The Wolf
JF-Expert Member
- Sep 10, 2013
- 9,468
- 20,877
Mwanzo kabisa niseme haya ni maoni na mawazo yangu, kwa ushahidi kidogo nilioupata.Imekuwa ni kawaida sana kukutana na mwanamke/mwanaume, inaweza kuwa kwenye daladala, ofisi, bar, beach na sehemu nyinginezo na kujikuta umeanzisha mahusiano ya kimapenzi kwa kufahamiana kwa mda mfupi au bila kufahamiana vizuri hata kidogo, soma story hii iliyotokealeo hii asubuhi.
Jamaa yangu mmoja, mshirika katika biashara tulikuwa na miadi ya kukutana asubuhi ya leo, akaniambia nimfate kwa kuwa hakuwa na usafiri na nikafanya hivyo, amefikia silver spring, sinza nilimfata mida ya saa kumi na mbili kasoro ili tuelekee nje ya mji.Wakati tunatoka nikapitia njia ya corner bar, niweke mafuta kwenye ile petrol station pembeni. Ile njia ina madadapoa wengi sana wanajipanga kwenye barabara na mida hiyo bado walikuwepo, ghafla jamaa akaniambia, embu simama kaka, akamuita dada mmoja kwa jina lake yule dada alivyokuja na kumuona jamaa alitimua mbio kila mtu alishangaa.
Nilimuiliza jamaa inakuaje, unamjua , jamaa alilia akaniambia huyu mwanamke ni mpenzi wake na anaishi kibaha na mama yake, wameanza kuwa pamoja kama miezi miwili imepita na alikuwa ana mpango wa kumuoa, jamaa nae anakaa Kibaha ila hawaishi pamoja,jamaa alitia huruma sana alilia kama mtoto business trip ikawa trip ya kupeana faraja, hata tulichokifata hakikufanikiwa nikajisemea hii ni mipango ya Mungu.
Labda biashara iliyotakiwa kufanyika siku hii ni hiyo ya jamaa kujua kuhusu mpenzi wake so sijilaumu,hajielewi mpaka mda huu ila nashukuru amenielewa kwa ushauri niliompa.Hii ishu imenifanya niwe muoga sana kwa hawa wadada ninaowatamani mtaani, inabidi tuwe makini sana na watu tunaonzisha nao mahusiano mtaani hilo liwe kama funzo, mjue mtu wako vizuri, tumia kinga na muombe Mungu sana.