Innocent Kirumbuyo
JF-Expert Member
- Jan 1, 2014
- 4,647
- 4,495
Wanaume wote Mungu awabariki sana, maana mna mioyo ya kipekee sana kwenye mahusiano;
Nilishasimuliwa na nikaona kwa macho yangu mwenyewe, vijana wanawapenda wapenzi wao mpaka kufikia hatua ya kuwasomesha kwa pesa zao, ila huko huko shuleni wanakowapeleka hao wapenzi wao huwa wanapata vijana wengine wa kuwapenda zaidi yao na wanapomaliza shule huwa wanakuja na jibu moja tu, siwezi kuolewa na mtu asiyekuwa na elimu.
Kipindi anaamua kukusomesha hukusema huwezi kusomeshwa na mtu ambae hajasoma, dunia duara! Hongera sana kijana ambae uko na moyo kama wangu, uliyetayari kutoa figo yako kwa ajili ya kunusuru maisha ya mapenzi wako, wakati yeye hawezi hata kukuchangia damu ukiwa umepungukiwa.
Tusaidiane kujipa moyo huku tukiwa kama mishumaa iliyo tayari kuangazia watu ikiteketea.Kuna siku nitawafafanulia mambo mawili niliyoyachunguza;
(1)Kwanini baba yangu alikuwa akiombwa pesa ya matumizi na mama, alikuwa anaenda nyuma ya nyumba na kuzibagua pesa kabla ya kurudi na kutoa.
(2)Kwanini mwanaume anatia mimba siku moja na mwanamke analea mimba miezi 9 ila mtoto akizaliwa jina la mwisho anapewa na baba.