Maswali ya kujiuliza kabla hujaamua kuingia kwenye ndoa

karv

JF-Expert Member
Dec 26, 2019
1,799
3,221
Habari zenu watanzania wenzangu hasa kwa wale ambao bado hamjaoa

Nimepata kitu nimeona ni bora kuchangia na nyie ambao mnatarajia kuoa siku za mbeleni.

Mambo yenyewe ni hayo hapo

Kwa nini ufungue ndoa na mtu?

~Usifunge ndoa sababu ya msukumo mkubwa wa kihisia au watoto (sababu ya mimba) au mambo ya nje (wazazi, ndugu, marafiki, tamaa ya pesa au mali hii hasa kwa wanawake nakazia hapo).

2)Ni kwa jinsi gani mnaweza kukabiliana na mabadiliko yoyote yatakayo tokea kwenye ndoa yenu?
~Hapa tunazungumzia kufilisika, magonjwa, kufukuzwa kazi nk

3)Unawezaje kukabiliana na kutoelewana kati yenu?
~Hapa ndio linakuja suala zima la uvumilivu pindi mnapokwazana gubu na malalamiko yasiyoisha.

4)Ni kwa muda gani unaweza kuvumilia kuwa mbali na mpenzi wako?
~Hapa nasema na wale ambao wapenzi wao ni watu wa kusafiri au wanatumia muda mwingi kwenye kazi kuliko kuwa na familia au wapenzi wao.

5)Je unataka watoto wangapi na waachane kwa muda gani?
~Usizae watoto ambao huwezi kuwahudumia mwishowe ukakimbia familia bure mwanamke ndio nguzo muhimu katika hili. Nakazia hapo

6)Mtashughulikia vipi maswala ya uzazi?
~kukosa watoto, Nguvu za kiume, kibamia, K mnako wengine bwawa ukikutana na hali kama hiyo utafanyaje. Hapa nakazia shake well before use shake wellll before use welll welll shake before to use it.

7)Utakabiliana vipi na hisia za kingono?
~kwa mfano wewe unataka yeye anakwambia hayupo sawa au hana au wewe unataka yeye yupo hedhi au wakati wewe hamu imepanda yeye hayupo yupo safarini.

8)Maswala ya mali itakuwaje mtashare au kila mtu kivyake? (nakazia hapa)
~utakuta familia mke na mume wote wafanyakazi halafu hela ya mke haionekani inaenda wapi zinatumika za mwanaume tu. Kama mtakubaliana kushare basi kila mmoja kipato chake kiwe wazi kwa mwenzake.

9)Mgawanyo wa kazi utakuwaje?
~Hapa nazungumzia maswala mazima ya uleaji na utunzaji wa familia yenu.

10)Jaribu kukumbuka nyakati ngumu na mlisolve vipi hilo tatizo?

11)Bajeti na maswala ya fedha itakuwa ni jukumu la mmoja kati yetu au wote?

12)Kama kutakuwa na tatizo nani awe mshauri au wapi pa kukimbilia(nakazia hapa)
~Sio kila mtu ni wa kuambiwa matatizo na changamoto za ndoa yenu.

13)Ikitokea tukawa mbali nitamudu vipi hisia zetu?(nakazia hapo)
~Kama mmoja hawezi bora mfatane kama kumbi kumbi tu vinginevyo mtachapiana tu.

14)Nani aache anachopenda kwa ajili ya familia?
~Baba unaweza kuacha kwenda baa jion au ukapunguza ili kutumia muda mwingi na watoto au familia.
~Mama unaweza kuacha safari zisizo na maana kwa ajili ya mume na wanao.

SIRI(nakazia hapa)
~Kuna baadhi ya mambo sio ya kusema ni kunyamaza tu na kukaa kimya.

16)Maswala mazima ya kidini na kiimani yapoje (nakazia hapo)
~Kama ni dini au imani tofauti nani atamfata mwenzie.

17)Je kuna umuhimu wa kushirikishana kihisia?
~Kama show ni mbovu nifanyaje mwenzangu atalipokeaje?

]18)Kipi unapenda kwake kipi hupendi kwake kipi anapenda kwako kipi hapendi kwako ?(nakazia hapa)

19)Safari na mitiko mbalimbali itakuwaje nani anapenda hapendi?

