Wanaume wanapokuwa waongo...!

Mtambuzi

Platinum Member
Oct 29, 2008
8,810
15,395
Black-couple.jpg

Wanaume na wanawake hudanganya, hilo halina ubishi, lakini sidhani kama kuna sababu iliyo nzuri katika kuelezea jambo hilo, kwamba kwa nini wanaume na wanawake hudanganya katika mapenzi.

Nitajaribu kuwaeleza sababu (Lakini sababu hizi ni za wapenzi wapya.).

Ninachoweza kusema ni kwamba wanawake na wanaume hudanganya lakini wakiwa na sababu tofauti. Katika mapenzi kila mmoja anajaribu kukwepa kumuumiza mwenzake kihisia na hapo ndipo wanawake na wanaume hujikuta wakidanganya ili kukwepa kuwaumiza wenzi wao kihisia.Wanaume wengi hudhani kwamba kwa kuwa wanawake ni viumbe wenye hisia basi hawawezi kukubali kuambiwa ukweli na hapa chini nitataja mifano ya uongo mzuri (sijui kama ni sahihi kuita hivyo) ambao wanaume huutumia ili kuepusha shari na wenzi wao……..
black-couple-eating1-378x414.jpg

Mh, we ni mpishi mzuri….!
Kama inatokea siku mapishi yanakutupa mkono na unagundua kwamba chakula ulichopika hakina ladha au mchuzi umechachuka, ni vyema ukakiweka kando na kutafuta namna nyingine. Unaweza kwenda kununua chakula kwenye mighahawa ya karibu (Take Away) na kumuandalia mpenzi wako. Usitarajie mpenzi wako akakwambia chakula ni kibaya, atakisifia sana na huenda akakila chote ili kukuridhisha, lakini moyoni mwake anajua hicho chakula hata mbwa asingethubutu kukitoa mdomoni…. Anachofanya ni kuepusha shari ili amani iendelee kuwepo

125751777-e1348072150995-328x414.jpg

Kweli vile sikupata ujumbe wako wa simu…
Inaweza kutokea mwanaume anataka kutoka kidogo na marafiki zake baada ya kutoka kazini, lakini anashindwa kumwelezi mpenzi wake kwa kuhofia maswali, hivyo huamua tu kuungana na marafiki zake na kuiweka simu yake silencer ili kuepuka simu za mpenzi wake atakapopiga ili kujua amechelewa wapi. Atakaporudi nyumbani na kuulizwa na mkewe mahali alipokuwa, atasingizia kazi nyingi, foleni za magari au atasingizia kwamba simu yake ina tatizo la network nk. Kwa hiyo ukikutana na utetezi wa aina hii kubali yaishe.
OfficeWomanManBoss620480.jpg

Leo nitalazimika kufanya kazi hadi usiku…
Wakati mwingine kama mwanaume ana mishemishe zake na anahisi atacheleawa, ili kuepusha maswali atakayoulizwa na mpenzi wake anatoa taarifa mapema kuwa atachelewa kurudi kwa kuwa kuna kazi muhimu au kuna ripoti anaiandaa ambayo ni muhimu sana. Kwa kutoa taarifa ya aina hiyo mapema, anajua kabisa kwamba ataepusha usumbufu wa kupigiwa simu mara kwa mara na kuulizwa yuko wapi. Sio kwamba analazimika kusema uongo wa aina hiyo kwa sababu anayo dhamira ovu, la hasha, inaweza kuwa anataka kujiunga na marafiki zake kwa ajili ya kupata kinywaji au kuangalia mechi muhimu na marafiki zake na asingependa kupata usumbufu wa mara kwa mara wa kupigiwa simu ili kuulizwa mahali alipo na anachokifanya. Sitetei kwamba ni sahihi wanaume kufanya hivyo bali ninachojaribu kueleza hapa ni
ni kuwajulisha wanawake kwamba jambo hilo huwa lipo……

Woman-waiting.jpg

Nitakupigia…..
Inatokea mwanamke anakutana na mwanaume kwa ule mtindo wa chapchap, wazungu wenyewe huita one night stand. Baada ya kumalizana, mwanaume anaagana na mwanamke akimwahidi kwamba atampigia simu baadae. Naomba mfahamu kwamba kwa mwanaume kusema atakupigia, anamaanisha huenda atapigia simu. Ni wanaume wachache sana wanaoweza kutimiza ahadi walioweka ya kupiga simu baadae kwa mpenzi waliyeachana muda mfupi uliopita. Ili kuondokana na jakamoyo ni vyema ukaendelea na shughuli zako na wala usiwe na matumaini makubwa ya kusubiri kupigiwa simu. Iwapo atapiga sawa, lakini akipotezea haitakuumiza.


cheating-black-man.jpg

Wala nilikuwa simwangalii yeye…..

