Umenikumbusha mwaka 2010 mtaa wa ohio dar es salaam..mida ya 11 jioni Nikamuona mwanaume mmoja almost kama 42 yrs akiwa anampiga makofi na mateke mwanamke mbele za watu mpaka akawa anavuja damu hakuna mtu aliyetokea kuwaamua, yule mwanaume alionekana amejazia Bausa. Baadae akachukua taksi na na kumwingiza yule mwanamke ndani kwa nguvu. Taksi ikaondoka mwendo kasi kupitia alihasani Mwinyi road
Kile kitendo kiliniumiza sana, katika maisha yangu nachukia uonevu na udhalilishaji. Kijana nikajitosa kichwa kichwa nami nikachukua taksi nikawa nyuma yao kama gari 3 hivi. Tulivyofika palm beach hotel kukawa na foleni kubwa nikashuka nikakimbia kwa miguu mpaka salenda police station nikaripoti tukio. nikapewa askari polisi 2 wenye silaha, ikawekwa road block pale salender, ile gari ilipofika ikaelekezwa iingie polisi station.
Wote wakachukuliwa nikiwepo na mimi, kumbe walikuwa mtu na mkewe! polisi wakaajitolea kumpeleka yule dada hospital akafungwa majeraha. Wakati huo yule bwana na mie tuko chini ya ulinzi..Yule dada amerudi almost saa 2 usiku, bwana akafunguliwa file la udhalilishaji, kupigana hadharani na kusababisha majeraha
Mashtaka yule mume anamshutumu mkewe ni malaya, kesi ikanigeukia mimi mume ananishutumu mie ni bwana wa yule mkewe, ukweli sikuwa nawafahamu hata kidogo. Huwezi amini niliwekwa lockup mpaka saa 8 usk, wakaja kudhaminiwa na ndugu zao wakaachiwa wote mie nikabaki lockup kumbe yule dada hakuondoka pale kituoni akarudi akanidhamini nikaachawa,dada akanikodishia taksi akanisindikiza mpaka getho kwangu ilala..
Kesho yake nikaripoti polisi baadae wakadrop ile kesi nikawa huru. Yule dada akawa ananipigia simu kunishukuru mwishowe it become happy ending........(dhambi ya happy ending nimeshatubu na kuacha.)
Ila Wanaume tutambue kabisa pshychological kumpiga mwamke unajidhihrisha wazi kwamba uwezo wako wa kufikiria ni mdogo kupita kiasi mpaka unaamua kutumia nguvu.. Lets be a real MAN