Maswala ya kiuandishi tutasameheana tu

SIJALAZIMISHA MTU KUOA MIMI

NDOA NDOANO

maendeleo hayana chama

NB: PICHA HAIHUSIANI NA UZI

JamiiForums2065598231.jpg

NDOA ni shule pekee ambayo unapata cheti kabla ya kuanza masomo. Ni shule ambayo kamwe hauwezi kuhitimu.

Ni shule ambayo unatakiwa kuhudhuria siku zote za uhai wako. Ni shule ambayo hakuna likizo ya kuumwa au sikukuu.

Ni shule ambayo iligunduliwa na Mungu katika misingi ifuatayo;

1. Msingi wa upendo.

2. Kuta za shule zimejengwa kwa "uaminifu"

3. Madirisha yametengenezwa kwa "uvumilivu"

4. Samani zimetengenezwa kwa "msamaha"

5. Na ikaizekwa kwa "Imani"

Ukumbuke kuwa wewe ni mwanafunzi tu na sio mkuu wa shule ya NDOA. Mungu ndio Mkuu wa Shule.

Hata wakati wa mapito, majaribu, kimbunga na misukosuko ya hapa na pale usikimbie nje ya shule.

Kamwe usiende kulala kabla hujamaliza homework yako. Kamwe usisahau kusoma somo la mawasiliano. Wasiliana na mwanafunzi mwenzio pamoja na Mwalimu mkuu.

Kama utaona kuna kitu kwa mwanafunzi mwenzako ambacho kimsingi haukipendi, basi ukumbuke mwenzako nae ni mwanafunzi na sio mhitimu mwalimu Mkuu bado hajamalizana nae. Hivyo ichukulie ni changamoto na muifanyie kazi kwa pamoja.

Msisahau kusoma kitabu kitakatifu kilicho kwenye mtaala wa shule ya Ndoa (Biblia na quran). Najua kuna muda unaweza ukajisikia kutokuhudhuria darasani lakini unatakiwa uhudhurie tu.

Utakapojaribiwa kuacha shule jipe ujasiri wa kuendelea na shule. Najua mitihani mingine ya muhula au nusu muhula inaweza kuwa migumu isiyo na majibu kwako.

Lakini kumbuka Mwalimu Mkuu anayo majibu tayari na anafahamu unaweza ukakabiliana nayo na anaona hiyo ndio shule nzuri kwako kuzidi nyingine.

Ni moja ya shule nzuri kabisa katika ulimwengu huu. Furaha, amani, na upendo husindikiza masomo ya kila siku.

Masomo mbalimbali hutolewa katika shule hii, ila somo kuu kuliko yote ni UPENDO.

Baada ya miaka yote ya kusoma kwa nadharia, ukijiunga na shule hii utasoma kwa vitendo.

Kupendwa ni kitu kizuri, lakini kupenda ni upendeleo wa vyote. Ndoa ni sehemu ya furaha. Inatakiwa kufurahia tofauti zenu na sio tofauti zenu ziwe chanzo cha kutoelewana.

Mimi J nawatakia kila la kheri wote mliopo kwenye hii shule takatifu. Na sisi ambao bado tumuombe mwenyezi Mungu ambae ni Mkuu wa Shule akatuchagulie wanafunzi wenzetu walio bora ambao tutaweza kujiunga nao katika hii shule nzuri hapa Duniani.

Mkuu wa Shule (MUNGU) awabariki.
 
Habari zenu watanzania wenzangu hasa kwa wale ambao bado hamjaoa

Nimepata kitu nimeona ni bora kuchangia na nyie ambao mnatarajia kuoa siku za mbeleni.

Mambo yenyewe ni hayo hapo

1)Kwa nini ufungue ndoa na mtu?
~Usifunge ndoa sababu ya msukumo mkubwa wa kihisia au watoto (sababu ya mimba) au mambo ya nje (wazazi, ndugu, marafiki, tamaa ya pesa au mali hii hasa kwa wanawake nakazia hapo).

