Wanawake kumbaka mwanaume inawezekanaje? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wanawake kumbaka mwanaume inawezekanaje?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Miranda, Oct 12, 2010.

 1. M

  Miranda Member

  #1
  Oct 12, 2010
  Joined: Oct 7, 2010
  Messages: 50
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Wanawake Watatu Wambaka Mwanaume Zimbabwe
  [​IMG]
  Sunday, October 10, 2010 4:35 AM
  Wanawake watatu wanatafutwa na polisi nchini Zimbabwe baada ya kumteka mwanaume na kisha kumbaka kabla ya kumtelekeza pembeni ya barabara baada ya kumuibia pesa zake.Mwanaume mmoja mwenye umri wa miaka 26 wa nchini Zimbabwe amebakwa na jumla ya wanawake watatu ambao walimteka baada ya kumlewesha kwa madawa ya kulevya.

  Polisi wa Bulawayo walitoa taarifa ikisema kuwa mwanaume huyo aliwekewa madawa ya kulevya kwenye kinywaji chake na alipopoteza fahamu wanawake hao waliifunga na kamba mikono yake na kuondoka naye.

  Mwanaume huyo aliripotiwa na polisi akisema kuwa wanawake hao walimbaka mara kadhaa na baadae kumtelekeza pembeni ya barabara baada ya kumuibia kiasi cha dola 300 alizokuwa nazo mfukoni.

  Tukio la kubakwa kwa mwanaume huyo kumepelekea idadi ya wanaume waliobakwa mwaka huu wafikie watano.
   
Loading...