Wanausalama ni watu muhimu sana

Wanausalama ni watu muhimu sana

Ndio wanausalama ni watu muhimu sana hapa nikimaanisha majeshi yote kwa nchi yetu mfano JWTZ, jeshi la
Polisi, Usalama wa Taifa...nk

Hawa watu wanahitaji sana maombi yetu na upendo wetu wakienenda katika yaliyo haki i mean kulinda mipaka ya nchi, rasilimali za nchi pamoja na sisi raia.

Ndio ogopa sana mtu aliyekula kiapo cha kufa kwa ajili ya kukulinda wewe na nchi yako, hebu fikiri wakati wewe umejficha ndani ya bomb shelter/bunkers hawa jamaa watakua frontline wakikabiliana na adui uso kwa uso.

Bila kujali adui ana silaha gani za kisasa ila tambu hawa wana usalama wetu ndio watakua wanapambana nao, chukulia mfano vita ya Kagera wanausalama wetu walijitoa kwa ari na mali kuipambania nchi yetu.

Heshimu sana mtu wakati wewe umelala fofofo yeye yupo macho na silaha nzito mkononi kuhakikisha unalala salama bila usumbufu wowote akipigwa na baridi kali hata kama kuna barafu

Mfano naangalia pale Ukraine wakati huu kuna barafu kali na baridi ila wanajeshi wa Ukraine bado wanapambana kwa ajili ya nchi yao wote wakike nawa kiume.

Nao kama binadamu wana mapungufu yao ila wanayoyafanya ni makubwa sana bado wanahitaji Upendo na sala zetu kwa wingi.

Ndio heshima ziende kwa vyombo vyote vya ulinzi vinavyohakikisha nchi yetu ipo safi mpaka leo natambua sio kwamba nchi yetu haina maadui ila kwa weledi wenu mnawatambua mapema na kudili nao mapema.

#Hongereni sana

Ni mimi mpenda amani na raia mwema....
Panapo kuja kuharibu ni pale wana siasa wanapokuja na maamuzi yao ya kushibisha matumbo yao wakati kuna wengine wanajitolea uhai kuzilinda rasilimali za nchi kwa damu na jasho. Inaumiza na kusikitisha sana.
 
Ukiona gari lao usisahau kuwasimamisha na kuwapongeza kwa kazi nzuri ya kutulinda
 
Furaha Yao sio pesa .
Furaha Yao ni utekelezaji.
Mnapata Viburi vya kutukana humu Kwa sababu Nchi yetu ni Salama, wapo wanaume kule wanafanya kazi yao Kwa weledi.
 
Furaha Yao sio pesa .
Furaha Yao ni utekelezaji.
Mnapata Viburi vya kutukana humu Kwa sababu Nchi yetu ni Salama, wapo wanaume kule wanafanya kazi yao Kwa weledi.

Wangejua basi tu binadamu tumeumbiwa kusema
 
Panapo kuja kuharibu ni pale wana siasa wanapokuja na maamuzi yao ya kushibisha matumbo yao wakati kuna wengine wanajitolea uhai kuzilinda rasilimali za nchi kwa damu na jasho. Inaumiza na kusikitisha sana.

Kabisa sana kiongozi ila yana mwisho yote hayo nahakika kama vitendo hivyo vipo na taratibu hazifwati ipo siku wana usalama wetu watachoka na kuwaweka hadharani wahusika
 
Umuhimu gani nchi inaibiwa menyewe yapo kutishia abiria kwenye mwendokasi

We shukuru unakula na kulala mengine yaache kama yalivyo kiongozi dont dig deep na mengine kama huyafahamu hata kukaa kimya ni busara pia
 
Taabu ya wengi uliowataja hapo rushwa ... Labda hawakuathiri wewe kwa sababu ya undugu ulio nao wewe nao au na walamba asali?

Hakuna rushwa kwenye kulinda amani na mipaka ya nchi na kwanini wewe utoe rushwa.

