Wanawake mnawezaje kuishi na mwanaume anayefokafoka?

Mamy K

JF-Expert Member
Apr 30, 2017
2,887
9,997
Habari zenu jamani.

Naomba kuuliza, inawezekana mie nimesahau mafundisho ya shangazi, wanawake wenzangu mnawezaje kuishi na mwanaume anaye fokafoka? Maana mimi naona yamenifika hapa!

Huyu mwanaume amenizidi umri kwa miaka saba, sasa sijui ananichukulia mimi mdogo yake! Yaani nikikosea kitu kidogo atafoka huku ananikata jicho kali, haijalishi kuna dada wa kazi karibu, ni atafoka tu! Huyo dada wa kazi nae anafokewa hadi namuonea huruma mtoto wa watu.

Huwa nanyamaza kisha namtafutia pose zuri namwambia anavyonikwaza ila routine ni ile Ile, nahisi kukonda, kugombana nae siwezi atanibonda nife.

Naombeni mbinu jamani nifanyeje, yamenifika kwa koo mwenzenu?!
 
Habari zenu jamani.

Naomba kuuliza, inawezekana Mie nimesahau mafundisho ya Shangazi....Wanawake wenzangu mnawezaje kuishi na mwanaume anayefoka foka? Maana Mimi naona yamenifika hapa...!

Huyu mwanaume amenizidi umri Kwa miaka Saba, sasa sijui ananichukulia Mimi mdogo ake! Yani nikikosea kitu kidogo atafoka huku ananikata jicho Kali, haijalishi kuna dada wa Kazi karibu, ni atafoka tu! Huyo dada wa Kazi nae anafokewa hadi namuonea huruma mtoto wa watu!

Huwa nanyamaza kisha namtafutia pose zuri namwambia anavyonikwaza Ila routine ni ile Ile, nahisi kukonda.....kugombana nae siwezi atanibonda nife!

Naombeni mbinu jamani nifanyeje....yamenifika Kwa koo mwenzenu!
Kaa kwa kutulia
Tunza ndoa yako acha ujinga wako
Utazoe
Na ukidhubutu kufungua huo mdomo wako utakula kipigo cha mbwa koko
JamiiForums2047296491.jpg


Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Mimi mdomo wangu unaishia jf....naogopa wanaume🤣
Katika yale uliomuahidi mbele ya kitabu kitukufu kuwa nitakuwa nawe kwa shida na karaha, basi jua karaha ndio hizo ndugu yangu , cha msingi jifanye mjinga na potezea na mzoee. Pili mkipata mda mzuri akiwa na furaha mweleze kwa hekima kuwa sio vizuri kunifokea mbele za watu subiri tuwe wawili tu, tatu na mwisho hakuna mkamilifu unaweza ona huyo ni mbaya ila kuna wabaya zaidi so jifunze kuzoea na kumfurahia alivyo utadumu nae daima
 
Una miaka nae mingapi?
Umemzoea au ndoa mpya? Maana kuna kumfundisha kwa jicho uki.wangalia tuu anajua hapa nikomkosea unajua hiyo mbinu. Akijua hilo jicho lako akiona umemtazama tuu atakuuliza nimefanya nini?
 
Hakuna mwanaume anayemfokea mwanamke mpole na asiye na mdomo. jiangalie Sana. anajihami kwa kukufokea baada ya kugundua una kiburi au mdomo pistol.

Mie sio mwongeaji Wala mpigaji. Ila mwaka huu nimeanza tabia ya kumfokea wife. amebaki anaduwaa kuwa miaka 16 yote sijawahi mfokea, imekuwaje Tena? namjibu tu achague mawili, kutuliza kimdomo chake au nimzibue mateke kabisa.

wanawake nanyi mnatubadilisha sana
 
Huko kwenye kumpea hafoki, kwanza sijawahi kumnyima toka anioe....ye mwenyewe anakiri hilo.
Ila hebu fikiria labda namtengea chakula, bahati mbaya wakati naweka glass mezani nikosee hesabu glass ijigonge, jamani atafokaaa, Yani atanifokea Kama mtoto.
Ah mzee baba ana stress za kazini ama ndalama? Maana bwana mwanaume ukikosa hela yaani kitu kidogo tuu ulisha kasirika
 
Ana gubu huyo,, pole,, mpuuze mafokeo yake usiyatilie maanani usiyaweke moyoni japo yanakera na inaonekana ana hasira za karibu sana
Kama ulikuwepo, Yani hiyo akifoka ningekuwa mtu wa kujibu jibu angemalizia na vibao.....Ila huwa nanyamaza, ntaomba msamaha, Ila Moyoni inaniumiza....Mimi ni mtu mzima ni suala la kuelekezana tu.
 
Habari zenu jamani.

Naomba kuuliza, inawezekana mie nimesahau mafundisho ya shangazi, wanawake wenzangu mnawezaje kuishi na mwanaume anaye fokafoka? Maana mimi naona yamenifika hapa!

Huyu mwanaume amenizidi umri kwa miaka saba, sasa sijui ananichukulia mimi mdogo yake! Yaani nikikosea kitu kidogo atafoka huku ananikata jicho kali, haijalishi kuna dada wa kazi karibu, ni atafoka tu! Huyo dada wa kazi nae anafokewa hadi namuonea huruma mtoto wa watu.

Huwa nanyamaza kisha namtafutia pose zuri namwambia anavyonikwaza ila routine ni ile Ile, nahisi kukonda, kugombana nae siwezi atanibonda nife.

Naombeni mbinu jamani nifanyeje, yamenifika kwa koo mwenzenu?!

Achana na hiyo ndoa, kwa nini? Mimi ni mwanaume, sikiliza:

1. Mwanamke akigombezwa hawezi kuwa na mapenzi ya hiyari.

2. Mwanaume anaweza asielewe na akikosa mapenzi ugomvi pale pale.

3. Usipokuwa na mapenzi naye atawaza unabated mtu nje ya ndoa - ugomvi Unaendelea.

4. Ataanza toka nje ya ndoa kwa sababu anaitaji mapenzi!

Achana naye! Hiyo cycle huishia kwenye mauaji
 
Back
Top Bottom