Wanaume tuoneeni huruma tu, inawezekana kweli tunawakosea

Chakorii

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
18,586
50,683
Habari za usiku.

Kwa masikitiko makubwa na huzuni isiyoyakawaida imeutawala moyo wangu.

Wanaume,inawezekana kweli tunawakwaza,iwe ni kwa kujua au kutokujua lakini haifanyi ukamwanika mke wako wa ndoa kwa mchepuko kwa kiwango cha lami kabisa

Leo nikiwa niko saloon nasafisha kucha, akaja mdada wa jirani na hiyo saloon niliyokuwepo(ni mashoga hawa)kaingia na simu ya mwanaume (mume wa mtu sasa) yule mwanamke (mchepuko) anamuonyesha shoga ake wa saloon picha za mke wa ndoa wa huyo mwanaume, jamani nilijihis kuzimia. Bora basi picha hizo ziwe za kawaida. Maskini ni picha za tumbo lake la ujauzito liko wazi bila nguo wala brah kumbe maskin ya Mungu dada wa watu keshajifungua ndo kwanzaa kaanza kunyonyesha mume kahamia kwa mchepuko.

Uzalendo walah ulinishinda ikabidi nimuulize huyo mwanamke,kwanini unamfanyia mwanamke mwenzio namna hii? ***** zake msenge yule alijua kunijibu nikajikuta nakalisha kalio chini aise.

Kwa madai ya mwanamke sasa anavyosema kuwa mwanaume hampendi mke wake kwa sasa kisa ananyonyesha hakuna kauli iliniuma kama hii jamani..aliongea mengi mno nashindwa kuyaandika hapa.

Na kwa anayoyasema inaonekana fika jamaa kam’bwagia mchepuko madhaifu ya mke

Wanaume, tubebeeni mapungufu yetu msiwasimulie michepuko madhaifu ya familia..shetani ndipo hupata mlango wa kuingilia na kutengeneza makazi.

Yes!tunajua hamuwezi kutulia na mwanamke mmoja basi kwa niaba ya wanawake wote ninaomba nichukue fursa hii kuwaomba wanaume,,mnapoenda kuchepuka,,nendeni na sehemu za siri pamoja na kondom akili ziache kwenye familia yako.

Sio kwa hiki nilichokishuhudia leo mchana..kimeuvunja moyo wangu vipande vipande nimejaribu kukivaa kiatu cha mke nikashindwa
 
Back to topic..
Watu wasioheshimu wengine nadra Sana kujiheshimu wenyewe pia..
Kupenda wengine kunaanzia na kujipenda wewe.. kuheshimu wengine ujiheshimu wewe Kwanza..

Mengine yote yanaepukika ukijali hivyo

Ni kweli kabisa The Boss mpaka sasa najiuliza ni akili za yule mwanaume au kalogwa🥺🥺🥺 ninakiri wazi mpaka sasa ninasikia uchungu wa ajabu nafsini mwangu.chozi lilinitoka nilishindwa jizuia kabisa
 
Back
Top Bottom