Wanaume wengine ni chanzo cha uharibifu wa maisha ya mwanamke

Talha

JF-Expert Member
Nov 11, 2021
202
220
Ila wanaume wengine ni chanzo cha uharibifu wa maisha ya mwanamke, kama mwanaume umeshindwa kuendelea na mwanamke kwanini usimuache kiamani unaamua kumzushia mambo ambayo hayafanyi ili umuharibie, ili jambo siyo zuri hata kidogo.

Mwanaume unamtoa mdada wa watu mahali au kwao unampeleka sehemu at the end of the days unamfukuza kama mbwa, this is not fair kabisa.

Wiki hii imekua ya mawazo kwangu baada ya ndugu yangu kupatwa na sekeseke katika mahusiano yake, ameishi na mwanaume amempa mtaji akaanza biashara, biashara imeonesha nuru, mwanaume kapata mwanamke mwingine basi muache mdada wa watu kama humtaki lakini wewe unamfukuza hutaki aishi aendelee na biashara uo mkoa yani kisa wewe ndiye uliye mleta lakini hajakukosea chochote muache kiamani.

This is not fair kbsa unajua kabisa mdada wa watu atatoboa kwenye hiyo biashara ata bila wewe unaamua kumuaribia, Mungu siku zote ni mwaminifu ukimfanyia mtu ubaya ipo siku yako Mungu atamfuta machozi uliyemfanyia ubaya.

Wanaume badilikeni unajua umepata mwingine muache mtu aendelee na life yake pale anapopataka, umemtoa mkoani leo unataka aondoke kisa wewe ndiye uliyemleta na mtu tayari kaanzisha biashara imesimama unataka kumrudisha nyuma.
 
Ila wanaume wengine ni chanzo cha uharibifu wa maisha ya mwanamke,kama mwanaume umeshindwa kuendelea na mwanamke kwanini usimuache kiamani unaamua kumzushia mambo ambayo hayafanyi ili umuharibie,ili jambo siyo zuri
Shida Ni kwamba tunawatoa mbali ....mkifika mjini mnaanza kujifanya wajanja....now Ni mwendo wa heavy sanctions tu....
 
Kuachwa na kuchukuliwa upya mbona ni mambo ya kaiwaida sana
 
Shida Ni kwamba tunawatoa mbali ....miifika mjini mnaanza kujifanya wajanja....now Ni mwendo wa heavy sanctions tu....
Na Ivo vikwazo ambavyo mnaweka ni kumkomoa mtu kuhakikisha anarud 0,kama alifika stage fulani arudi tena mwanzo kitu ambacho hakina maana,muache mtu aendelee na maisha yke ulimtoa mahali ujue pia umempotezea muda wake,na zaidi ya yote unampangia pa kuishi asikae mkoa ambao wewe umempeleka.
 
Na Ivo vikwazo ambavyo mnaweka ni kumkomoa mtu kuhakikisha anarud 0,kama alifika stage fulani arudi tena mwanzo kitu ambacho hakina maana,muache mtu aendelee na maisha yke ulimtoa mahali ujue pia umempotezea muda wake,na zaidi ya yote unampangia pa kuishi asikae mkoa ambao wewe umempeleka.
Inauma kiupande mwingine hujui tu mapenzi yanatesa sana kwa kweli usiombe demu umemfanyia kila kitu then azingue
 
Inauma kiupande mwingine hujui tu mapenzi yanatesa sana kwa kweli usiombe demu umemfanyia kila kitu then azingue
Sasa hyo ni another case, but kama we mwanaume ndo umepata sehemu nyingine patamu zaidi basi muache uyu aendelee kuishi apambane mkoa uo uo uliomleta lakini unaona aibu ukimuach atatoboa hatoshindwa kuendesha biashara kwanini umfukuze? Hutaki kumuon mkoa ulimpeleka,ni unyanyasaji uliovuk mipaka.
 
Sasa unataka ang'ang'anie biashara ya mwanaume...?! Sasa hivi ukifukuzwa unaondoka na ulivyo kuja navyo tu...
Tatizo lenu wanawake mnaamini ndoa ni mafanikio ktk maisha, acha muendelee kuuwawa kupigwa na kuumizwa... Tafuta maisha yako uinjoi dunia
 
Umemsikiliza na mwanaume anasemaje kuhusu hilo swala?
Nimemsikiliza hana hoja ya msingi anachotaka mwenzie aondoke na hataki kusikia la mtu,adi Baba mwenye nyumba kamnyoshea mikono hataki kikao na mtu.
 
Sasa hyo ni another case, but kama we mwanaume ndo umepata sehemu nyingine patamu zaidi basi muache uyu aendelee kuishi apambane mkoa uo uo uliomleta lakini unaona aibu ukimuach atatoboa hatoshindwa kuendesha biashara kwanini umfukuze? Hutaki kumuon mkoa ulimpeleka,ni unyanyasaji uliovuk mipaka.
Lete tusikie na upande mwingine wa hii kesi. Hakuna mwanaume katili anayeweza kuamka tu from nowhere na kuamua kumfukuza mwanamke wake kama mbwa. Lazima kuna kitu umekikoroga.....

Kama jamaa amekutoa huko kwenu kijijini akakupeleka mjini akakupa mtaji akakupambania na sasa umeona biashara imesimama umeanza kumdharau na kumuona siyo wa type yako mbona asicharuke na kuchukua mtaji wake kisha kukutimua? Au ulitaka mpaka akuue?

Na inavyoonekana wewe ni mmoja wa wale wanawake mnaopenda kujifanya ngangari kwa kila kitu halafu gemu likigeuka mnaanza kulia lia ili muonewe huruma. You made your bed, now lay on it!

Unamfungulia mwanamke biashara halafu anataka kuolewa na wateja. We ulisikia wapi?
 
sasa unataka ang'ang'anie biashara ya mwanaume...?! Sasa hivi ukifukuzwa unaondoka na ulivyo kuja navyo tu...
Tatizo lenu wanawake mnaamini ndoa ni mafanikio ktk maisha, acha muendelee kuuwawa kupigwa na kuumizwa... Tafuta maisha yako uinjoi dunia
Umempa mtu kiasi fulani fungua biashara yko ndogo unayotaka,umepambana mpka biashara imekua,sasa kama unataka aondoke kama alivyokuja muache atafute chumba uko uko aendelee na biashara mtu tayari kashakuza brand yke ya biashara,hutaki kumuona ata uo mkoa unamtishia vibaya,iyo ni haki kweli?na unajua kabisa lazima atoboe kma sio wivu na roho mbaya ni nn
 
Kama wanaume siku tukiamua kuweka mambo tunayokutana nayo na vitu tunavyopoteza kwenye mapenzi basi maji ya bahari yangekauka au yangepungua chumvi.
 
Nyinyi wanaume mnajua wenyewe kama mkipata sehemu nyingine mkashikwa mnabadilika lazima uone cha zamani hakifai,Uyu mwanaume yeye ndo mkorofi kapata sehemu nyingine na walishagombana kuhusu akasema amemuacha lkini inaonesha bado yko nae.
 
Wanawake mnapenda kulialia ili mtie huruma muonekane mnaonewa... Sikuzote ukiona mwanamke analalamika ujue yeye ndie shetani namba 1. Ni vile wanaume hatupendi kuongea hovyo, mwanaume hawez kufikia maamuz hayo kama mwanamke katulia... All in all wanawake ndoa zitawatokea puani, sasa hivi ni "Tit for tat"
 
Back
Top Bottom