wanawake mbona twaumizana wenyewe?

wanawake mbona twaumizana wenyewe?

Realme

JF-Expert Member
Joined
Jan 12, 2013
Posts
214
Reaction score
155
Nimekuwa nikipita sana JF kama Guest,lakini shida niliyonayo imenifanya leo nijiunge na JF maana mawazo ya members humu jukwaani yamekuwa yakinisaidia sana japo nilikuwa napita kama mgeni.
Nina mdogo wangu kajifungua Dec2012 kwakua alijifungua kwa kupasuliwa waliniomba na Mumewe nije nimsaidie kwa hizi siku za mwanzo. Juzi limetokea tatizo mdogo wangu kapata taarifa rafiki yake wa karibu kajifungu na inasemekana mototo ni wa huyo mume wake, dogo mwanzo aligoma kuamini kwa sababu aliamini huyo dada ni rafiki yake na zaidi ya hapo huyo ndo alimfanya afahamiane na huyo mume na mwanzo alikuwa anamsifia sana amepata mume mzuri. Leo kaamua kuvunja ukimya kamuuliza mumewe mume kakiri ni kweli kazaa na huyo anaeitwa rafiki. Basi toka saa tisa mchana jana mpaka muda huu dogo yupo chumbani na mwanae, shemu yupo hapa amewasha Tv ambayo sina hakika kama anaangalia maana sijjawahi muona asubuhi kama kaamkia TV.chakula nilichooandaa usiku asubuhi nimekuta hakijaguswa na mtu. Hivi nimemtumi sms dogo aamke apate chochote maana akishindana na huyu jamaa atakufa kwa njaa na hivi ananyonyesha,Mgeni mimi nashindwa hata nifanye nini kumsaidia mdogo wangu.ingawa naona yupo katika wakati mgumu sana. Natamani nisingekuwepo kushuhudia haya.
Wanawake kwa nini hatupendani? Unazaa na mume wa mwenzio ukifikiria nini? Kama anakupenda kwa nini hakukuoa maana alikufahamu kabla hata ya huyo mwenzio. Alaf unajiita ni rafiki urafiki gani huo wa kuumizana? Unawaza nini? Na endapo ukafanikiwa ndoa ikafa utaingia wewe?na ukiingia unafikiri kweli utakuwa na amani?wanawake tunajitesa wenyewe maana ninaamini wewe unaezaa na mume wa mtu huna raha yoyote. Na huyo mwanaume hawezi kukuamini kama umeweza kumsaliti unaemwita rafiki lazima atakuwa na wasiwasi na wewe kuwa hata yeye utamzunguka, kama unafurahia ndoa ya mwenzio iyumbe/ife kwa ajili yako ni dhambi, hata kama umetongozwa au umejitongozesha Mume wa mtu ni laana, wamama tusipeane shida.
 
Nafikiri lawama zako zimeenda pasipo.
Wa kulaumiwa ni huyo shemeji yako aliyeapa na kumuahidi Mdogo wako kuwa watakuwa pamoja as mwili mmoja.

That other woman (rafiki) hajaapa chochote, ingawa hajatenda vizuri as a rafiki au a human being. Lkn responsible one ni mume wenu.
Kama mna guts, mconfront na kumsema, sio kumalizia Hasira kwa mtu mwingine.

Mwisho nampa pole sana huyo dada, it hurts sana maana amekuwa betrayed na two people aliowatrust na kuwapenda sana probably. Akitulia atafanya maamuzi yanayomfaa!
All the best!
 
mmh kikulacho......
Nampa pole mdogo wako lakini namshauri aangalie afya yake na mwanae kwanza bcoz kwa kajfungua kwa oparesheni. Akiwa too much stressed atapata physical complications zitakazoathiri kidonda chake.
Mungu amsaidie, ampe hekima ya kulikabili hili na ujasiri wa kukubaliana na ukweli.
 
Ukweli ni mchungu sana kuujua lakimi wakati mwingine tunautafuta
"
Mwizi aliyeiba na akaamua kubadilika kwa hiyari huja kuwa binadamu wa maana kuliko yule ambae hajaona utamu na uchungu wa wizi
"
Tatizo litakuja pale ambapo mwizi huyo hatajutia wala kuona ubaya wa wizi
"
Atakua hatari kwa jamii!
 
Ujue leo jumapili wajameni inabidi nipunguze makali ya comment hii kwa shingo upande!!!!!!!!

1.Adui wa mwanamke ni mwanaume!!!!!!! Huyo shemeji yako ni kitombile mkubwaaa! Yaani anatumbukiza dudu hadi kwa shostito wa mkewe??????/ Laanakum mkubwa huyo! He has no shame at all!!!!!! Mfupa wa aibu umengoka kama sio kuexpire kabisaaa!

