Wanaume wenzangu, kuwa na mpenzi mmoja ni hatari kuliko ugonjwa wa kisukari

Huo ushaur wako wataupokea wazinz. Ila usichopenda tutendewa na ww ucmtendee mwenzio au unadhan wanawake wao wana mioyo ya tofaut na wanaume? Au wanawake wao waksalitiwa hawaumii?
 
Uhuru na Kazi, Kazi na Bata!

Tukiacha unafiki pembeni, wengi ni mashahidi katika hili.

Unapokuwa na 'mahusiano' mapya, kuna raha sana kimwili na kihisia. Kila wakati unatamani kuwa na mpenzi wako, japo kwa maongezi tu kwa njia ya simu ikiwa yuko mbali nawe.

Kila unachofanya unatamani kumshirikisha na kusikia maoni yake, hamu ya kuwa naye inakuwa katika kiwango cha juu sana kisichomithilika.

Hiki ndo pekee kipindi ambacho furaha yako ya mapenzi unapaswa kuipima, lakini cha ajabu baada ya muda haya yote husahaulika na kupotea kabisa!

Basi achana na porojo za kuvumilia kwamba hiyo ni kawaida, hakuna cha kawaida hapo. Ndiyo maana ukipata mpenzi mwingine ile furaha tele hukurejea tena.

Sisemi hii kwa lengo la kupotosha au kuhamasisha mtindo usiofaa, la hasha. Ni ukweli ambao upo hata nisipokwambia, mimi ndivyo ninavyojisikia.

Hata katika mahusiano yenye malengo madhubuti, mathalani kuelekea ndoani. Kipindi cha furaha kwa walio wengi ni kipindi cha uchumba tu, hapa kila mmoja anakuwa 'at their best'.

Baada ya hapo huko ndoani ni uvumilivu tu na kulea familia, ndiyo maana wajanja waliostukia huwa hawavuki hatua ya uchumba. Furaha ikiisha piga chini, pata mchumba mwingine kula raha mpya.

Note:
Linapokuja suala la familia itabidi uvumilie tu, lakini sio kweli kwamba utazipata raha kwa kiwango kile... labda mjifanyishe tu ili siku ziende.

Kupanga ni kuchagua, nimechagua FURAHA.
 
Bosi samahani lakini,hivi hapa umeongelea jinsia gani zaidizaidi?

Hoja yako inaweza kuwa na mashiko kwa vijana Wa kiume ambao hawajaoa,ila kwa mabinti unawafundisha kuchepuka hata wakiwa tayari ndani ya uhusiano.
 
Bosi samahani lakini,hivi hapa umeongelea jinsia gani zaidizaidi?.
Hoja yako inaweza kuwa na mashiko kwa vijana Wa kiume ambao hawajaoa,ila kwa mabinti unawafundisha kuchepuka hata wakiwa tayari ndani ya uhusiano.

Furaha ni kwa jinsia zote mkuu, kwanini umeona mashiko kwa vijana wa kiume tu... hata mabinti wanahitaji hicho kipindi cha kufurahi.
 
Back
Top Bottom