Wanaume wa Jf "hala hala na mke wangu

Wanaume wa Jf "hala hala na mke wangu

hearly

JF-Expert Member
Joined
Jun 19, 2014
Posts
54,346
Reaction score
80,219
Yapata mwezi mmoja ( 1 )sasa Tangu nilipoanza kubaini kuwa Tabia ya mke wangu imebadilika " jinsi alivyo hivi sasa sio Yule mke wangu niliyekuwa namfahamu miaka minne (4) iliyopita
Mwanamke Ambaye aliyekuwa ananifanya nitembee kifua mbele mithili ya mtu aliyepigwa ngumi ya mgongo mbele ya ndugu na marafiki zangu ' na kumuita Wife material
Lakini haya mabadiliko ya ghafla yaliyojitokeza dhidi ya mke Wangu Yalianza kunipatia simanzi ya Moyo wangu " nikaamua kuanza kumfanyia uchunguzi'

STORY KAMILI IKO HIVI
======================
Majuzi baada ya kuona kwamba Tabia ya mke wangu inazidi kubadilika na kuvuka mipaka "(kutwa nzima anashinda on-line" akipika chakula kuna wakati huwa anajisahau mpaka kinaungua baadhi ya mahitaji ya ndoa haya timizi vile inavyopaswa/stahiki )

Nikaamua kumfanyia Uchunguzi wa ghafla kwa kina bila yeye kubaini kuwa Nina mkakati wa kumchunguza "....

Juzi nilipo rudi nyumbani nilimkuta akiongea na shoga yake kwenye simu huku wakisimuliana habari za Jf haswaa zinazo tokea kwenye hili jukwaa la MMU na Yanayoendelea huko PM..Nilipoingia ndani ghafla akakata simu na kuja kunilaki " nadhani hakuwa ametambua kuwa niliyasikia mazungumzo yake ,( niweke wazi kuwa mke wangu huyu hajui kuwa Mimi nimtumiaji wa Mtandao huu ninao uhusudu sana "

Basi ulipofika wakati wa kulala Mimi nikaingia ndani mapema ..huku nikijifanya kuwa Nina usingizi mno .nikawa nimemuacha sebuleni akiendelea kuperuzi online " ....ilipotimu usiku wa SAA 8 nikaamka nakumkuta akiwa amelala .... Nikaichukua simu yake nikachukua dole gumba lake nakuitoa lock ' kisha nikaanza kufanya upekuzi "

Nilipo elekea kwenye URL nikaingia sehemu ya history nikakuta simu inaonyesha kuwa alipita jf " nilipo jaribu kuingia nikakuta haja logout (dah!!kumbe mke wangu ni mdada ambaye I'd yake ni maarufu tu humu kiasi chake ")

Nikajaribu kusoma baadhi ya comments zake 'nikakuta akiwa ana bebishana na wanaume kadhaa kwenye majukwaa ya MMU Moyo ukapasuka ghafla ila nikajipa moyo kuwa kubebishana kwenye majukwaa ni mambo ya kawaida sometimes hata Mimi huwa nafanya lakini sio kweli kwamba huwa Nina mahusiano na hao ninao bebishana nao". Nikajitahidi kuvuta subira huku kijasho chembamba kikiwa kinanitoka"

Baada ya kupiga Moyo konde nikasogea mpaka kwenye ile sehemu ya bahasha na kuingia PM (huku moyo ukinienda mbio mithili ya gari la dereva maarufu wa mashindano ya langa langa lewis Hamilton)

Nilipofika pm ...looohhh salaaleee jamani jamani Moyo unauma mjue " Niliyojionea huko Acheni tu yameupasua moyo wangu " mpaka sasa nastaajabu kwanini bado ninaishi ..... Ikanibidi niende bafuni huko nakuanza kulia ...nimelia sana ndugu wasomaji kuna wakati nililia kwa sauti mpaka wife akawa ameamka .... Akawa ananiuliza (baba jack) mbona unalia una tatizo gani " basi najifanya kuzuga mke wangu kichwa kina niuma mnoo '.... Palivyo kucha nilishindwa hata kwenda kazini " nikaenda kununua pombe nakuzifakamia mnoo hiki kitendo kilifanyika baada ya wife kuwa amekwenda kazini ''Leo ni siku ya tatu(3) tangu nishuhudie Yale niliyo yasoma Kwenye Pm ya mke wangu '... Bado nahisi kama moyo unakatwa katwa na kisu "

Najua hata wife atapita hapa nakuusoma huu Uzi na atabaini kuwa nimeshajua Madudu yake anayo yafanya '.... Nimepanga kwenda kushtaki kwao (, ukweni ) nilichukua uthibitisho wa screenshot ambazo zina uthibitisho mpaka wa picture zake '....

Wakuu nitawapatia mrejesho baada ya hicho kikao '

Maombi yenu tafadhali Maana maumivu Nayo yapitia sasa najihisi kama vile nipo kuzimu "

===Wanaume wa JF hala hala na mke wangu nitakuja kumpiga Mtu Vodoo Aise " Niliowakuta Pm wote majina yenu nayahifadhi kwa sababu ya Sheria za Jf ...otherwise wote ninge waorodhesha hapa " ==



BTW --Hii ni fiction story tu haina uhalisia wowote ule na maisha yangu au ya mtu yeyote " ...
 
Back
Top Bottom