Unafahamu kwamba mtoa na mpokeaji rushwa wote ni wa kusukumia ndani
 
We shukuru unakula na kulala mengine yaache kama yalivyo kiongozi dont dig deep na mengine kama huyafahamu hata kukaa kimya ni busara pia
Kabisaa ukitaka kuamini uende mikoa ya pembezoni mwa nchi hasa kigoma utaelewa tunalo lisema hapa. Mimi kilio changu ni kwa wana Siasa wanao sahau yakuwa Nchi ina walinzi ambao wamejitolea maisha yao kwaajili yetu sote.
 
Mm pia napenda Sana kulinda ili maisha Yangu yawe Safi kabsaa ,na nlinde wengne wakat wa vita
 
Ya
Yes Boss Kila mtu ni muhimu kwa nafasi yake ila ogopa mtu aliye tayari kufa kwa ajili ya wengine sidhani kama mwl au dr kaweka uhai wake rehani kama mwanajeshi au polisi na huyo mwl, dr, mkulima anafanya kazi zake kwa amani kwa sababu ya wanausalama.

Pesa sio kitu ndani ya uhai kiongozi

Ushawahi sikia mlio wa mizinga wewe omba Mungu sana usije kusikia
Yanapotokea magonjwa ya milipuko mfano corona na ebola mtumishi wa afya anahatarisha maisha yake,waandishi wa habari za uchunguzi wapo hatarini pia,Ulishawaza usalama wa vijana wanaopandisha material ghorofani wakati wa ujenzi?
 
Daktari anakula kiapo cha kutunza siri za wagonjwa na sio kutoa uhai wake kwa ajili ya wagonjwa.

Umeona wale wameguswa kidogo tu Mirembe wameanza kulalamika je ukimpeleka frontline kwenye vita si ndio atakimbia kabisa
Vipi usalama wa afya zao yanapotokea magonjwa ya milipuko mfano corona na ebola?
 
Ya

Yanapotokea magonjwa ya milipuko mfano corona na ebola mtumishi wa afya anahatarisha maisha yake,waandishi wa habari za uchunguzi wapo hatarini pia,Ulishawaza usalama wa vijana wanaopandisha material ghorofani wakati wa ujenzi?

Tukubaliane dr anakula kiapo cha kulinda siri za mgonjwa na sio kufa kwa ajili ya mgonjwa hiyo inatokea kama bahati mbaya ndio maana wanavaa Protective Gear PPE sijui gown, gloves, mask, boot...nk na pia wengine wanapata na chanjo kabisa kabla hawajaanza kudili na hizo outbreak tofauti na mjeshi au polisi anayepambana na mtu aliyeshika kitoa uhai Bunduki au Bomu au mizinga.

Ndio maana ratio ya Drs wanaokufa kwenye outbreak na wanajeshi wanaokufa vitani ni tofauti kabisa.
 
We shukuru unakula na kulala mengine yaache kama yalivyo kiongozi dont dig deep na mengine kama huyafahamu hata kukaa kimya ni busara pia
Nayafahamu mengi kupita kiasi na tunaumia zaidi kuliko unifikiriavyo
 
Vipi usalama wa afya zao yanapotokea magonjwa ya milipuko mfano corona na ebola?

Blaza ogopa unapambana na mtu ambaye naye nia yake ni kutoa uhai wako ndio maana tunaambiwa principle see your enemy before your enemy see you ukiruhusu awe wa kwanza kukuona umekwisha.

Real utalinganisha Mwanajeshi anayepambana na Taleban au Alqaida na Dr anayetibu Cobid au Ebola huku umevaa Full PPE and you work in calm area huku yule anakwepa risasi na landmines za kutosha
 
Ushahidi upi unautaka wewe, au unafikiri tupo gizani kama miaka ya nyuma ? Mengine tunashuhudia kwa macho yetu na kuona rasilimali za nchi zinavyokwenda na tunatoa taarifa kwa wakubwa zetu na bado hawawezi kuchukua hatua
Ushahidi unao?
 
Namshukuru Mungu pekee ambae sio mnafiki na wala hachoki kukupenda na mpenda haki, mangapi tunaripoti na hayachukuliwi hatua tena mengine ni hatari kwa taifa letu tuliloapa kulilinda kwa gharama yeyote ile
Ungefahamu mengi ungewashukuru wachapakazi hawa.
 
Back
Top Bottom