Wanaume tuna Matatizo

Wanaume tuna Matatizo

technically

JF-Expert Member
Joined
Jul 3, 2016
Posts
13,553
Reaction score
57,843
Sio mpenzi sana wa jukwaa hili ila kuna tabia nimeiona imenishangaza baada ya kwenda likizo home kama unavyojua janga la corona.

Kuna wapangaji pale home huyu sasa ni mwalimu ameoa unamkuta anafua nguo za ndani za mkewe, nguo za mkewe watoto, anaosha vyombo na kupiga deki ndani duh! Ukweli kanishangaza na ukimcheki mke wake anaonekana mpole.
 
Piga kazi wewe kama huna kazi njoo nikupe kazi ya kushusha mapeto. Ya ndani ya ndoa waachie wenyewe
FB_IMG_15886848177506270.jpg

We jamaa unamatatizo makubwa kuliko Huyo anaeosha vyombo.
 
Mbona hakuna tatizo hapo. Mbali na kufua pia anaweza hata kumsaidia mkewe kupika na maisha ya upendo yakaendelea.
 
Usioyajua ni sawa na usiku wa giza,inawezekana mwenzio usiku anapata huduma ya kutosha,kwahiyo mchana anampa mama mapumziko na wewe unaona jamaa anaonewa...
 
Ni wivu tuu,...

Japo mm siwezi mruhusu mume wangu adeki hata kama ananipenda to the moon and back,.

Raha ya kudeki uiname,ujitikise tikise hasa maeneo flan huku mume anakuona,.sasa mume apige deki anataka kutikisa nini jomonii??lol

Aisee..
 
Sio mpenzi sana wa jukwaa hili ila kuna tabia nimeiona imenishangaza baada ya kwenda likizo home kama unavyojua janga la corona.

Kuna wapangaji pale home huyu sasa ni mwalimu ameoa unamkuta anafua nguo za ndani za mkewe, nguo za mkewe watoto, anaosha vyombo na kupiga deki ndani duh! Ukweli kanishangaza na ukimcheki mke wake anaonekana mpole.

Hayo ni mapenzi mkuu.

Wewe kama unashangaa mtu kufanya hivyo basi ujue wewe ni katili sana yaani hutaki hata mwanamke asaidiwe hizo kazi kana kwamba ni mwiko.

Kama unaweza kumsaidia rafiki yako kufua na kuosha vyombo vipi kwa mke usimsaidie wakati mke ni zaidi ya rafiki ?

Hapo utaona kuwa wewe kama umeoa basi unaishi maisha ya ajabu sana na mkeo na hauoni kama anahitaji upendo zaidi ya ule wa rafikiyo.
 
Ni wivu tuu,...

Japo mm siwezi mruhusu mume wangu adeki hata kama ananipenda to the moon and back,.

Raha ya kudeki uiname,ujitikise tikise hasa maeneo flan huku mume anakuona,.sasa mume apige deki anataka kutikisa nini jomonii??lol
Dah aisee.

Mimi kwa kweli wife ananisifia sana nadeki vizuri,sasa pengine isijekuwa natikisa sehemu unazosema aisee?
 
Back
Top Bottom