Wanawake Lindeni Afya Zenu

Wanawake Lindeni Afya Zenu

Mara nyingi ukisikia Takwimu za waathirika wa UkIMWI wanawake wanakuwa kwa idadi kubwa kuliko sisi wanaume, hata magonjwa ya zinaa mengine ni hivyo hivyo hii kwa asilimia kubwa hutokana na Uzembe kwa upande wa wanawake na wengi hawafahamu kuchukua tahadhari hasa linapokuja suala la ngono.

Wanawake wengi hawana maamuzi kabisa katika suala la kutumia kinga, yani mwanaume wewe ndiye utakayeamua utumie kinga ama usitumie, yeye mwanamke usipotumia sawa ukitumia sawa, hata kama ni udhaifu suala la afya yako mlinzi wa kwanza ni wewe mwenyewe bila kujali jinsia yako, nilazima uwe na uwezo wa kuchukua tahadhari juu ya afya yako.

Hasa hawa mabinti wenye miaka 16-25 nilazima wafundishwe jinsi ya kujilinda bila hivyo tutakuwa na wakati mgumu sana katika kutokomeza UKIMWI. asanteni
Nadhani takwimu hizi ni kwasababu wanaume wengi hawapimi hiv, wanawake inawalazimu kupima hasa nyakati za ujauzito.
 
Nadhani takwimu hizi ni kwasababu wanaume wengi hawapimi hiv, wanawake inawalazimu kupima hasa nyakati za ujauzito.
Sasa mke wako akikutwa nao si atakuambia au akikuambia wewe utakufa kiume hutataka kutumia ARV au nin🤓 Ukimwi haujifichi bila kutumia dawa utakuumbua na huwezi kupata dawa bila kupima.
 
Wanawake wengi sana ni wagonjwa wa magonjwa ya zinaa, wenyewe wakijisikia homa kidogo wanakimbilia kutibu UTI... Bin'adamu hampo salama
 
Watoto wa siku hizi wanaogopa sana mimba kuliko UKIMWI, na wanajisahau kama kuna homa ya ini inayokula kwa njia zile zile za UKIMWI na bonus ya majasho, magonjwa ya zinaa nayo
 
Back
Top Bottom