Wanaume wengi tunaoa wanawake wenye sifa hizi

Wanaume wengi tunaoa wanawake wenye sifa hizi

MUONEKANO- Awe mzuri wa kawaida tu, kwani naamini binadamu wote ni wazuri sema tunazidiana kwenye maeneo flaniflani, ila tuwe na uwiano kwenye height

AWE MCHA MUNGU- Apende kusali, hata kama hatokwenda kanisani mara zote, angalau aende mara mojamoja basi

ASILI- Sichagui kabila ila naomba tu asiwe MMACHAME (usiniulize kwanini)

USAFI- Awe msafi wa ndani na nje, anukie vizuri wakati wote, sio anuke janaba!!!

ELIMU- Awe na elimu ya kuanzia degree, form 6 anaweza kufikiriwa pia ila kama ana dhamira ya dhati ya kutaka kujiendeleza kielimu

ASIWE TOO DEMANDIND- Yani akitaka jambo lake eti ni lazima liwe, tena kwa wakati alioupanga yeye

TABIA- Asiwe na gubu, akihisi nimemkosea aniulize ili apate ufafanuzi, sio alipize

UPENDO- Anipende kwa dhati, mimi pamoja na ndugu zangu esp baba na mama mkwe wake

ASINIZUIE KUNYWA POMBE- Sio lazima ninywee bar, naweza nikanunua kakreti kangu nikawa nakatwanga nyumbani

UBUNIFU- Awe mbunifu kwa kuchangia mawazo on how to utilize the resources available ili tujistabilize kimaisha

AONYESHE DALILI ZA KUTAKA KUNISAIDIA NINAPOKWAMA- Huu ni msaada wa kimawazo au hata material things kama fedha (yaani asiwe bahili)

MIMI NADHANI WANAUME TULIO WENGI TUNAPENDA SIFA HIZI, KAMA TUTAPISHANA BASI NI KWENYE MAENEO MACHACHE SANA, AU MNASEMAJE MASELA....

sijui mimi -----! hivi unataka mwanamke awe na degree unamlipa mshahara? halafu utegemee asiwe too demanded wakati kaenda shule? shule asomeshwe na wazazi wake halafu unategemea awaangalie zaidi wazizi wako? wakati tunaelewa kuwa jinsi siku zinavyokwenda extended family zinapungua na hasa wazazi.
mazingira ya kuweka kigezo cha kusaidiwa ni dalili ya woga wa maisha wanaume tunatakiwa kupanga mipango ya maisha yetu msaada ukitokea acha kufikiria kubebwa.
achana na videgree kama kigezo kwanza kwa kiasi kikubwa mwanmke jinsi anavyoendelea kuwa na shule ndivyo anavyokuwa punguza risk katika maisha hivyo hana hofu na wala humsumbui na kindoa chako .
hivyo degree sio kigezo oa mke kisha mwendeleze na mpe degee mwenyewe -mpeleke shule sio usubiri upelekewe
 
Hili ni tangazo la biasharaaaa au unataka na sisi wanaume wengine tueleze tupendayo kwa wanawake??

kaka mkubwa umemchana utamu, maana hata sijaelewa anataka na sisi tumwage ya kwetu, au?
 
sijui mimi -----! hivi unataka mwanamke awe na degree unamlipa mshahara? halafu utegemee asiwe too demanded wakati kaenda shule? shule asomeshwe na wazazi wake halafu unategemea awaangalie zaidi wazizi wako? wakati tunaelewa kuwa jinsi siku zinavyokwenda extended family zinapungua na hasa wazazi.
mazingira ya kuweka kigezo cha kusaidiwa ni dalili ya woga wa maisha wanaume tunatakiwa kupanga mipango ya maisha yetu msaada ukitokea acha kufikiria kubebwa.
achana na videgree kama kigezo kwanza kwa kiasi kikubwa mwanmke jinsi anavyoendelea kuwa na shule ndivyo anavyokuwa punguza risk katika maisha hivyo hana hofu na wala humsumbui na kindoa chako .
hivyo degree sio kigezo oa mke kisha mwendeleze na mpe degee mwenyewe -mpeleke shule sio usubiri upelekewe

Mbona unatokwa na povu aisee! soma uzi vizuri, uuelewe kisha ndio ucomment, wacha kukurupuka wewe,,,
 
Basi tusiosoma tunatabu.

sio kwamba natetea ubaguzi kielimu au nawakandamiza wasiokwenda shule,najaribu kuweka uwiano sawa,wewe mwanamke ukishakugundua elimu ni ndogo basi tafuta bwana ambaye hamjapishana sana kielimu ili,unajua mara nyingi wanaume waliosoma wanakuwa kama indirect wameambukizwa na western culture hivyo mambo yao mengi wanataka wafanye kizungu zaidi,sasa mwenzangu na mimi elimu yako ya STD VII au form 4 tena failure utaweza mchakamchaka wa western life style? hapo utaishia kulia tu na kuona maisha ya ndoa ni magumu,
 
Back
Top Bottom