Wanaume tutafute hela kwa juhudi zote

Wanaume tutafute hela kwa juhudi zote

Nilishajiapiza sitegemei mtt au mtu ni kijinyonga mapema

Niliamua kuzaa lzm niwape haki yao ya msingi sihitaji malipo kabisa
 
Hiyo ni picha ya familia za uswahilini.

Ila familia za kujielewa nyingi sana mzazi wa kiume bado anathaminika na kutambulika.
 
Wanaume wenzangu, tufanye kazi kwa bidii tutafute hela ili uzee wetu tuwe na uwezo wa kujitegemea. Hakikisha kwenye uzee wako una pesa zako mwenyewe za kukufanya usurvive. Sahau kuhusu watoto, na mama yao kwamba watakutunza. Wewe ndiye stranger pekee kwenye hiyo familia unayoiita ya kwako. Hiyo nyumba ni ya huyo mwanamke na watoto wake. Not yours.!
Babu yangu aliniambia kwamba mwanaume aliyeoa ni sawa tingatinga, ambalo linatengeneza barabara, lakini ikishakamilika linabebwa juu juu kwenye lori na kuondolewa, eti likitembea litaharibu barabara. Yani barabara ambayo tingatinga lenyewe limeitengeneza haliruhusiwi kutembea juu yake.
Vivyo hivyo kwa mwanaume aliyeoa. Atajinyima, atajishughulisha, atajizuia kufanya anasa, atakopa, atavaa mitumba ili tu watoto wake waishi vizuri, wale vizuri na kusoma shule nzuri. Siku hizi urithi pekee uliobaki ni elimu bora coz mashamba ziliishaga. Lakini pamoja na yote hayo, bado ukizeeka hao watoto sio wako, ni wa mama yao. Wewe watakuita "kamzee".
Watoto wakiwa na umri wa miaka 10 ndipo mama yao anaanza kuwajaza taarifa zisizovutia kuhusu wewe. Kadri wanavyokuwa ndivyo wanavyoelezwa mambo mengi. Wakifika utu uzima atawaambia "isingekua mimi hamgesoma, yeye alikua ni pombe tu na wanawake" Ukisikia hivyo ujue tingatinga limemaliza kazi yake sasa linakaribia kuondolewa barabarani.
Watoto wanapoanza kazi, mzee anakua amestaafu. Wanapokuja kutembelea wazazi, wakiondoka wanampa baba elfu 5 mbele ya mama. Halafu wanaenda jikoni na mama, wanampa hela kwa siri bila mzee kujua. Wakiondoka mama anamfuata mzee na kumwambia sukari imeisha. So ni suala la mzee kuamua kutoa ile elfu 5 aliyoachiwa na watoto ikanunue sukari, otherwise anywe chai isiyo na sukari. Hii ni moja ya sababu inayowafanya wazee kufa mapema baada ya kustaafu na kuacha wake zao wajane.
Nimeshuhudia wazazi wenye watoto ng'ambo wakimchukua mama yao akaenjoy life majuu, na kumuacha baba yao nyumbani akilisha ng'ombe zao mbili, na kutafuta chakula cha kuku.!
Wanaume work hard and save something for yourself at old age. Tafuta pesa kwa bidii, wape watoto elimu bora, wape mahitaji yao muhimu, jenga nyumba nzuri waishi vizuri, lakini ukizeeka dont expect too much from them. Enjoy maisha ya uzee kwa pesa zako mwenyewe ulizochuma ujanani. Kama huna hela utaumwa hata na mbwa yako mwenyewe.!!
Please acknowledge the Author
 
Hiyo ni picha ya familia za uswahilini.

Ila familia za kujielewa nyingi sana mzazi wa kiume bado anathaminika na kutambulika.
Kwa uswahilini ni kweli inatokea Mara nyingi mama ananafasi kubwa kuwashawishi watoto maana anakuwa nao muda mrefu. Kunamzee hapa watoto na mama yao wanamuundia zengwe mzee hanaraha kabisa chai tu anaipata kwa mbinde
 
Mkuu Bujibuji nimekuelewa.
Maneno haya yameniingia kichwani kiukweli ukweli.

Nimevuta picha ya wazee wachache wanaosota kitaani hapa, nimetazama walivyokomaa na watoto enzi hizo na leo wazee wanakufa njaa ilihali wake zao wanang'ara Kama mabinti
 
Ukizaliwa mwanaume ni tabu kabisa. Wanaume wanahagaikia familia zao lkn akifika uzeeni mama na watoto humkejeli kwa sababu pato limepungua au hamna kabisa kama hakuwekeza.
Na kikazi chetu sijui kitakuwaje bila fedha you are nothing kwa mwanamke.
 
Mmh thanks bujibuji , nilikua nimeanza kuku underrate ila kwa ujumbr huu mkuu credit zako zimerud pale pale
 
Aisee....huo mstari wa mwisho kwamba 'mbwa wako mwenyewe atakung'ata' ina maana.....
 
Furaha ya mwanaume ni kuona wanae na mama yao waishi kwa furaha na amani kwa hiyo lazima baba utafute kwa nguvu zote na ndio maana wababa tunakufa mapema na kuacha wajane
 
te..teh...teh... tutaelewa tu! mpaka serikali hii iondoke tutakuwa tumeshajifunza mengi sana.
kwa kifupi wanaume wameshituka wanafanya auditing kwa kila fedha wanayodondosha na sasa wanafaa viatu vyao zaidi kwa kutazama mbele ambako wake zao hawatazami ili iwasaidie kuishi zaidi.
good!
 
Huu uzi naomba Mods wauhifadhi kwa faida ya kila kijana na mwanaume wa Tz.

Huu ni Uzi hamasishi maishani.
 
Back
Top Bottom