Wanawake kujisahau wanapokuwa kwenye ndoa

Wanawake kujisahau wanapokuwa kwenye ndoa

Da King'asti..ndio maana mimi nina filosofia ya 'mapenzi huisha', kwa sababu mbali mbali. Haijalishi ni sababu gani, iwe ya mume au mke au both...but it is a reason enough kumaliza mapenzi, na mapenzi yanapoisha ndio kunabaki kuvumilia na mazoea. Sasa hapo ndio tunapotofautiana...wengine wanaweza vumilia longer, wengine mazoea tu maisha yanaendelea..na wengine ndio hawawezi hiyo 'biashara'. Na kwa wasioweza hapo ndio inafuata kuflirt, kucheat, na kwa wasio wastaarabu even masengenyo, magomvi, na pengine mpaka kudhuriana mwili!

Sa kisa nini husubiri mpaka mfikie 'extreme'!? Ukiona mapenzi yameisha....chapa lapa! Kwani umezaliwa naye huyo!?
Kweli ndoa ndoano,ukiingia umeingia, kumbe penzi huwa linaisha!ila jamani kuna wanaopendana japo umri umekwenda hadi unatamani,yani penzi tamu mwanzo mwisho.
 
Mnapokua na familia ni tofauti na mlivyokua peke yenu,mama kama mama lazima awe busy na mtoto,we baba zima unataka ufanyiwe kila kitu,kwanza mwanaume wapaswa kumsaidia baadhi ya kazi mkeo,sio mpende dezo coz hata mke anachoka na hakuna kazi ngumu kama kulea!
 
Pole weeee!

Women need affection from there husband... Mjali mkeo, mpe mapenzi ya dhati (si maanishi tendo la ndoa).

Matatizo mengi saana yanaanzia hapo.. Humjali mkeo.. Unazurura katika mabaa daily. Unafikiri ulimwoa aje akulindie nyumba.

Mke akiwa na kiburi, kashfa na dharau kwa mumewe kuna sababu haiji from no where (though si support hii hata kidogo).

Mpende mkeo, pata muda wa kukaa na familia yako, msaidie katika kulea watoto, wacha ubabe na manyanyaso yasiyokuwa na msingi then kila kitu kitakuwa Mswanoooooo..



Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
ki ukweli kuna baadhi ya wanaume hupunguza mapenzi pale wake zao wanapoanza kuzaa na kukimbia majukumu na kuona hao watoto kama wanampa kero.Hivyo suluhisho anaona ni kutafuta ka small house baada ya kusaidia majukumu ya ulezi na mengineyo ili upendo uendelee kudumu.mh ki ukweli wamama wanastahili pongezi na kuheshimiwa wanabeba majukumu makubwa ktk ulezi na familia kwa ujumla.
 
Ndomaana pakawepo na nyumba ndogo, za kati na kubwa. lol
 
Siyo kwamba wanawake ndio wanaharibu ndoa, bali kwa muda huo inawawia vigumu kuyatimiza yote kama awali.

Hebu fikiria mwanamke anakaa na mtoto toka asubuhi mpaka jioni halafu ukizingatia watoto wanavyosumbua unadhani atakuwa anastahili lawama yoyote katika hilo, ukizingatia alikuwa anafanya kazi muda wote? Mtoto akilia tu, mama huyo.

Ikifikia hapo inatakiwa mwanaume na yeye amuelewe mkewe, aangalie kazi ambazo mkewe anazifanya toka kulipo kucha mpaka kunapokuchwa.

Kwahiyo hata akipata mara moja moja haina shida.

haya ndo majibu ya mwanaume wa ukweli anayeelewa ndoa ni nini
 
Back
Top Bottom