Peculiar
JF-Expert Member
- Apr 5, 2015
- 821
- 689
Wanawake wengi ni wavumilivu na ni wasiri mno.
Wapo wanaopigwa,wapo wanaonyimwa pesa ya matumizi,wapo wanaingiziwa vimada ndani ya nyumba,au kushuhudia mumewe na kimada.wapo wanaonyimwa unyumba.
Wapo wasioshea vitanda.wapo wanaoingiliwa kinyume na maumbile.
Yaani wake zetu wamekuwa ni watu wakulia tu ndani kwa ndani.wengi wanajuta kuolewa.
Na yote haya sisi wanaume ndio chanzo.
Lakini bado,wanatupikia,wanafulia,wanatunza nyumba.wanatembelea ndugu zetu. Hawasemi yanayowasibu ndani ya nyumba zao.
Hebu tufikiri upande wa pili.
Sisi pia tuna dada zetu tunaowapenda. Sisi pia tuna watoto wakike tunaopenda kuona wakiwa na furaha muda wote.
Hivi tutajisikiaje tukigundua dada zetu na mabinti zetu wanateswa na waume zao?
Wengi wanatembea wanacheka,wameshikana mikono barabarani!
Ila ukiambiwa wanawake wanavyofanyiwa na hao wanaume,huwezi amini!
Wanaume tuishi kwa akili na wake zetu.
Wanawake wana mengi yanayowashughulisha jamani!
Tuwapende tuwasaidie na tuwahurumie!
Nawasilisha!