Wanaume wa karne hii mmekumbwa na nini?

Wanaume wa karne hii mmekumbwa na nini?

Habari wadau wa jf
Hakika waswahili husema ukishangaa ya musa utayaona ya firauni
Sielewi baadhi ya wanaume wa siku hizi wamepatwa na nini

Miezi minne ilopita nilifahamiana na kaka mmoja jirani na ofisi nayofanyia yeye alikuwa ni mfanyabiashara.

Basi tulizoeana na mwisho akaniapproach na tukajikuta tumeanza mahusiano.

Aliniambia anakoishi kuwa amejenga na anaishi na wadogo zake wawili mmoja ke mwingine me

Na hao wote nilifanikiwa kuwaona hapo kwenye biashara yake.
Basi nami nilimweleza napoishi hivyo, basi week ya kwanza tu akawa anatamani sana tuonane faragha, alipogusia hilo tu nilimpa msimamo wangu kuwa siwezi kufanya hicho kitu kabisa mpaka hapo tutakapokuwa na ndoa kama kweli anamanisha.

Basi, alikubali, muda ukaenda kwa kuwa aliniambia kajenga nikaona kama ni mpenzi wangu ni muhimu angalau kufahamu anapoishi, nilipomgusia suala la kwenda kwake aligoma kabisa akasema haitaleta picha nzuri mimi kwenda pale na wadogo zake wakiwepo, nikawa sielewi mwanaume wa 30+ anaofiaje wadogo zake?

Kuna mambo mengi nikawa nashangaa kuna siku akaniambia jiandae weekend hii tutaenda garden flan ambayo ni sehemu tulivu tunaweza kuongea mipango yetu na kubadilishana mawazo, nikakubali weekend nikajiandaa akaja na boda amepakiwa akasema panda (mshikaki) nikatamani kugoma ila nikavumilia boda akaanza kutembea nikashangaa nimeshushwa nyumba ya udongo yenye pazia la kanga nikahisi labda kuna ishu anafata nikamuliza hapa ndo rose garden? Akasema hapa ni kwa John(kijana wake wa dukani) kuna kitu nataka tuchukue then tuendoke, nikasema poa chukua twende, akasema ingia upaone nikagoma, (kumbe alishakodi geto ya huyo dogo ili apige mambo )lakini akashindwa kuniambia akanidanganya so hapo nikiingia tu story inabadilika

Nikamwambia ingia ngoja nifike dukani nichukue maji ya kunywa na pipi nakuja akasema poa, nilichukua boda boda nikamwambia akimbize anirudishe home.

Kesho yake akaanza kuomba misamaha mingi sana, nikamsamehe
Maajabu mengine nikifika dukani kwake anasema una elfu tano hapo hebu mara moja, ndo inaondoka mazima
Naenda dukani kwake nakaa anasema hebu mkoba wako anaatafuta hela akipata buku anaangiza soda nikiuliza anasema nitakulipa
Basi tabia hizo zikaendelea, kuna siku akaenda dsm kufata mzigo akiwa huko akapiga simu yuko moto flani naomba nisaidie laki mbili nikija nitakurefund kuna bidhaa zimeongezeka, dah nikaona ni mtu wangu nimsaidie dakika hiyo hiyo nikamrushia aliporudi alikaa zaidi ya week mbili hadi nikawa mkali ndo akaanza kunilipa tena kidogo kidogo

Siku moja nikawa nadaiwa hela flani na fundi sasa nikapelewa na 30k nikampigia nisaidie 30k by tomorrow nitakurejeshea akasema hana, je jioni ukishauza akasema hana dah niliumia sana

Ikaisha kama week zilikuwa tareh za mshahara nashanga naitwa beby, honey mke wangu mzuri, a kasema kuna jambo anataka tuongee basi tukakutana mKe wangu unajua nina malengo makubwa sana na wewe sasa week ijayo naenda karikoo ila hela yangu imepelea najua mshahara tayari umetoka naomba laki tano nikija niuze uze na wewe utaenda kuchukua mzigo nikirudi, nikamwambia siwezi kabisa kumkopesha Mana na mimi nitaenda kufata mzigo kariakoo siku si nyingi nikamnyima.

Kufupisha stori nilipigwa mizinga ya bila kujishtukiza hadi najicheka hizi elfu zangu, elfu mbili, elfu tano dah, nilipokuja kushtuka tuna miezi miwili ya mahusiano ila nishakopwa hadi sijielewi nikamwambia imetosha, umekuja kwangu kunichuma sasa imetosha.

