NEGLIGIBLE
JF-Expert Member
- Feb 3, 2011
- 354
- 92
Jana katika pitapita zangu nilikutana na mwanamke aliyebeba mtoto mgongoni akiomba msaada kwa wasamaria wema ili mtoto wake akatibiwe malaria.yule mama alikuwa akilalamika kuwa mtoto wake pamoja na yeye hawakula toka jana,baba wa mtoto kamkimbia.nilipojaribu kumdadisi zaidi nikagundua kuwa yule mama hajui hata nyumbani kwa mzazi mwenzie..........mara nyingi pia nimeshuhudia ombaomba wakiomba msaada barabarani,lakini cha kushangaza ni kuwa unaweza kukuta mama anayeomba msaada barabarani ana watoto watatu wadogo.sasa unajiuliza hivi kweli mtu huyo yuko `responsible`?kwani ,kwa mfano unapofikiria kuzaa usifikirie pia jinsi ya kulea watoto wako?nani anapaswa kukulelea watoto wako?unaweza kukuta huyo msamaria mwema unayemuomba msaada yeye ana mtoto mmoja sio kwa kupenda ila ugumu wa maisha.kwa nini mnajirahisi hivi?