Wanausalama ni watu muhimu sana

Wanausalama ni watu muhimu sana

Life2

JF-Expert Member
Joined
Jun 8, 2016
Posts
3,377
Reaction score
4,847
Ndio wanausalama ni watu muhimu sana hapa nikimaanisha majeshi yote kwa nchi yetu mfano JWTZ, jeshi la
Polisi, Usalama wa Taifa...nk

Hawa watu wanahitaji sana maombi yetu na upendo wetu wakienenda katika yaliyo haki i mean kulinda mipaka ya nchi, rasilimali za nchi pamoja na sisi raia.

Ndio ogopa sana mtu aliyekula kiapo cha kufa kwa ajili ya kukulinda wewe na nchi yako, hebu fikiri wakati wewe umejficha ndani ya bomb shelter/bunkers hawa jamaa watakua frontline wakikabiliana na adui uso kwa uso.

Bila kujali adui ana silaha gani za kisasa ila tambu hawa wana usalama wetu ndio watakua wanapambana nao, chukulia mfano vita ya Kagera wanausalama wetu walijitoa kwa ari na mali kuipambania nchi yetu.

Heshimu sana mtu wakati wewe umelala fofofo yeye yupo macho na silaha nzito mkononi kuhakikisha unalala salama bila usumbufu wowote akipigwa na baridi kali hata kama kuna barafu

Mfano naangalia pale Ukraine wakati huu kuna barafu kali na baridi ila wanajeshi wa Ukraine bado wanapambana kwa ajili ya nchi yao wote wakike nawa kiume.

Nao kama binadamu wana mapungufu yao ila wanayoyafanya ni makubwa sana bado wanahitaji Upendo na sala zetu kwa wingi.

Ndio heshima ziende kwa vyombo vyote vya ulinzi vinavyohakikisha nchi yetu ipo safi mpaka leo natambua sio kwamba nchi yetu haina maadui ila kwa weledi wenu mnawatambua mapema na kudili nao mapema.

#Hongereni sana

Ni mimi mpenda amani na raia mwema....
 
Sisi walima nyanya wenye kujidhania nasi ni muhimu kumbe bure kabsaa, tuna comment wapi ndugu mwana usalama?

Hata mimi ni mkulimwa wa Nyanya ntole kiongozi ila kungekua hakuna usalama sidhani kama kulima na kuuza nyanya zetu na kujipatia kipato vingewezekana
 
Kila mtu ni muhimu kwa nafasi yake,hao wanaolinda mipaka wanalinda bure(bila malipo)?

Yes Boss Kila mtu ni muhimu kwa nafasi yake ila ogopa mtu aliye tayari kufa kwa ajili ya wengine sidhani kama mwl au dr kaweka uhai wake rehani kama mwanajeshi au polisi na huyo mwl, dr, mkulima anafanya kazi zake kwa amani kwa sababu ya wanausalama.

Pesa sio kitu ndani ya uhai kiongozi

Ushawahi sikia mlio wa mizinga wewe omba Mungu sana usije kusikia
 
Natamani niwe mmoja wa hao kwaajili ya taifa langu,inahitaji ujasiri na moyo wa kujituma.

Mungu awapiganie na kuwalinda kwa huduma yao.
 
Mnajipa umuhimu tu, hakuna aliye bora kila mtu ni muhimu kwenye kada yake, tusemaje kuhusu madakatari?..

Kiongozi huyo dr ili kazi zake ziende vizuri iwe kufanya C/section, kutek history, kufanya normal delivery, myomectomy, lazima pale na usalama kwanza umeona Madr wa Ukraine wanavyofanya kwenye mazingira magumu wanafanya C/section kwa tochi simply hakuna usalama
 
Uhai wako au usalama wako una thamani ya sh ngapi? Ukipata jibu utajua kwamba hata hiko unachosema wanalipwa ni sawa na bure tu

Shida binadamu tunadhani pesa ndio kila kitu pesa hazinunui Uhai wanashindwa kutambua hilo waulize wanafamilia ambao vijana wao shupavu walipoteza maisha wakiipigania nchi wakati wa vita vya Uganda kama pesa zimeweza kurudisha uhai wa wapendwa wao
 
Huko ni kujipa umuhimu tu, kwani wanafanya bure? Si wanalipwa?..miaka hiyo tulipigania kuingia huko kwa sababu kuna mshahara

Daktari anakula kiapo cha kutunza siri za wagonjwa na sio kutoa uhai wake kwa ajili ya wagonjwa.

Umeona wale wameguswa kidogo tu Mirembe wameanza kulalamika je ukimpeleka frontline kwenye vita si ndio atakimbia kabisa
 
Hata mimi ni mkulimwa wa Nyanya ntole kiongozi ila kungekua hakuna usalama sidhani kama kulima na kuuza nyanya zetu na kujipatia kipato vingewezekana

Taabu ya wengi uliowataja hapo rushwa ... Labda hawakuathiri wewe kwa sababu ya undugu ulio nao wewe nao au na walamba asali?
 
Back
Top Bottom