stephot
JF-Expert Member
- Mar 1, 2012
- 17,746
- 27,217
Kumekuwa na matatizo makubwa sana ya mizozo ndani ya ndoa,kudharauliana,kujibishana,kutukanana na hata kukashifiana,hili jambo mnapoanza urafiki mpaka kufika mnaoana huwezi kulikuta au inaweza chukua hata miaka kadhaa 2-3 kukiwa shwari kabisa,katika udadisi nilioufanya nimegundua kuna kundi kubwa la wanaume walio kwenye ndoa wakilalamika kuwa wanawake ndio chanzo kikubwa cha mambo haya na hili linatokea immediately baada ya kuanza kuzaa,kwani wanawake huhamishia mapenzi kwa watoto na kuona wanaume ni kama mizigo tu kwenye familia na hawahitaji kuendelea kupata special treatment kama ilivyokuwa hapo awali,tufunguke kwenye hili wadau nani hasa anastahili lawama na nini kifanyike kuepukana na hii mifarakano kwenye ndoa inayosababishwa na wanawake?