Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 37,916
- 46,658
Nimemsikia mmojawapo wa wachungaji wa KKKT akilalamika na kusikitika kuhusu wanawake wengi zaidi kuzidi kuimarika kiuchumi kiasi cha wanaume kushindwa kuwamudu. Ameenda mbali zaidi akiwataka waumini wake wanaume kwa wanawake kukemea roho hiyo ya aliyoiita ya Yezebel!
Huko Kenya mke wa makamu wa Rais ni mwanaharakati wa utetezi wa wanaume! Pia kumeibuka harakati kubwa za kinachoitwa kumpambania "boy child" kutoka kwa wanaharakati mbalimbali. Wapo pia wanaopiga kelele za kuongezeka kwa single mothers wakilaani na kulaumu mmomonyoko wa maadili wa wanawake kama chanzo kimojawapo.
Kinachokosekana kwa wengi wa wachungaji hawa wanaharakati wa boy child na raia wengine wengi kuhusu suala la usawa wa kijinsia kuzidi kuimarika na wanawake kuzidi kufanikiwa ni ukosefu wa maarifa ya kihistoria na evolution.
Kwa ufupi ni kwamba katika kipindi kirefu cha historia ya mwanadamu mafanikio makubwa ya kiuchumi, uongozi na jamii yalitegemea nguvu za misuli zaidi na aggressiveness ya mtu ila kadri muda ulivyoendelea mafanikio ya binadamu yamezidi kuegemea zaidi uwezo wa akili.
Pia kutokana na mambo na mazingira hayo kwa muda mrefu zaidi wanawake walikuwa wakitegema wanaume kwa ajili ya kupata mahitaji yao na hasa zaidi ya watoto wao hali iliyowafanya wakukubali kuwa chini ya dominance ya wanaume. Mazingira ya sasa yamebadilika sana na yanazidi kubadilika kutohitaji misuli na mabavu bali akili kwa ajili ya kupata mafanikio na mahitaji ya maisha na hii inapelekea mabadiliko makubwa ya usawa wa kijinsia kwa sababu binadamu wa jinsia zote wana kiwango sawa cha akili.
Wachungaji na wanaharakati wengine wa wanaume au "boy child" msihangaike kuwapigania watoto wa kiume hakuna conspiracy dhidi yao wanaume wala hakuna masuala yoyote ya kiroho, ni mabadiliko ya kimazingira na evolution inayoendelea kutokea taratibu vinavyoratibu huu usawa unaotishia nafasi ya mwanaume.