2)Ni kwa jinsi gani mnaweza kukabiliana na mabadiliko yoyote yatakayo tokea kwenye ndoa yenu?
~Hapa tunazungumzia kufilisika, magonjwa, kufukuzwa kazi nk

3)Unawezaje kukabiliana na kutoelewana kati yenu?
~Hapa ndio linakuja suala zima la uvumilivu pindi mnapokwazana gubu na malalamiko yasiyoisha.

4)Ni kwa muda gani unaweza kuvumilia kuwa mbali na mpenzi wako?
~Hapa nasema na wale ambao wapenzi wao ni watu wa kusafiri au wanatumia muda mwingi kwenye kazi kuliko kuwa na familia au wapenzi wao.

5)Je unataka watoto wangapi na waachane kwa muda gani?
~Usizae watoto ambao huwezi kuwahudumia mwishowe ukakimbia familia bure mwanamke ndio nguzo muhimu katika hili. Nakazia hapo

6)Mtashughulikia vipi maswala ya uzazi?
~kukosa watoto, Nguvu za kiume, kibamia, K mnako wengine bwawa ukikutana na hali kama hiyo utafanyaje. Hapa nakazia shake well before use shake wellll before use welll welll shake before to use it.

7)Utakabiliana vipi na hisia za kingono?
~kwa mfano wewe unataka yeye anakwambia hayupo sawa au hana au wewe unataka yeye yupo hedhi au wakati wewe hamu imepanda yeye hayupo yupo safarini.

8)Maswala ya mali itakuwaje mtashare au kila mtu kivyake? (nakazia hapa)
~utakuta familia mke na mume wote wafanyakazi halafu hela ya mke haionekani inaenda wapi zinatumika za mwanaume tu. Kama mtakubaliana kushare basi kila mmoja kipato chake kiwe wazi kwa mwenzake.

9)Mgawanyo wa kazi utakuwaje?
~Hapa nazungumzia maswala mazima ya uleaji na utunzaji wa familia yenu.

10)Jaribu kukumbuka nyakati ngumu na mlisolve vipi hilo tatizo?

11)Bajeti na maswala ya fedha itakuwa ni jukumu la mmoja kati yetu au wote?

12)Kama kutakuwa na tatizo nani awe mshauri au wapi pa kukimbilia(nakazia hapa)
~Sio kila mtu ni wa kuambiwa matatizo na changamoto za ndoa yenu.

13)Ikitokea tukawa mbali nitamudu vipi hisia zetu?(nakazia hapo)
~Kama mmoja hawezi bora mfatane kama kumbi kumbi tu vinginevyo mtachapiana tu.

14)Nani aache anachopenda kwa ajili ya familia?
~Baba unaweza kuacha kwenda baa jion au ukapunguza ili kutumia muda mwingi na watoto au familia.
~Mama unaweza kuacha safari zisizo na maana kwa ajili ya mume na wanao.

15)SIRI(nakazia hapa)
~Kuna baadhi ya mambo sio ya kusema ni kunyamaza tu na kukaa kimya.

16)Maswala mazima ya kidini na kiimani yapoje (nakazia hapo)
~Kama ni dini au imani tofauti nani atamfata mwenzie.

17)Je kuna umuhimu wa kushirikishana kihisia?
~Kama show ni mbovu nifanyaje mwenzangu atalipokeaje?

18)Kipi unapenda kwake kipi hupendi kwake kipi anapenda kwako kipi hapendi kwako ?(nakazia hapa)

19)Safari na mitiko mbalimbali itakuwaje nani anapenda hapendi?

Maswala ya kiuandishi tutasameheana tu

SIJALAZIMISHA MTU KUOA MIMI
NDOA NDOANO

maendeleo hayana chama

NB: PICHA HAIHUSIANI NA UZIView attachment 2098261
Hivi umeshawahi kujiuliza kwa nini unataka kuoa au kuolewa? Ni kwa sababu rafiki zako wengi wameoa au kuolewa? Ni kwa sababu wadogo zako wote tayari wana ndoa zao isipokuwa wewe? Ni kwa sababu unataka urahisi wa kutimiza haja zako za kimwili?

Umewahi kujiuliza kwamba unaingia kwenye ndoa kwa sababu kweli unahitaji kuanzisha familia na kuwa na mwenzi wa maisha yako mtakayevumiliana na kupendana kwenye shida na raha, uzima na maradhi, umaskini na utajiri?

