Ipo tofauti kubwa kati ya mwanamke mwenye tabia mbaya kwa asili na mwanamke anayevutwa na mazingira kufanya mabaya. Kwa kusoma hadithi hii inaonesha kuwa mwanamke hakuwa mbaya kivile isipokuwa alishawishiwa na mashost baada ya kuona Franco yuko Loose kupita kiasi. Hata baada ya kujua kuwa huenda mkewe anarubuniwa hakuchukua hatua stahiki. Angaliweza kumuonya, kumwadhibu au kumwacha mapema akatafuta wife material siyo huyu manung'ayembe, angalionekana ni mwanaume sio huyu wa kulialia bila kuchukua hatua. Ubowa wa adhabu ya kisaikolojia ni kwamba inakuumiza pia wewe mwenyewe. Angalia Franco alianza kukosa usingizi na kuwa mlevi wa wine, wakati awali ilikuwa siyo hivyo. Hii ni matokeo ya ugonjwa wa msongo wa mawazo (stress). Halii isipotibiwa unakuwa kichaa kabisa na inawezekana usitibike. Kjunju, kwa nini utoe adhabu ambayo inakuumiza zaidi wewe kuliko unayemwadhibu?