Wanaume wa karne hii mmekumbwa na nini?

Wanaume wa karne hii mmekumbwa na nini?

Lady of Destiny1

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2019
Posts
588
Reaction score
869
Habari wadau wa jf
Hakika waswahili husema ukistajabu ya musa utayaona ya firauni
Sielewi baadhi ya wanaume wa siku hizi wamepatwa na nini

Miezi minne ilopita nilifahamiana na kaka mmoja jirani na ofisi nayofanyia yeye alikuwa ni mfanyabiashara.

Basi tulizoeana na mwisho akaniapproach na tukajikuta tumeanza mahusiano.

Aliniambia anakoishi kuwa amejenga na anaishi na wadogo zake wawili mmoja ke mwingine me

Na hao wote nilifanikiwa kuwaona hapo kwenye biashara yake.
Basi nami nilimweleza napoishi hivyo, basi week ya kwanza tu akawa anatamani sana tuonane faragha, alipogusia hilo tu nilimpa msimamo wangu kuwa siwezi kufanya hicho kitu kabisa mpaka hapo tutakapokuwa na ndoa kama kweli anamanisha.

Basi, alikubali, muda ukaenda kwa kuwa aliniambia kajenga nikaona kama ni mpenzi wangu ni muhimu angalau kufahamu anapoishi, nilipomgusia suala la kwenda kwake aligoma kabisa akasema haitaleta picha nzuri mimi kwenda pale na wadogo zake wakiwepo, nikawa sielewi mwanaume wa 30+ anaofiaje wadogo zake?, any way nikawa mwelewa nikapotezea asione naforce sana.

Kuna mambo mengi nikawa nashangaa kuna siku akaniambia jiandae weekend hii tutaenda garden flan ambayo ni sehemu tulivu tunaweza kuongea mipango yetu na kubadilishana mawazo, nikakubali weekend nikajiandaa akaja na boda amepakiwa akasema panda (mshikaki) nikatamani kugoma ila nikavumilia boda akaanza kutembea nikashangaa nimeshushwa nyumba ya udongo yenye pazia la kanga nikahisi labda kuna ishu anafata nikamuliza hapa ndo rose garden? Akasema hapa ni kwa John(kijana wake wa dukani) kuna kitu nataka tuchukue then tuendoke, nikasema poa chukua twende, akasema ingia upaone nikagoma, (kumbe alishaazima geto ya huyo dogo ili apige mambo )lakini akashindwa kuniambia akanidanganya tunaenda garden so hapo nikiingia tu story inabadilika

Nikamwambia ingia ndani ngoja nifike dukani nichukue maji ya kunywa na pipi nakuja(vile alivo mbahili hata akugoma akaona niende tu, nafikiri angekuwa mwanaume wa kweli angeenda yeye na angelipia vinywaji na kuja navyo) vile anapenda slope akasema poa nenda kumbe mimi narudi nyumbani pale siingii hata kwa dawa, nilichukua boda boda nikamwambia akimbize anirudishe home.

Kesho yake akaanza kuomba misamaha mingi sana, nikamsamehe
Maajabu mengine nikifika dukani kwake anasema una buku hapo hebu mara moja, ndo inaondoka mazima
Naenda dukani kwake nakaa anasema hebu mkoba wako anatafuta hela akipata buku anaangiza soda nikiuliza anasema nitakulipa
Basi tabia hizo zikaendelea, kuna siku akaenda dsm kufata mzigo akiwa huko akapiga simu yuko moto flani naomba nisaidie laki mbili nikija nitakurefund kuna bidhaa zimeongezeka, dah nikaona ni mtu wangu nimsaidie dakika hiyo hiyo nikamrushia aliporudi alikaa zaidi ya week mbili hadi nikawa mkali ndo akaanza kunilipa tena kidogo kidogo

Siku moja nikawa nadaiwa hela flani na fundi sasa nikapelewa na 30k nikampigia nisaidie 30k by tomorrow nitakurejeshea akasema hana, je jioni ukishauza akasema hana dah niliumia sana mana kwa jinsi ambavyo nilikuwa namkopesha hela kubwa sikutegemea ashindwe na elfu 30 na kwa biashara yake uhakika wa kuuza more than hiyo upo, nikapiga moyo konde nikaazima kwingine

Ikaisha kama week zilikuwa tarehe za mshahara nashanga naitwa beby, honey mke wangu mzuri, akasema kuna jambo anataka tuongee basi tukakutana mKe wangu unajua nina malengo makubwa sana na wewe sasa week ijayo naenda karikoo ila hela yangu imepelea najua mshahara tayari umetoka naomba laki tano nikija niuze uze na wewe utaenda kuchukua mzigo nikirudi, nikamwambia siwezi kabisa kumkopesha Mana na mimi nitaenda kufata mzigo wangu kariakoo siku si nyingi nikamnyima.

Katika kipindi cha mwezi mmoja kulikuwa na mipango mingi sana mara tufungue duka letu tunachanga mtaji then tunaweka mtu ( namshukuru mungu hili wazo niligoma japo misisitizo ilikuwa mingi)

Kufupisha stori nilipigwa mizinga ya bila kujishtukiza hadi najicheka hizi elfu zangu, elfu mbili, elfu tano dah, nilipokuja kushtuka tuna miezi miwili ya mahusiano ila nishakopwa
hadi sijielewi nikamwambia imetosha, umekuja kwangu kunichuma sasa imetosha.

Baadhi ya wanaume wenye hizi tabia mjirekebishe, raha ya mwanaume hugharamikie si ugharamikiwe
 
Hahaha ...daah kuna wanaume baadhi yetu ni wahuni sana .

Pole sana mkuu ----, uliweza vipi kuji-connect na mtu mwenye tabia za kihuni kiasi hicho !?
Alikuwa ni very innocent, yani huwezi mdhania niliona nimepata bonge la gentleman, dah alivyoanza kusema una buku hapo? Mara ya kwanza ya pili ya tatu 'nikaanza kushtuka tho sikutake action nikijua maybe atabadilika duh nakaribia kufilisiwa kila anachoona kwangu anakiomba, kuna matofali yalibaki akayaona nyumbani akasema haya si hayana kazi nina mahali nataka kujenga nayaomba my God, sijui nilikutana wapi na huyu kupe
 
Back
Top Bottom