Trend ya Maisha inabadirika sasa hivi, tulizoea kuona wanaume ndo wanaowalea wanawake tu, sasa hivi si one way traffic tena, wanawake nao wapo kwenye kulea wanaume.Juzi jpili kaja dada mmoja hivi ni meneja sijui kwenye shirika flani la wakimbizi wana ofisi hapa Dar, ana takriban 38yrs maka 40. Sijajua bado background yake lkn alikuwa na mchumba wake, huyu mchumba ni kijana wa miaka kama 26-28, alikuwa anaishi Mwanza, lkn wote ni watu wa MOSHI (CHagga). Huyu kijana background yake si nzuri sana ingawa mzazi wake ni mtu aliyekwenda shule lkn alioa mwanamke ambaye hakwenda shule na malezi ya watoto hayakuwa mazuri sana. Huyu kijana alikuwa anaishi Mwanza na kaka yake, shughuli aliyokuwa akiifanya si nzuri sana, alikuwa mtu wa kupuliza sana Dope (bangi) kupora watu nk. Ikafika kipindi akaokoka akawa anajifunza uchungaji pale Moshi, Ndipo alipokutana na huyu dada ambaye na yeye ni mwokovu(KAMA KWELI). Huyu dada yupo desparate kuolewa na huyo kijana, kamleta Dar anamhudumia kila kitu. Kijana kamwambia yule dada hana pesa za kufanyia harusi dada kapenyeza rupia kampa jamaa millioni 5, ili asionekane hana kitu na sasa kampangishia chumba cha elfu arobaini kwa mwezi pale sinza. Dada kwa kweli amependa kila kijana anachotaka kitafanywa, wasi wasi wangu ni kwamba huenda huyu dada atakuja lia sababu kijana anaonekana kishaona mwanya wa kupata pesa, jana walinipigia simu dada anatafuta nyumba ya kununua kwa 50M, kampa kazi kijana ya kutafuta nyumba, dogo anasema yeye si mzoefu hapa dar, akaniuliza mie wapi house zinapatikana, nikamwambia atulie lkn hakuridhika akasema kwa nini nisimshawishi huyo dada hiyo 50M aiweke kwenye account ya jamaa ili iwe rahisi kununua nyumba pindi ipatikanapo? nikaona mmmh segerea inanukia hapa, nikamwambia awe mpole haya mambo hayahitaji haraka kiasi hicho. Dogo aliacha pombe kwa muda wakati anajifunza uchungaji, sasa hivi yupo town namuona kaanza kulamba Konyagi upyaaaaa na anajificha mchumba wake asigundue. Kule alikokuwa anajifunza uchungaji tayari kanisa limemtenga coz yule dada anataka ndoa iwe mwezi wa saba mwaka huu yaani miezi mitano tu toka wamekutana, wakati Mchungaji alimwambia amchunguze vizuri yule dada na si kuparamia tu, atakuja juta, lkn dogo jeuri ya pesa ya dada imemtia kiwewe, na yeye hasikii wala haambiwi. Nadhani mwanamke na yeye ana preferance zake ni uchumi tu ndo unawabana lkn wangekuwa na uwezo wa kutosha nadhani wangeweza jichagulia mume wnanayemtaka na muda vile vile wa kuolewa au wengine wasingependa kabisa hizi ndoa NDOANO za siku hizi, na wengine wange zaa tu na wanaume ili mradi awe na watoto basi, saa hivi ndicho kinachotokea, wanaanza kuwa na uwezo kwa hiyo wanachagua kipenda roho hata kama kijana ni mdogo ili mradi kampenda na kwenye malovee ana mkuna sawa sawa!!!!!!!!!!!! basi huyo ndo chaguo lake