2.Hatuwezi jua bwana ukweli wa hili jambo! My take ni kuwa huyo shemeji alikuwa anampenda sanaa huyo dada aliezaa nae ila dogalasi wako ni BF Snatcher aliwachezea tictac hapo akajibebesha mimba na kuzaa afu akaolewa sababu ya mimba na mwenye hisa zake original akagoma kuliquidate! Akasema kama kuzaa ni ujanja hata mimi kizazi ninacho! Ndo kajibu mapigo kama hivo !!!!!!! Na ndio maana hata huyo shemeji amekuwa na ujasiri wa kumwambia kweli ile kule damu yangu!!!!!!

3.All in all kama kazaa tu nje sio ishu kubwa sanaa ila kama ndo anataka kuhamia kule hapo cha cha!!!!!! Lazima dogolasi wako chupi i mbane! Ila Kama imeandikwa ipo basi itakuwepo tu! Wala asijipe pressure!!!!!! Kama yaliyomo yamo huu upepo utapita! Ila kama ndo alifoulisha basi na afoulishe tenaaaa!!!!!!!!!
 
wee mwanamke una akili sana...wanawake mnatekezana wenyewe...mwanamke kutongozwa na kuombwa kugegedwa jamba ccommon na sie vidume ata tukioa bado tutagegeda nje becoz wanawake mnagawa papuchi kirahisi.
 
MMMh,mazito hasa ukiyapitia,mpe pole sana mwambia muhimu kwa sasa ni mtoto na afya yake mume hagombewi sababu wako wengi wakuoa...
 
kwani mume alibakwa na huyo rafiki?

Hebu komeni kuwatupia lawama zote wanawake utadhani mwanamme hana share ya kosa.
 
Nadhani ifike hatua wanaume tulinde familia zetu kuliko kurukaruka nje ambapo tunabomoa sisi wenyewe
 
Realme!
Hujambo? Habari za Kitaa, Habari za uzebaki (hg)?

Tatizo ni kuzaa nje?
Au tatizo jamaa kalowea huko nje?

Mshauri dogo qanza ajiangalie yeye ana upungufu gani;
Nyoka huanza kutafutwa miguuni.
Pili aongee qa upole na mumewe kujua kisa na mkasa,
Inaweza kuwa aliyaingilia mapenzi ya mwenzie; qani sio rahisi hivyo kama adhanivyo.

Qangu mwanamke akijilengesha shurti nigegede qa qenda mbele.
Inawezekana shoga alijilengesha qa shemeji.
​

Uqeli utafutwe qanza;
Ndipo tujue nani wa kulaumiwa.
Lakini maisha lazima yaendelee;
Akiwa ndani au nje ya ndoa.


Bazazi!
​
 
Last edited by a moderator:
kwani mume alibakwa na huyo rafiki?

Hebu komeni kuwatupia lawama zote wanawake utadhani mwanamme hana share ya kosa.

Na pia akumbuke "hawara ni sawa na gari la kuvutwa,haliwezi kuovertake.."
 
afu mie nashangaa

watu wanadhani wanawake hawataki kugegedana kwa utamu mu afu anasepa.

Na hawara hawatongozani.

Na pia akumbuke "hawara ni sawa na gari la kuvutwa,haliwezi kuovertake.."
 
Wanawake ni waoga na dhaifu ndio maana badala ya kucomfront real issue tunatafuta sehemu laini ya kutupia lawama. The devil is her husband; face him ukiweza lkn. Ukishindwa basi laumu hata hali ya hewa kuliko kupeleka lawama pasipo. Maana leo ni shosti, kesho atakuwa Mdogo wako au hata maid wako.
 
You can say that again

Wanawake ni waoga na dhaifu ndio maana badala ya kucomfront real issue tunatafuta sehemu laini ya kutupia lawama. The devil is her husband; face him ukiweza lkn. Ukishindwa basi laumu hata hali ya hewa kuliko kupeleka lawama pasipo. Maana leo ni shosti, kesho atakuwa Mdogo wako au hata maid wako.
 
Wanawake ni waoga na dhaifu ndio maana badala ya kucomfront real issue tunatafuta sehemu laini ya kutupia lawama. The devil is her husband; face him ukiweza lkn. Ukishindwa basi laumu hata hali ya hewa kuliko kupeleka lawama pasipo. Maana leo ni shosti, kesho atakuwa Mdogo wako au hata maid wako.

Kaunga said it all!
 
Last edited by a moderator:
Kosa ni la shemeji yako. Hiyo kitu yake ishindwe na ilegee. Ndio dizaini za wale unasikia baba anatembea na binti yake. Shame on him
 
Back
Top Bottom