Wanaume tunaopenda kuvaa suti njooni tushauriane jinsi ya kuchagua rangi na aina za suti nzuri

Mukulu wa Bakulu

JF-Expert Member
Aug 12, 2014
4,051
12,949
Habari zenu ndugu.
Wataalam wanasema mwanaume angalau uwe na hata jozi moja ya suti kenye kabati lako la nguo.

Ni ukweli usiopingika kua suti humfanya mtu alieivaa kuonekana wa tofauti ila watu hua tunafanya makosa kwenye kuchagua aina na rangi ya suti na vipimo hivyo unakuta mtu umevaa suti lakini unaonekana kituko.

Kuvaa na kupendeza sio lazima uwe mwanamitindo au uwe na mshauri wa mavazi, mimi binafsi hua napenda kuvaa suti angalau mara moja kwa wiki au basi kwa mwezi mara mbili.

Suti ni koti, kama koti la suti halijashonwa vizuri likakukaa vizuri au haliendani na umbile lako basi suti nzima inaonekana kituko kwako.

Tuepuke makosa yatakayopelekea tusionekane vituko tuvaapo suti kama vile suti oversize, koti kua limeshonwa vibaya, suruali kua pana kupita kiasi na pia rangi ya suti na mahala unapoenda/tukio. Tuangalie pia maumbile yetu kama urefu, unene nk.

Katika rangi za suti mbazo hutakiwi kukosa ni suti nyeusi/rangi ya mkaa maana mimi naona kama hufaa karibu kila mahali isipokua kwenye matukio machache.

Mimi binafsi napenda rangi zifuatazo, nyeusi, blue, sky blue, charcoal. Aina nayoipenda ni single button na double vented.

Unakaribishwa kutoa maoni yako na ushauri, pia tunaweza kuelekezana wapi wanauza/shona suti nzuri na bei gharama, upatikanaji wa mapambo ya suti nk.
images (2).jpg
8ac98d49bbd2c4dc20a29203c87840f5.jpg
new-men-suits-sky-blue-single-breasted-wedding.jpg
images (3).jpg
images (1).jpg
 
Daaaahh ila hiyo style ya mwisho kitaa wanaita "Korean style" kwa sisi bongo sio suruali inakubana kama skin tight bhaana.! Inatakiwa ikae mkao tuu wa mwili wako cause kuna watu daah "TOO MUCH" kwenye kuvua sijui inakuwaje aisee.! Attire ni vazi nlipendalo sana cause ya my "Noble profession"
 
Daaaahh ila hiyo style ya mwisho kitaa wanaita "Korean style" kwa sisi bongo sio suruali inakubana kama skin tight bhaana.! Inatakiwa ikae mkao tuu wa mwili wako cause kuna watu daah "TOO MUCH" kwenye kuvua sijui inakuwaje aisee.! Attire ni vazi nlipendalo sana cause ya my "Noble profession"
Mkuu wewe ni lawyer?
Hivi suti nyeusi hua ni dress code yenu?

Ni kweli suruali isiwe 'modo' ikubane sana, inatakiwa iendane na mwili, sio pana sana wala ikubane sana.
 
Hivi tai inakiwa iandaen na shati au na nin uwa sielew kwny mpnglio tai inakuwa kwny kundi gani au inavaliwa na shati lolote tu??
 
Back
Top Bottom