Wanaume wenzangu, kabla ya kuamua kuingia ndoani fanya kama mimi

TheMnyonge

JF-Expert Member
Mar 25, 2022
400
896
Baada ya kuwa kwenye mahusiano kwa takribani mwaka mmoja na miezi kadhaa, nikajiaminisha kuwa sasa ni muda wa kuanza process za kuoa rasmi!

Nikakaa chini na kutafakari kama huyu ninayetaka kumuoa ni mke wa kuishi naye kwenye shida na raha au anakuja kushiriki tu kwenye matumizi ya pesa zangu? (Nikaamua kuingia kwenye uchunguzi) kwa mbinu za kivita!

Kwanza kabisa nikaomba ruhusa kazini, (likizo ya mwaka) nikamwambia mchumba wangu kuwa kuna tatizo ghafla kazini, hivyo nimesimamishwa! (akashtuka sana na facial expression ikabadilika), wiki iliyofuata nikaona majibu yake nikimuandikia text yamekuwa mkato mkato tu, ule uchangamfu wake ukatoweka! (Hapo tumesha tambulishana pande zote mbili)

Nikawa namchora tu, anavyobadilika rangi kama kinyonga, (hapo yeye anakwenda kazini kama kawaida na pesa anapata), nikamwambia nina uhitaji mkubwa wa pesa kama laki tano na hamsini, nitakurudishia, akanijibu "kazi yenyewe huna utapata wapi pesa ya kunirudishia, SINA CHA KUKUSAIDIA" nikamsihi sana kwamba kwa point niliyopo ntadhalilika asiponisaidia akaniambia "HAUTAKUWA WA KWANZA KUDHALILIKA"

Nikafunika kombe mwanaharamu apite, nikamkaushia akakausha, kila nikimpigia anaonekana hana interest kabisa ya kuongea na mimi, juzi nikamuomba aje home, akasema angekuja jana,(wakati huko siku za nyuma alikuwa ananipigia anaomba ufunguo akafanye usafi, kama kuosha vyombo, kufua n.k) mpaka nikasa huyu sasa ndo mke, kumbeeeeee!

Jana tangu asubuhi nampigia simu hapokei, nimeandika text kama 8 hivi haikujibiwa hata moja, nikamuandikia "kulikoni mpnz wangu" akani-blue tick bila kusema chochote!

Leo asubuhi nikamtafuta tena, hajajibu chochote, ilivyofika majira ya saa kumi hivi nikapata majibu, huyu naye ni garasa tu, ana-act kuwa mtu kwa sababu ya pesa, ila hana mapenzi kabisa na mimi, nikamuandikia kuwa asinitafute tena, na haya yakawa ndiyo majibu yake...

Hakika wanawake wapo wengi sana ila kupata mke bado ni kibarua kizito mno, ngoja niendelee kuishi ishi kwanza, zoezi la kuendelea na habari za kulipa mahari linasimamishwa kwa na mchakato wa kuanza kutafuta mwingine unaanza Mara moja!
Screenshot_20220805-211208~3.jpg
 

Nakukunda

JF-Expert Member
Jul 10, 2017
797
1,438
MKUU UNAKAA HOME MWAKA MZIMA KISA MDADA? RUDI KAZINI BANA UKAPAMBANE.....

Katika maisha kama vile ambavyo wewe unavigezo vya kuchagua mke na mchumba wako pia anavigezo vya kuchagua mume

Wewe ukiwa unapenda mwanamke mvumilivu kwa shida na raha na yeye anapenda mwanaume ambaye sio jobless....

Ni kama tu vile baadhi ya wanaume wanapenda kuoa walimu na wengine wanapenda kuoa mke akae home

Hata mwanamke wako ana selection na hiyo haimfanyi kuwa mke bora au mke mbaya.
 

Lanlady

JF-Expert Member
Feb 27, 2019
347
1,002
Ndio ni sahihi
Ila sio kwenye maisha
Fedha inaweza kuja na kupotea
Je ni vyema mwenzio akipoteza kazi umsumbue?
What if kama na yeye aliomba apate mtu ambaye sio tegemezi kwake?
Binafsi hii michezo ya seek and hide kwenye mahusiano siitaki kabisaa.
Life itself is full of trials and temptations! Kujaribiana sio kuzuri.
Watu washavurugwa vya kutosha
 

Nakukunda

JF-Expert Member
Jul 10, 2017
797
1,438
What if kama na yeye aliomba apate mtu ambaye sio tegemezi kwake?
Binafsi hii michezo ya seek and hide kwenye mahusiano siitaki kabisaa.
Life itself is full of trials and temptations! Kujaribiana sio kuzuri.
Watu washavurugwa vya kutosha
Kabisa

Ikitokea mume kawa Jobless kwenye ndoa tutahandle sababu hiyo ni changamoto kama nyingine tu na inavumilika ila sio kupimana kwenye uchumba

Huo mtihani aliompa sio kabisa
 

Agera 1

JF-Expert Member
Jun 5, 2014
3,138
2,598
Baada ya kuwa kwenye mahusiano kwa takribani mwaka mmoja na miezi kadhaa, nikajiaminisha kuwa sasa ni muda wa kuanza process za kuoa rasmi!
Mimi kuna shetani mmoja alikuwa ananiambia et mwanaume hakosi kazi! Yeye anachowaza ni pesa zangu bila kujua nimepata wapi mazingira gani. Yaani hata kama ulivokuwa ofisini unalamba posho nzuri ghafla haupo et next week uingie kuzibua hata mitaro na vyeti vyako kweli au awe na subira upate ishu nyingne
 

Lee Swagger

JF-Expert Member
Mar 30, 2018
927
1,631
Kuna Makosa Makubwa ya Mahusiano. Nayaona Hapa. Ukimtafuta Mwanamke asipokujibu, Usimtafute Tena mpka Siku 3, zipite.

Alafu Baada ya Hizo Siku 3 Asipokucheki. Mcheki alafu usimuulize kwann hajajibu. Muulize Kuhusu Ishu Nyingine.

Kwa Maoni Yangu, Msamehe lakini Usimwamini. Alafu Ntakupa Mbinu Nyingine Ya Kumpima.
 

Just a person

Senior Member
May 16, 2022
188
169
Mimi kuna shetani mmoja alikuwa ananiambia et mwanaume hakosi kazi! Yeye anachowaza ni pesa zangu bila kujua nimepata wapi mazingira gani..ya i hata kama ulivokuwa ofisini unalamba posho nzuri ghafla haupo et next week uingie kuzibua hata mitaro na vyeti vyako kweli au awe na subira upate ishu nyingne
😁😁 nmecheka watu mnasahau uanaume ni nini
 

vanus

JF-Expert Member
May 27, 2017
341
699
Mapenzi na upofu wake hayokosi maajabu, utashangaa mshikaji analegeza na kujipa matumaini kwamba atabadilika mbele ya safari wakati ushaujua ukweli kwamba huyo si mke

Kiungo kikubwa cha ndoa ni upendo, maana ya upendo ni kukubaliana, kuikumbatia hali ya mwenzako haijalishi amefilisika, mlemavu au maskini, haya ni madhaifu madogo sana ambayo hakuna anayependa au kutamani kuwa nayo, ila kwa huyo mkeo mtarajiwa hana upendo wowote yeye anaangalia mazuri tu kwako ambapo ni kitu kigumu kwa binadamu ambaye asili yake si mkamilifu.

Upendo ni kukubaliana na madhaifu ya mwenza wako, na wala si mazuri tuu
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

39 Reactions
Reply
Top Bottom