Wanawake LIVE kipo hewani..

Wanawake LIVE kipo hewani..

BAI SM

Member
Joined
Nov 16, 2010
Posts
49
Reaction score
33
Kumekuwa na kelele kwa siku nyingi kutoka kwa viongozi CCM kwamba CCM ni chama sikivu na imejitahidi kuleta maendeleo katika nchi, kama unakumbuka ndugu mwana JF, kuna wakati CCM ilianzisha vipindi kwenye TV na RADIO kuonesha maendeleo yalioletwa na chama hicho, na wakawa wanapita mijini tu wakionesha mambo machache machahe bila kuonesha upande wa pili wa maisha kule vijijini.

Joyce Kiria kupitia kipindi chake cha wanawake LIVE ameanza angalau kuonesha Watanzania walio wengi walioko vijijini wanavyoishi maisha ya taabu.

Kipindi ambacho kinaendelea leo pamoja na kwamba anaonesha mambo ya wanawake lakini ni wazi anaweka wazi maisha ya watanzania walio wengi wanavyoishi kama wako jehanamu.

Naamini kwa kipindi hiki ambacho Joice ameamua kuonesha uhalisia wa maisha ya mtanzania kitawapa wakati mgumu wa kutosha watu kama akina Mwigulu ambao kazi yao si kutafuta namna ya kutatua matatizo ya Mtanzania isipokuwa kupambana na watu kama akina Slaa na CHADEMA.
 
joice kanifurahisha sasa watu wajionee jinsi watanzania wanavyopata taabu vijijini.kisha wafananishe na maisha ya vigogo wa nchi hii.
 
Dada nimempenda, huchoki kumsikiliza na anapangilia vizuri maneno yake.!
 
kuna -------- mmoja juz alikua anapuuzia sana hki kipindi na alidiriki kusema akimkuta mkewe anaangalia hiki kipind atampa talaka nikajua ni hawa haw mafirauni hawataki wanawake wakombolewe na nina hakika atakua ametoka zanzibar sababu kule wanawake wa zanzibar sawa na tambara la deki
 
Kumbe wanawake live! kama ni hivyo mi hakinihusu.
 
kuna -------- mmoja juz alikua anapuuzia sana hki kipindi na alidiriki kusema akimkuta mkewe anaangalia hiki kipind atampa talaka nikajua ni hawa haw mafirauni hawataki wanawake wakombolewe na nina hakika atakua ametoka zanzibar sababu kule wanawake wa zanzibar sawa na tambara la deki

Mshaurini mrudi kwa mume wake.
 
:A S-fire1::A S-fire1: dada jitahidi ufike kijijini kwetu Kigera Etuma ujionee wanawake wanavyoishi kwa shida wakati kijiji kina mgodi ambao mpaka leo hautambuliki.
 
Ahahahahhh...
Mkuu kumbe unatokea KIGERA Etuma! Nilipita huko one day, kweli kule watu wanaishi kwa shida

:A S-fire1::A S-fire1: dada jitahidi ufike kijijini kwetu Kigera Etuma ujionee wanawake wanavyoishi kwa shida wakati kijiji kina mgodi ambao mpaka leo hautambuliki.
 
Umesahau msemo unaosema, ''ukiona cha nini wenzio wanajiuliza watakipata lini''

nelly.jpg

Mbele ya kasisi

harusi1.jpg

Mmmh, hapa wapi tena?
 
Back
Top Bottom