakabili wanawake walioko kwenye ndoa au uhusiano wenye mashaka. Tafiti zinaonyesha kwamba, wanawake wote ambao wana mashaka na wasiwasi kuhusu usalama wa ndoa zao, wasiowaamini waume zao, kwa kawaida, wanakuwa na kinga dhaifu sana dhidi ya maradhi. Haiyumkini hata wale wanawake waliosemwa kuwa wamekufa kwa ukimwi huku waume zao wakiendelea kudunda na maisha na pengine hata kuoa na kuzaa kama kawaida, wake hao walipoteza maisha kutokana na sababu hii.


  Mtafiti mmoja Angelo Picardi wa Italia anasema, amethibitisha kuhusu hilo kwa kuwakagua wanawake wapatao 61. Kumbuka kwenye miili yetu kuna seli ambazo kimaumbile kazi yake ni kupambana na maradhi. Kwa wale wanawake wanaoishi kwenye ndoa za mashaka, ambapo hawawaamini waume zao na huku wakihofia kupoteza ndoa zao, mfumo wao wa seli hizo za kinga ni dhaifu, ukilinganisha na wanawake ambao hawana wasiwasi na ndoa zao huvunjika au kuachwa na waume zao.


  Maana yake ni nini? Ni kwamba, wanawake ambao wana hofu kwamba, waume zao wanaweza kuwaacha na hivyo kuhisi kutishika na wale ambao wana wivu kwa sababu hawajiamini, hushikwa na maradhi kirahisi sana. Ni rahisi kwao kuwa nyondenyonde kwa sababu mfumo wa kinga katika miili yao umezorota sana. Kuna maradhi ya utegemezi wa kihisia (co-dependence) ambayo ni maradhi ya kiakili, yanayomfanya mtu kuamini kwamba, bila mwingine kuwepo au kuwa karibu naye, hawezi kuishi. Kwa hali hiyo, siwezi kuwalaumu hawa. Lakini napenda kuwaambia kwamba, wanaumwa. Nadhani siyo vibaya kumkumbusha mtu kwamba, tatizo alilonalo ni maradhi, ili atafute tiba.


  Bahati mbaya kuumwa kwao huko, huwaletea maradhi mengine, mengi sana kwa sababu ya kushuka kwa kinga ya mwili kama nilivyobainisha hapo awali. Ninavyojua ni kwamba, mtu akiwa na wasiwasi na hofu za kila wakati huharibu kinga na mwili wake kila siku unakuwa kwenye maradhi yasiyoisha. Idadi kubwa ya wanawake wenye shinikizo la damu au hata kisukari, ukichunguza utakuta chanzo cha maradhi hayo ni madhila ya ndoa. Kwenye ukoo hawana historia ya maradhi hayo na staili za maisha yao haziwaweki kwenye uwezekano wa kuyapata, lakini wasiwasi na mashaka ya ndoa, ndiyo chanzo.

  Wakati mwingine, mume anaweza kuwa anamwambia mkewe karibu kila siku, ‘nitakuacha mimi’ au‘nitakurudisha kwenu ukiniletea ujinga.’ Mke huogopa na huanza kujiona akiwa hana usalama tena, kwani akicheza atarudishwa kwao. Naye anaamini kurudishwa kwao ni jambo baya kuliko yote maishani. Hebu nikuulize wewe mwanamke. Hivi ni kitu gani kinachokupa hofu kwamba, mumeo atakuacha na kwenda kuchukua mwanamke mwingine? Lakini hata kama akifanya hivyo, hebu niambie, ina maana ni kweli unaamini hutaweza kuishi? Jaribu kufikiri tena upya, kwa sababu kama unaamini hivyo unajidanganya.

  Kumbuka mwanaume huyo anaweza kufa, kama ambavyo wewe unaweza kufa. Hebu fikiria kwamba, mumeo amekufa, ina maana nawe utaona kuishi hakuna maana? Kama ni hivyo, unaumwa, tena unaumwa sana. Unaweza kukuta mwanamke ana ajira yake au ni mjasiriamali aliyesimama kimtaji, na ni yeye mwenye kuilisha familia, lakini anaamini hawezi kuishi bila mumewe. Huu ndio unaitwa utegemezi wa kihisia, sio wa kifedha au kitu kingine.

  Wataalamu wanasema, kati ya vifo kumi vya wanawake ambavyo vinatokana na maradhi yasababishwayo na mateso ya ndoa, vitano vinatoka kwenye utegemezi wa kihisia. Mwanamke anaumwa, analazwa hospitalini hadi anatoka, mume hana habari. Lakini, akitoka yeye ndiye mwenye kuhalalisha mumewe kutoenda kumwona wakati alipokuwa anaumwa. ‘Najua ulikuwa na shughuli nyingi, wala usijali mume wangu, mradi nimeshapona.’Atamwambia mumewe kwa unyenyekevu. Haya ni maradhi mabaya sana na yanahitaji tiba ya haraka kuliko hata Malaria Sugu.
  utambuzi na kujitambua
   
 2. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #2
  Aug 28, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,873
  Likes Received: 6,223
  Trophy Points: 280
  i see. . .
   
 3. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #3
  Aug 28, 2012
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  Duuuh !sasa ngoja nipate coffee kwanza MziziMkavu ..ushauri wako nini...?
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 4. Freema Agyeman

  Freema Agyeman JF-Expert Member

  #4
  Aug 28, 2012
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 3,282
  Likes Received: 1,432
  Trophy Points: 280
  Wengine tuko almost 80% kushinda hayo maradhi ya utegemezi wa kihisia. Ni vita ngumu; ukizingatia inajumuisha mazoea na matakwa ya jamii inayokuzunguka inayotaka uishi itakavyo jamii na si uwezavyo.
   
 5. Eiyer

  Eiyer JF-Expert Member

  #5
  Aug 28, 2012
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 28,238
  Likes Received: 3,669
  Trophy Points: 280
  He!Hii picha ya dada King'ast mmeitoa wapi??Kudadadeki lazima mniambie. . . . . Lol!
   
 6. mayenga

  mayenga JF-Expert Member

  #6
  Aug 28, 2012
  Joined: Sep 6, 2009
  Messages: 3,749
  Likes Received: 545
  Trophy Points: 280
  Thanks Mzizimkavu!
   
 7. cacico

  cacico JF-Expert Member

  #7
  Aug 28, 2012
  Joined: Mar 27, 2012
  Messages: 8,392
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  aiseeee, job true true!
   
 8. ram

  ram JF-Expert Member

  #8
  Aug 28, 2012
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 6,201
  Likes Received: 905
  Trophy Points: 280
  Asante Mzizimkavu, kumbe na huku huwa upo, nilidhani unapatikana JF Doctor tu
   
 9. mito

  mito JF-Expert Member

  #9
  Aug 28, 2012
  Joined: Jun 20, 2011
  Messages: 7,618
  Likes Received: 2,004
  Trophy Points: 280
  Mkuu next time ongeza font kidogo, wengine macho yana shida kidogo, ila thanks for this, nimeipenda mada yako. Lakini hapo kwenye utegemezi wa kihisia,loh ni kazi sana kupashinda, easy say than having it done!
   
Loading...