Wanawake angalieni hili

sasa ilikuwaje wakati mnaviziana na jamaa. Ulitumia vigezo gani kumwamini na alitumia mianya ipi kukupata

nilishawahi kuzungumza humu .............hakunipata mpaka aliponioa.......nafikiri nimeeleweka
 
bora mwanaume anaoshwa uso ndugu, tena sehemu zingine zote zimezibwa kikamilifu. sasa unaweza kulinganisha na mwanamke kuchezewa unyanyo hadi mapaja?
 
nilishawahi kuzungumza humu .............hakunipata mpaka aliponioa.......nafikiri nimeeleweka
labda sijaona huko ulikozungumzia. si wengine bwana tunaogopa kuuziwa mbuzi kwenye gunia kwa namna dunia inavyoenda. unaonaje ukiniunganisha na mdogo wako maana mko damu moja-ya kukwepa mishale
 
Nini Mpenzi hata mke ; ni aidha anajieleza na kuapa kutorudia ama ndoa ndio kwishnei; maana anaweza kuwa amaeingia mkenge wa kiuga ukisasa kaka kasuku!
mkuu akishanogewa na mikono ya mpaka rangi atakuapia kwa miungu yote lakini mwisho wa siku atamwambia mpaka rangi watafute chimbo lingine akamsugue miguu vizuri
 
Naomba nijinukuu. Katika pitapita zangu nimefanikiwa kuona hawa wapaka rangi siku hizi wakiwa kwenye vibanda vyao ama katika saluni za kike ama kwenye maduka ya kuuzia urembo. Naona kweli hatua moja inaanzisha nyingine. Cha msingi tu wadada angalieni na mipaka ya kurembeshwa, maana wengine mahusiano yenu yana dosari sasa bahati mbaya kijana kajaliwa kuchezea miguu hiyo, basi isiwe tiketi ya kusema, 'bwanae...ka mbuai, mbuai bwana!'
 

Sister usicheze kabisa na mambo haya, tumeona wengi tuu wenye tabia njema wakiingia majaribuni.
 
Hahaaa. Sawa ipo na sio sawa pia ipo.

Sawa inakuwepo ikiwa mwanamke anayeoshwa hizo kucha atajistiri vizuri pasi kumshawishi muoshaji na sio sawa ikiwa anayeoshwa kavaa nguo zenye kumuacha uchi baadhi ya maungo yake ambapo kwa walio wengi huwa zinaleta ushawishi kwa waoshaji.

Pia nimalizie kwa kusema urembo wa miguu hata sisi wanawake tunaweza kuwa nao pasi kutegemea hao vijana.
 
Ila si sawa
 
Mke wa mtu mwenye akili nzuri hawezi kufanyiwa hivyo.

Hawa wadada aliowatolea mfano naimani hawajaolewa.

Mkuu hadi hapo inaonyesha ww hutokei katika mkoa mkuu...

katika huu mkoa mkuu ukiingia mtaani huwezi kutofautisha kati ya mke wa mtu ,,kicheche,,,mdangaji,,, sometimes hata changudoa

na hata kwa sisi wanaume ni hivyo hivyo katika huu mkoa mkuu huwezi fananisha baba wa familia na bachelor...muhuni...kibaka...kivulana sijui kuna tatizo gan katika huu mkoa mkuu

hope huko mikoani mambo yapo shwari
 
Kuna dada mmoja ni mke wa mtu tuliwahi kufanya ofisi moja.Alikuwa anashindwa kabisa kufanya kazi siku aki wa miss waosha miguu.Kila wakati alikuwa akizungunzia ana hamu ya kuoshwa miguu.
Nilipomuuliza kulikoni anakuwa obsessed na shughuli hiyo,alikiri huwa inampa raha hadi anapata orgasm.
No liashangaa sana.Waacheni tu wake zenu waende enyi wanaume wa Dar!
 
Sijasema iko shida ila namna ya ukaaji wakati unafanyiwa hivyo.

Ila hata mwenyewe unaweza ukajiosha na kuonekana mrembo.
Ukaaji wake ni mzuri labda kama hao wameamua tu kukaa hivyo, unapewa taulo kubwa la kujifunika tena safi kabisa ambalo hajatumia mtu mwingine. Pia kuna saluni nzuri za kufanyiwa sio kama hao pichani naona kama wako barabarani
 
Ila si sawa
Hahaaa. Nyie ndio mnalichukulia ni jambo zito.

Cha muhimu na kinachotakiwa kupigiwa kelele ni hao wanawake kujitambua tu na kujua wao ni kina nani. Sababu usafi muhimu Mkuu.

Na hatuwezi kusema si sawa wakati kiuhalisia wateja wao ni wengi kupita kiasi.
 
Kwa kweli hapo hata mimi napata wakati mgumu sipati picha ya wanao paka rangi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…