TheMnyonge
JF-Expert Member
- Mar 25, 2022
- 739
- 1,871
Baada ya kuwa kwenye mahusiano kwa takribani mwaka mmoja na miezi kadhaa, nikajiaminisha kuwa sasa ni muda wa kuanza process za kuoa rasmi!
Nikakaa chini na kutafakari kama huyu ninayetaka kumuoa ni mke wa kuishi naye kwenye shida na raha au anakuja kushiriki tu kwenye matumizi ya pesa zangu? (Nikaamua kuingia kwenye uchunguzi) kwa mbinu za kivita!
Kwanza kabisa nikaomba ruhusa kazini, (likizo ya mwaka) nikamwambia mchumba wangu kuwa kuna tatizo ghafla kazini, hivyo nimesimamishwa! (akashtuka sana na facial expression ikabadilika), wiki iliyofuata nikaona majibu yake nikimuandikia text yamekuwa mkato mkato tu, ule uchangamfu wake ukatoweka! (Hapo tumesha tambulishana pande zote mbili)
Nikawa namchora tu, anavyobadilika rangi kama kinyonga, (hapo yeye anakwenda kazini kama kawaida na pesa anapata), nikamwambia nina uhitaji mkubwa wa pesa kama laki tano na hamsini, nitakurudishia, akanijibu "kazi yenyewe huna utapata wapi pesa ya kunirudishia, SINA CHA KUKUSAIDIA" nikamsihi sana kwamba kwa point niliyopo ntadhalilika asiponisaidia akaniambia "HAUTAKUWA WA KWANZA KUDHALILIKA"
Nikafunika kombe mwanaharamu apite, nikamkaushia akakausha, kila nikimpigia anaonekana hana interest kabisa ya kuongea na mimi, juzi nikamuomba aje home, akasema angekuja jana,(wakati huko siku za nyuma alikuwa ananipigia anaomba ufunguo akafanye usafi, kama kuosha vyombo, kufua n.k) mpaka nikasa huyu sasa ndo mke, kumbeeeeee!
Jana tangu asubuhi nampigia simu hapokei, nimeandika text kama 8 hivi haikujibiwa hata moja, nikamuandikia "kulikoni mpnz wangu" akani-blue tick bila kusema chochote!
Leo asubuhi nikamtafuta tena, hajajibu chochote, ilivyofika majira ya saa kumi hivi nikapata majibu, huyu naye ni garasa tu, ana-act kuwa mtu kwa sababu ya pesa, ila hana mapenzi kabisa na mimi, nikamuandikia kuwa asinitafute tena, na haya yakawa ndiyo majibu yake...
Hakika wanawake wapo wengi sana ila kupata mke bado ni kibarua kizito mno, ngoja niendelee kuishi ishi kwanza, zoezi la kuendelea na habari za kulipa mahari linasimamishwa kwa na mchakato wa kuanza kutafuta mwingine unaanza Mara moja!