Wanawake acheni kuvaa mawigi

Wanawake acheni kuvaa mawigi

Sonko Jr.

JF-Expert Member
Joined
Oct 10, 2015
Posts
806
Reaction score
320
Mwanamke anapendeza na kuvutia zaidi anapokuwa na nywele zake za asili wala sio mawigi. Hiyo ni FACT.

Mawigi yanaboa na yanatupunguzia hisia, mfano pale mwanaume unavyozishika au kujaribu kuzichezea halafu unajua kabisa hizi nywele sio.

Ni kama likofia fulani hivi linalovaliwa au kushonwa kichwani kwa mwanamke, ambayo pamoja na kwamba KIUHALISIA halimuongezei mwanamke mvuto (hata kama ni la Laki Moja), linatakiwa libadilishwe kila baada ya muda fulani.

Wanawake bakini na nywele zenu za asili, zipeni matunzo na usafi wala hamna haja ya kuhangaika na kubadilisha mawigi maana wanaume {99.99%} hatuzipendi. Zinaboa hata kuangalia.

Cha kushangaza, utamkuta mwanamke wa kibongo eti naye anahangaika kuweka liwigi lake vizuri kanakwamba linamzuia kuona vizuri wakati ni FAKE HAIR na yeye mwenyewe kaliweka hivyo kwa makusudi kuiga Wazungu.

Say NO to Fake Hair.
 
Aiseehhh mimi huwa nakerwa zaidi nahisi, yani mimi na mama watoto wangu ndo ugomvi kila kukicha,namkataza lakin wapi,unakuta wigi la rangi sijuwi kijani, sijuwi pink yani hakuna relation na uhalisia wa nywele za binadamu, siyapendi mawigi na sipendi kumuona alady amevaa
 
Aiseehhh mimi huwa nakerwa zaidi nahisi, yani mimi na mama watoto wangu ndo ugomvi kila kukicha,namkataza lakin wapi,unakuta wigi la rangi sijuwi kijani, sijuwi pink yani hakuna relation na uhalisia wa nywele za binadamu, siyapendi mawigi na sipendi kumuona alady amevaa

Ni kutojitambua tu, mawigi ni ulimbukeni
 
Hata mimi ndo ugomvi wangu wa mawigi. Nikiona mtu amevaa huwa nashindwa kuona uhalisia wa nywele. Sipendi wig.
 
Wewe nani uwape amri kutovaa wigi? Labda uongee na rais atangaze NO Wigs, nje ya hapo unajipa presha bure kwa mambo yasiyokuhusu. Ila kwa habari ya mkeo muombe asiweke hizo nywele

Hii sio amri ni ushauri ukizingatia kuwa hazikuongezei mvuto wowote

Ungebaki na nywele zako ungevutia zaidi, hujui tu
 
Ha ha ha ha imebidi nicheke mi pia haya madudu kwangu ni tatizo kubwa sana
 
Teh teh..Yani sometimes unakuta msichana anageuka kuangalia upande mwingine ila wig limebaki straight tu..halijafwata direction ya kichwa...

Hahaaa wakati mwanamke anapochana wigi lake zinadondoka chini, ukiwa karibu naye zinakudondokea
 
Masomo English medium kituo cha grecious ni bora na watoto wanamwelewa mwlm sana
 
Hii sio amri ni ushauri ukizingatia kuwa hazikuongezei mvuto wowote

Ungebaki na nywele zako ungevutia zaidi, hujui tu

Unalazimisha sasa, ushauri haulazimishwi wala Ombi halilazimishwi. Kila mtu anacho anachotaka na sio lazima kimvutie mwingine, huna cha kufanya mtu akiamua kuvaa wig labda awe mkeo utamvua maana wengine hawajali kama huvutiwi
Mara nyingi wanawake wanashindana wenyewe maana hakuna mwanaume anayejua wigi la human hair au la laki 3 ila mwanamke mwenzie atajua na kumsifia. Sio mara zote lengo wewe uvutiwe so yanakuwa hayakuhusu
 
Back
Top Bottom