wanaume wa fesibuku wanapenda kweli?

Naombeni mnisaidie kidogo ili nipate kufahamu maana naona hii social network haina faida kabisa,
Mara ya kwanza tulionana fesibuku nililike picha yake hapo sasa ndo kosa baada ya hapo nikatumiwa namba mi sikuona hatari kwani nilichukulia kama social networking tukawa tunawasiliana alinialika nyumbani kwake sikwenda basi akanialika ofisini kwake.

Sikua na wasiwasi kwani nilijua ofisi ni sehemu yenye watu wengi hivyo hakuna baya linaloweza kutokea baada ya story za hapa na pale niliomba kuondoka akaomba anikumbatie bila hiyana nikakubali kumbe hilo ndo kosa langu hapo hapo mara akaanza na mabusu mara antaka na romance sikuweza kumkubalia ilibi nimng'ate kumbe ndo kama nilikua nampandisha hisia zaidi hakunielewa mara ulimi sikioni na kutaka kunichania blouse lakini sikukubali matokeo yake aliniumiza shingoni nikaondoka na alama.

Sio siri nilijuta sana ile siku na dakika hiyo hiyo nikadeactivate account yangu ili kujipa break kwanza,
Baadae alintumia message na kuniambia 'I love you' nikabaki najiuliza huko kunipenda ghafla kumetokea wapi au ndo love at first sight inavyokuwa?au alikua na kiu zake akataka kuzimalizia kwangu?
mimi sina hisia zozote juu yake zaid namuona kama rafiki embu nisaidieni mapenzi ndo huwa yanakua hivi?
wanaume wa fesibuku wanapenda kweli au wanataka kutimiza tu kiu zao?na ni sahihi kweli kupata mchumba fesibuku au mi sielewi

Sisi tuliojiajiri tunatumia fursa ya facebook kutangaza biashara zetu Welcome to Facebook - Log In, Sign Up or Learn More; siju wewe unatangaza sura au ku "LIKE" handsome boys wakikubusu kuna shida gani wakati ni handsome?
 
Ukiwa facebook unatakiwa kuwa makini sana,sio facebook tu na social network zingine,usiwe na haraka ya kukutana na mtu,
pia unatakiwa uwafahamu kwanza marafiki zake wa karibu,na kama ni mara ya kwanza ndo mmepanga kukutana na mtu
unatakiwa uende na rafiki yako bila hata kumwambia yeye kuwa mnaenda wangapi,huo sio upendo,anayekupenda lazima
akujali na kujali hisia zako na unachomwambia,just kuwa makini,wengine wanaupload pics zao za nyumbani,flat screens,
na vitu vingine vya gharama halafu pia wameandika na location wanazoishi,hiyo unasababisha pia uvamiwe na vibaka au majambazi,kuwa makini.
 
hawapendi.kwa sababu totoz wengi,na kila mmoja kajitahid kwenda photopoint.wanadate tu.hakuna love.
 
Nenda kafanye assignment we mtoto. Marafiki wa shule na wa mtaani kwenu hawakutoshi unataka uongeze wa FB, kule wengi pasua kichwa. Kuwa nao makini.
 
Pole mdada. Wanaume ni wanaume, haijalishi wa fb, jamiiforums wala twitter. Akili kichwani mwako.
 
Back
Top Bottom