Kama hujawahi kujiuliza, hebu jiulize hivi sasa, lengo hasa linalokufanya utake kuingia kwenye ndoa (kama bado haupo kwenye ndoa) ni nini? Au kama tayari upo kwenye ndoa lakini hakuna amani kati yako na mwenzi wako, kila siku ni migogoro isiyokuwa na mwisho, jiulize nini hasa kilikufanya uingine kwenye ndoa?
Utashangaa kugundua kwamba wengi wanaingia kwenye ndoa kama fasheni tu, kwamba kwa sababu ni lazima mwanaume na mwanamke waoane na kuanzisha familia, basi na wao wanafuata mkumbo tu. Matokeo yake, ndoa za namna hii zinakosa uhai na ndiyo chanzo cha nyingi kuvunjika muda mfupi baada ya kufungwa au miaka kadhaa baadaye.

Jambo la msingi ambalo unapaswa kulizingatia kabla ya kuingia kwenye ndoa (kama bado hujaingia) ni upendo wa dhati. Hata vitabu vya dini vinaeleza kwamba upendo una nguvu kuliko mauti.

Unapompenda mtu kwa dhati, utakuwa tayari kuachana na mambo mengine yote na kushikamana naye kujenga ndoa itakayokuwa bora na itakayodumu. Lakini kuwa na upendo pekee haitoshi kuwa sababu ya kuingia kwenye ndoa, jambo lingine muhimu ni dhamira ya dhati.

Je, moyo wako unahitaji kweli kuingia ndani ya ndoa na upo radhi kukabiliana na yote utakayokumbana nayo ndani yake? Kama jibu ni ndiyo, basi upo tayari kuingia kwenye ndoa. Jambo ambalo watu wengi huwa hawalielewi, ndoa siyo kitu cha kukifanyia mzaha au majaribio, ‘kwamba ngoja niingie nione itakuwaje!’

Ni lazima ujiridhishe sana kuhusu huyo unayeenda kuanzisha naye maisha ya ndoa. Utashangaa kugundua kwamba watu wanaingia kwenye ndoa lakini bado wanaendeleza zile tabia za ujana kama walizokuwa nazo kabla hawajaingia kwenye ndoa.

Wewe ni mke wa mtu tayari, una sababu gani ya kuvaa mavazi yanayoudhalilisha utu wako? Una haja gani ya kukesha baa na marafiki huku ukimuacha mwenzi wako akipigwa na baridi? Una sababu gani kutwa nzima upo kwenye mitandao ya kijamii, unachati na kuwasiliana na watu wa jinsia tofauti au kuposti picha zinazoshusha hadhi ya mwenzi wako?

Umeshaingia kwenye ndoa, kwa nini unaendelea kuambatana na marafiki hata wasiojua maana au thamani ya ndoa? Kwa nini huachi tabia za ‘ujana’? Unataka uende disko na marafiki mpaka usiku wa manane, unataka uendelee kupigiana simu na marafiki wa jinsia tofauti na yako kwa sababu tu mlisoma pamoja au mnafanya kazi pamoja?

Sisemi kwamba unapoingia kwenye ndoa basi ndiyo uwe mtumwa, hapana! Kuna baadhi ya vitu unapaswa kuvipunguza sana au kama havina maana ni bora ukaviepuka ili kuondoa migogoro isiyo ya lazima.

Upo usemi wa masihara maarufu mitaani kwamba ndoa ndiyo mtihani pekee ambao unapewa cheti kabla ya kuingia kwenye chumba cha mtihani! Ukiamua kuingia kwenye ndoa, achana na mambo ya ujana, utaifurahia ndoa yako.

Kwangu,mm sijaoa ,hivyo nachukua notebook yangu naenda kuorodhesha maswali yote ili kusudi niwe nacheck list yangu kabla yakuingia ktk ndoa,nakama kuna nondo zingine muhimu katika sekt hii ,mleta mada nakuomba usisite kudondosha nondo hapa,binafsi nnakushukkuru Sana,kwauzi mzuri,
 
Back
Top Bottom