Wanaume wenzangu, kuwa na mpenzi mmoja ni hatari kuliko ugonjwa wa kisukari

Mukulu wa Bakulu

JF-Expert Member
Aug 12, 2014
4,052
12,906
Hua nikipata muda hua siachi kuwaasa wanaume wenzangu mambo yahusuyo mahusiano na maisha yao.

Hii ni kuwakumbusha tu, kua na mpenzi mmoja ni hatari kuliko kua na ugonjwa wa kisukari na presha.

Heri uugue presha na sukari kuliko kua na mpenzi mmoja. Siku akikuacha unaweza kujiua.

Wanawake hawaaminiki, halafu huwa maamuzi yao ni ya kushtukiza na kushtusha na ya ghafla. Unaweza kuwekeza kwake moyo wako siku akikuacha unaweza kuua mtu.

Last time niliwaasa wanaume wenzangu kuhusu kuwapa wanawake mioyo yenu, heri umpe hela ila usije kumpa moyo wako.

Sasa leo nakuongezea hili, kua na mpenzi mmoja ni hatari kuliko ugonjwa wa kisukari, heri uugue kisukari kuliko kua na mwanamke mmoja.

Huu ni ushauri tu, unaweza kuuchukua au ukauacha ila siku zote ukweli hubakia kua ukweli, bila kujali kua utaukubali au utaukataa na ukweli ndio huu.

Soma mijadala hii pia:

1) Ukweli Usemwe: Hakuna Mwanaume mwenye mpenzi mmoja. Bado sijaona

2) Unasumbuliwa na tatizo la kutodumu na mpenzi mmoja?

3) Wanawake ni wengi kuliko wanaume sasa itakuwaje kuwa na mpenzi mmoja?

4) Mpenzi mmoja kwa Wanawake wa Bongo ni Uongo wala haijawahi kutokea, wanaume Shituka..

5) Ni kitu gani hutufanya tuwe na mpenzi zaidi ya mmoja?

6) Niwapongeze wanaume wenzangu wenye mke/mpenzi mmoja na hamchepuki, nyie sio watu wa kawaida!
 
Utajiongopea vyote lakini kamwe huwezi kuiongopea nafsi yako!!!!....

Kuwa na wapenzi wengi hakupunguzi maumivu ya kuachwa na umpendaye......!!!!

Hata ulale na wanawake wote duniani lakini mwanamke mmoja ambaye moyo wako upo kwake.....unaweza ukakataa hadharani lakini ndani ya nafsi yako unakiri ukweli huu.....!!!

Ukiwa na mpenzi wako ndio unafanya mapenzi na ukiwa na hawara zako ndio unafanya ngono!!!!!....

Suala la kubadilika kila mtu anabadilika!!!!! Wake kwa waume!!!!
 
Ukiwa nao wengi, ukienda kwa huyu na yule naye aliyeachwa apumzike naye
anaenda huko kubebishwa kanakuwa kamduara
 
Utajiongopea vyote lakini kamwe huwezi kuiongopea nafsi yako!!!!....

Kuwa na wapenzi wengi hakupunguzi maumivu ya kuachwa na umpendaye......!!!!

Hata ulale na wanawake wote duniani lakini mwanamke mmoja ambaye moyo wako upo kwake.....unaweza ukakataa hadharani lakini ndani ya nafsi yako unakiri ukweli huu.....!!!

Ukiwa na mpenzi wako ndio unafanya mapenzi na ukiwa na hawara zako ndio unafanya ngono!!!!!....

Suala la kubadilika kila mtu anabadilika!!!!! Wake kwa waume!!!!
Noted
 
Back
Top Bottom