Hiki nacho ni kichekesho cha uongo wa wanaume. Inaweza kutokea mwanaume yuko na mwenzi wake wanatembea, mara wanakutana na mwanamke akiwa na hamsini zake, lakini mwanaume huyu anageuka kumtazama mwanamke huyo na anajisahau kiasi cha kumsindikiza kwa macho. Mara nyingi wanaume hupenda kukodolea macho matiti ya wanawake, makalio au eneo lolote la mwanamke linaloamsha hisia za mapenzi. Inapotokea akaulizwa na mwenzi wake kwamba kwa nini anamkodolea macho mwanamke fulani, mwanaume huyo atakanusha vikali kwamba hakuwa anamuangalia huyo mwanamke wakati ni dhahiri kabisa alikuwa anamkodolea macho. Kwa kawaida wanaume hukodolea wanawake macho bila wao kujijua na ndio maana hufanya hivyo hata wakiwa na wenzi wao, lakini cha ajabu wakiulizwa hukanusha vikali.

Nitaendelea kuwaletea uongo wa wanaume kwa kadiri nitakavyopata muda.....

 
Baba wa uongo ni shetani na uongo unamaanisha ukweli haupo

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
 
na wewe ulietangaza bikira humu?tukuiteje?

Mimi si muongo!!! NASISITIZA NI UKWELI MPAKA ATOKEE MTU WA KUTHIBITISHA PASI SHAKA YOYOTE KUWA IM NOT!!!!! NA KUWA NILIMPA KIDUDE, ATOE NA SUPORTING EVIDENCE!!!! For the time being im queen virgin here!!! Hahaaaaaa! Unasonyaje kimya kimya!!!! LOL! FOR THE TIME BEING IM INOCENT UNTILL PROVEN GUILTY!!!! Hahahaaaaa! TRUST ME IM ENJOYING WHILE IT LASTS!!!!
 
Mimi si muongo!!! NASISITIZA NI UKWELI MPAKA ATOKEE MTU WA KUTHIBITISHA PASI SHAKA YOYOTE KUWA IM NOT!!!!! NA KUWA NILIMPA KIDUDE, ATOE NA SUPORTING EVIDENCE!!!! For the time being im queen virgin here!!! Hahaaaaaa! Unasonyaje kimya kimya!!!! LOL! FOR THE TIME BEING IM INOCENT UNTILL PROVEN GUILTY!!!! Hahahaaaaa! TRUST ME IM ENJOYING WHILE IT LASTS!!!!

Unanikumbusha enzi za Sinta!!
 
Sie tuliovuka hizi songombingo ngoja tujisomee mawaidha ya wahusika, ingawa naona kama wanachungulia na kukaa kimya.
 
Usidandie TRENI KWA MBELE!!! Ohooooo! The Boss KAKIMBIA MZIKI HUU WA CD 700. LOL!!!! Better be neutral for your own good!

Who are you by the way, unatisha tisha watu....!
Yaani mwanamke mmoja uwashinde wanaume wooote humu JF, na ninakuhakikishia mwaka huu hauishi, mwanaume waukweee ataondoka na hiyo kitu unayoringia........LOL
 
Atangaze namba hadharani kama anajiamini ye mkareeee... Anajivua kufuli mwenyewe na anabembeleza amegwe... Chezea vijana nini... K lyn amekimbilia kwa mzee machache baada ya kuchoka kuvulia kufuli vijana then anaambulia maumivu tu... Na huyu sasa hivi atakimbilia kwa azam
 
Who are you by the way, unatisha tisha watu....!
Yaani mwanamke mmoja uwashinde wanaume wooote humu JF, na ninakuhakikishia mwaka huu hauishi, mwanaume waukweee ataondoka na hiyo kitu unayoringia........LOL