Baadhi ya wanaume wenye hizi tabia mjirekebishe, raha ya mwanaume hugharamikie si ugharamikiwe
utafiti wako ni fake yaani mwanaume mmoja unamchkua sample then una generalize wanaume wote,,,,?
 
Pole dadake huyo angekupausha tu
Acha kabisa, mpaka naachana naye nilikuwa namdai elfu 35 nilizomkopesha acha sile za mizinga ambazo sidai na simu ya tochi aloniazima.

Bada ya kuachana naye nikamwambia anilipe deni na aniletee simu, akasema poa pitia kesho kesho yake nikapita dukani kwake akasema nakuja ngoja nikufatie hela yako benki kwenye atm iliyopo tu jirani akachukua boda akaniacha hapo akasema anakuja bada ya dakika tano, uwezi amini nilikaa masaa mawili na nusu hakuja kumbe ilikuwa mbinu ya kunikimbia, basi nikadai mpaka nikachoka

Nikakaa nikasema kwenye maisha kama ni hasara nilishapata nyingi sana acha na hii simu na hizzi hela zangu nione kama hasara nyingine nazitoa sadaka kama ataniletea fyn kama asipoleta fyn sontadai nikaiambia nafsi yangu kila ukikumbuka simu na hizo hela ukaumia tazama magari ya mafuta yanayolipuka na kumwagika kila siku, tazama magorofa yanayoanguka je wamiliki wanafanyaje dah hiyo ikanipa faraja nikakubali kuwa nimepoteza nikajisamehe maisha yakaendelea
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] Duuh jamaa hapanaa mpaka anataka kukulia kwenye nyumba ya Udongoo.. alikushusha thamani sanaa
Ni ubahili mana uwezo wa kwenda hata garden au sehemu nzuri anajua pale tutakula au tutakunywa au tutalipa kiingilia so anidanganye ili niingie geto chafu la kuazima

Yani wakati naondoka lile eneo naona aibu sijekutana na mtu anayenijua natokea kanyumba kabaya hahhaha kaudongo mungu wangu sitaki kukumbuka
[emoji22][emoji22][emoji22][emoji22][emoji22][emoji22]
 
Ni ubahili mana uwezo wa kwenda hata garden au sehemu nzuri anajua pale tutakula au tutakunywa au tutalipa kiingilia so anidanganye ili niingie geto chafu la kuazima

Yani wakati naondoka lile eneo naona aibu sijekutana na mtu anayenijua natokea kanyumba kabaya hahhaha kaudongo mungu wangu sitaki kukumbuka
[emoji22][emoji22][emoji22][emoji22][emoji22][emoji22]
Noma sanaa[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Huyo jamaa hatarii
 
Na wewe una moyo yani Mimi jianaume hata kwake halinionyeshi hata Ndugu zake Wa karibu siwajui yani sielewielewi kiukweli hata 50 simpi maana inavyoonekana ana Mke shoga ukitaka kujua ukweli siku akifunga mfatilie nyumanyuma kiaina hapo alikuwa anakugeuza sijui buzi ivi wanawake wanaochunwa wanaitwaje vile
 
Shida yote unajua imeanzia wapi dada? Kumnyima tunda.

Wanaume wachache Sana wanaweza vumilia hii kitu na bado akakupenda kwa dhati

Elewa hivyo tu
Hapana tabia hiyo ipo damuni ukiachia mbali suala la kumnyima, nikitu ambacho alishakizoea yani trik zake ni kama alikuwa na phd ya ukanjanja
 
Pole mkuu katudhalilisha sana wanaume hizo sio sifa za wanaume wa kweli. Wanaume wa kweli huwa tunajitanabaisha kwa kuwa responsible ila usikate tamaa wanaume wa kweli bado tupo
Sina hamu kabisa, yani kuna siku nilimpigia simu usiku naomba anitumie buku 2 niunge kifurushi mana alikuwa bado dukani, akasema sawa akafika dukani akapiga simu umesema buku au buku jero hahahha nikamwambia nimesema buku mbili dah hakuamini kama elfu mbili inamtoka hivi hivi
 
Usikwepe majukumu, ujue anakupima, kama siku akikosa chapaa, utaweza vumilia, vile uko "financially stable", mpe akili na pesa yako yote, ajue kuwa uko "wife material", ile siyo taka "divorce after honey moon night".
 
Back
Top Bottom