Wanaume tutafute hela kwa juhudi zote

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
74,850
155,799
Wanaume wenzangu, tufanye kazi kwa bidii tutafute hela ili uzee wetu tuwe na uwezo wa kujitegemea. Hakikisha kwenye uzee wako una pesa zako mwenyewe za kukufanya usurvive. Sahau kuhusu watoto, na mama yao kwamba watakutunza. Wewe ndiye stranger pekee kwenye hiyo familia unayoiita ya kwako. Hiyo nyumba ni ya huyo mwanamke na watoto wake. Not yours.!
Babu yangu aliniambia kwamba mwanaume aliyeoa ni sawa tingatinga, ambalo linatengeneza barabara, lakini ikishakamilika linabebwa juu juu kwenye lori na kuondolewa, eti likitembea litaharibu barabara. Yani barabara ambayo tingatinga lenyewe limeitengeneza haliruhusiwi kutembea juu yake.
Vivyo hivyo kwa mwanaume aliyeoa. Atajinyima, atajishughulisha, atajizuia kufanya anasa, atakopa, atavaa mitumba ili tu watoto wake waishi vizuri, wale vizuri na kusoma shule nzuri. Siku hizi urithi pekee uliobaki ni elimu bora coz mashamba ziliishaga. Lakini pamoja na yote hayo, bado ukizeeka hao watoto sio wako, ni wa mama yao. Wewe watakuita "kamzee".
Watoto wakiwa na umri wa miaka 10 ndipo mama yao anaanza kuwajaza taarifa zisizovutia kuhusu wewe. Kadri wanavyokuwa ndivyo wanavyoelezwa mambo mengi. Wakifika utu uzima atawaambia "isingekua mimi hamgesoma, yeye alikua ni pombe tu na wanawake" Ukisikia hivyo ujue tingatinga limemaliza kazi yake sasa linakaribia kuondolewa barabarani.
Watoto wanapoanza kazi, mzee anakua amestaafu. Wanapokuja kutembelea wazazi, wakiondoka wanampa baba elfu 5 mbele ya mama. Halafu wanaenda jikoni na mama, wanampa hela kwa siri bila mzee kujua. Wakiondoka mama anamfuata mzee na kumwambia sukari imeisha. So ni suala la mzee kuamua kutoa ile elfu 5 aliyoachiwa na watoto ikanunue sukari, otherwise anywe chai isiyo na sukari. Hii ni moja ya sababu inayowafanya wazee kufa mapema baada ya kustaafu na kuacha wake zao wajane.
Nimeshuhudia wazazi wenye watoto ng'ambo wakimchukua mama yao akaenjoy life majuu, na kumuacha baba yao nyumbani akilisha ng'ombe zao mbili, na kutafuta chakula cha kuku.!
Wanaume work hard and save something for yourself at old age. Tafuta pesa kwa bidii, wape watoto elimu bora, wape mahitaji yao muhimu, jenga nyumba nzuri waishi vizuri, lakini ukizeeka dont expect too much from them. Enjoy maisha ya uzee kwa pesa zako mwenyewe ulizochuma ujanani. Kama huna hela utaumwa hata na mbwa yako mwenyewe.!!
 
Kwa hiyo baba akabaki analisha ng'ombe mbili wakati huu mama yuko majuu.
Wakuu hii inshu ina ukweli sana kama mfano ulio hai ni demu wa Sugu anavyofanya vituko
 
Hii kitu iko sahihi kabisa, na mifano anuai ninayo

Mkuu ubarikiwe kwa kuliona hili

Na ili kuliona hili vizur mwanaume aoe na kuanzisha familia yake
 
Daahh......sio siri hawa wadada wanapenda sana kujimilikisha mali zetu tukishazeeka.........wanazngua sana.....dawa ni kuwa na mali ambazo anazijua mama ako mzazi tu
 
Ndio mana mi nashauri jamani kuna haja ya unapowahudumia watoto iwe nguo, Ada, chochote kama tayari wanajielewa ebu fanya hivo mbele yao na mama yao akiwepo na siyo kumpa mama hera ndo awahudumie mana hizi zama wamama hawana huruma na sisi.
 
Dah, ukweli tupu, hebu tutolee vivid exAmple mkuu, ilikuajekuaje hadi ukatuletea challange hii iliyo mbele yetu walume ndago ,yaani nini kimesababisha uje na ushauri huu kwetu?

Back
Top Bottom