Hahahahaaaaaa! Bwana Mtambuzi badala ya kubembeleza mtoto huko, waja kunichokoza JF! LOL! Mamangina mikono ishamuuma! :focus: MIMI UBISHI WANGU NA HAWA VIDUME NI KUWA, MTU SIJAWAHI KUKUONJESHA KIDUDE HATA SIKU 1 UNABISHAJE HADHARANI KUWA MIMI SIO UNUSED!!!!! WHY!!! Nikiwabana balls zao WATOE EVIDENCE KWA MADAI YAO HAFIFU HAO WANAKIMBIA!!! Waache MAJUNGU!!! Unaweza kumponda demu ulielala nae tu kuwa sio unused wengine wote waliobaki as long as hujaonja, GIVE THEM THE BENEFIT OF THE DOUBTS!!!! LOLEST!!!!
 
mh !na humu mukonfesni yote tukianzia na Mtambuzi,sijui leo umemdanganya vipi mama ngina ili usibembeleze mtoto
then aje hapa The Boss nae aseme anamdanganyaje mama the boss
kisha aje my pacha kakaangu aliyeniachia ziwa SnowBall
akimaliza aje mtani wangu platozoom
kisha amalizie mwanafunzi wangu Kaizer
wakishamaliza atakuja retired officer Dark City
hawa wakishasema uongo wao BAK aje atupe wimbo wowote unaoendana na hii mada
hatua zoote hizo zikipitiwa wala haitakuwa na haja ya Mtambuzi kurudi humu!lol!
 
Last edited by a moderator:
Usidandie TRENI KWA MBELE!!! Ohooooo! The Boss KAKIMBIA MZIKI HUU WA CD 700. LOL!!!! Better be neutral for your own good!

Who is The boss anyway?Kuna mziki gani hapo?Mbona tumeshajua tayari?Unadhani ni mdomo ndo unazungumza?If ur telling the truth,kwa nini unajaa povu mtu anapokubishia?
 
Who are you by the way, unatisha tisha watu....!
Yaani mwanamke mmoja uwashinde wanaume wooote humu JF, na ninakuhakikishia mwaka huu hauishi, mwanaume waukweee ataondoka na hiyo kitu unayoringia........LOL

waondoke nayo mara ngapi?
ukiona hivyo ujue hata kusema tu ni scandal
so wanaondoka nayo kimya kimya lol
 
Who is The boss anyway?Kuna mziki gani hapo?Mbona tumeshajua tayari?Unadhani ni mdomo ndo unazungumza?If ur telling the truth,kwa nini unajaa povu mtu anapokubishia?

Where is Kaunga?
 
Last edited by a moderator:
Who is The boss anyway?Kuna mziki gani hapo?Mbona tumeshajua tayari?Unadhani ni mdomo ndo unazungumza?If ur telling the truth,kwa nini unajaa povu mtu anapokubishia?

Hahahahaaaaaaa! Ndo maana NIMEKWAMBIA USIDANDIE TRENI KWA MBELE!!! Wewe hii mada umeikuta leo umeidandia tuu! Hujui orig yake wala chanzo cha The Boss kutoa hizo shutuma! Mtambuzi anaelewa chanzo ndo maana sijamshangaa kuchangia! Sasa wewe ona unavotapatapa huelewi A wala B. Mimi IM TELLING THE TRUTH AS LONG AS HAKUNA ANAYEWEZA KUPROVE WITHOUT DOUBT IM LYING!!! Hujajua chochote bado UPO GIZANI SANAAAA! Kama umeamua kubisha USIBISHIE MSULI, TOA SUPPORTING EVIDENCE KUWA IM NOT WHAT I CLAIM TO BE!!!Otherwise ni MAJUNGUNIZATION!
 
Last edited by a moderator:
waondoke nayo mara ngapi?
ukiona hivyo ujue hata kusema tu ni scandal
so wanaondoka nayo kimya kimya lol

YOU WISHHHHH! Acha majungu na fitina! KUWA MSOMI TOA EVIDENCE HAPO ZA KISOMI KUWA MADAI YAKO IM NOT YANA UZITO
 
Back
Top Bottom