Wanaume wengi tunaoa wanawake wenye sifa hizi

Wanaume wengi tunaoa wanawake wenye sifa hizi

[/QUOTE] hahahaa unakutana na mtu ana sifa zote tajwa hapo juu lakini kupelekwa chooni ndo anatakana tabia yake
sa sijui utafanyaje wakati vigezo vyote anavyo au jamaa kasahau kuindicate[/QUOTE]

Kwa wengine hiyo ndo ile kitu kwenye matangazo ya kazi huandikwa kama, "added advantage"!
Ila kuna ambao ni "exclusion criteria" kama kwa mkuu Amicus Curiae
 
MUONEKANO- Awe mzuri wa kawaida tu, kwani naamini binadamu wote ni wazuri sema tunazidiana kwenye maeneo flaniflani, ila tuwe na uwiano kwenye height

AWE MCHA MUNGU- Apende kusali, hata kama hatokwenda kanisani mara zote, angalau aende mara mojamoja basi

ASILI- Sichagui kabila ila naomba tu asiwe MMACHAME (usiniulize kwanini)

USAFI- Awe msafi wa ndani na nje, anukie vizuri wakati wote, sio anuke janaba!!!

ELIMU- Awe na elimu ya kuanzia degree, form 6 anaweza kufikiriwa pia ila kama ana dhamira ya dhati ya kutaka kujiendeleza kielimu

ASIWE TOO DEMANDIND- Yani akitaka jambo lake eti ni lazima liwe, tena kwa wakati alioupanga yeye

TABIA- Asiwe na gubu, akihisi nimemkosea aniulize ili apate ufafanuzi, sio alipize

UPENDO- Anipende kwa dhati, mimi pamoja na ndugu zangu esp baba na mama mkwe wake

ASINIZUIE KUNYWA POMBE- Sio lazima ninywee bar, naweza nikanunua kakreti kangu nikawa nakatwanga nyumbani

UBUNIFU- Awe mbunifu kwa kuchangia mawazo on how to utilize the resources available ili tujistabilize kimaisha

AONYESHE DALILI ZA KUTAKA KUNISAIDIA NINAPOKWAMA- Huu ni msaada wa kimawazo au hata material things kama fedha (yaani asiwe bahili)

MIMI NADHANI WANAUME TULIO WENGI TUNAPENDA SIFA HIZI, KAMA TUTAPISHANA BASI NI KWENYE MAENEO MACHACHE SANA, AU MNASEMAJE MASELA....

Hapo kwenye red pana kazi sana ie akuache asikushauri kuacha pombe na ameona unamissbehave akuache tu kisa kakuta unakunywa pombe na umesema unataka mcha mungu, mbona unachanganya sasa. Wacha Mungu kwao pombe mwiko labda mcha mungu wa kubeep. Kwenye blue umezungumzia elimu mbona kuna walioishia form 4 wanafaa tu au je huoni kuwa hiki kitakua kikwazo cha wewe kumpata alie bora hata alie na elimu chini ya uliyotaka.

Kiukweli sifa hizo kama hautakua flexible basi mtu huyo bado hajazaliwa. Sidhani kama ni rahisi kumpata wa hivyo.
 
hiyo ya pombe mkuu mi big NO hata kiafya sio nzur mana inazuia reabsorption of water through inhibition of antidiuretic hormone na hivyo kupelekea upungufu wa maji mwili
hivi "visayansi mshenzi" vyenu vinawapotosha sana,hakuna kitu kinachoingia mwilini kikakosa madhara,issue ni kutumia kila kitu kwa kiwango maalum
 
Ina maana unaoa elimu au unaoa binadam? Kazi unayo! Kwa kuangalia elimu! Na hakuna mwenye elimu hyo atakayekubali wewe uwe juu yake vingnevyo itakua maigzo.

MIMI NADHANI WANAUME TULIO WENGI TUNAPENDA SIFA HIZI, KAMA TUTAPISHANA BASI NI KWENYE MAENEO MACHACHE SANA, AU MNASEMAJE MASELA....

Chini ya uzi wangu kuna maneno hayo hapo juu... kwenye blue kunakuhusu, hapo ndipo tunapopishana
 
Yeah_hapo kwenye blue pana matter sana mkuu,..mtu amekukuta unapiga zako ndovu...siku si nyingi analeta za kuleta eti uache pombe kwa kudai visingizio kibao mara oooh..inamaliza hela_kwani kuna kitu kimekwama(hapana),..inakusababishia tabia mbaya kama umalaya_kwani umewahi kunifumania(hapana)...itakusababishia magongwa_kwani ninaumwa(hapana)...mimi nimegoma kuacha.

Ha ha well said mkuu,yani akianza kuleta upinzani kwenye gambe sitamuelewa kbs
 
hahahaa unakutana na mtu ana sifa zote tajwa hapo juu lakini kupelekwa chooni ndo anatakana tabia yake
sa sijui utafanyaje wakati vigezo vyote anavyo au jamaa kasahau kuindicate[/QUOTE]


Unantafuta ubaya ww ha ha ha
 
Mimi sikuzote nilipenda sana nioe bonge la mwanamke. mi mfupi kiasi (itategemea unanilinganisha na nani) so ili kuonyesha ukidume wangu shurti nioe mtu kama tembo ili niwe najisifu kila nikimwangalia tu kuwa......hahahaaaaa ukiambiwa mimi ndio naendesha gari kubwa hivi. Then ntafarijika sana na kujiona kidume. sio unaoa kademu kaduchuuuuu na wewe pisi la mtu. huo utakua ni woga na kutojiamini.

CC: Paloma Little Angel
 
Last edited by a moderator:
Ukiwa unataka sifa zote hizo the vice ersa should be true...........
Sio unataka awe msafi wakati wewe kuoga kwenyewe mtihani

na ukichagua sana waweza kosa kabisa au kumpata asie
na tabia tajwa

Ha ha ha ha ha ha
 
Back
Top Bottom