Extrovert
JF-Expert Member
- Feb 29, 2016
- 67,106
- 173,889
Jana katika pita pita zangu mitandaoni nikakutana na lile sakata la yule Bi. Mkubwa aliechezea vitasa mjini Moshi baada ya kuhusishwa na fumanizi flani.
Katika hali ambayo iliamsha hisia zangu zaidi ni mahojiano ambayo yalifanyika kati yake na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Mhe. Anna Mghwira ambapo mwisho wa siku aliamua kutoa ufafanuzi flani juu ya lile tukio kama kuhitimisha.
Alisema, "Kupendwa ni haki ya kila mtu hivyo hakuna sababu ya wanawake kupiga wenzao maana kimsingi hakuna kosa kwenye kupenda. Isitoshe mwanaume huwa anapenda kwa vipande vipande (sections) na huwa hapendi mwanamke mzima. Kwako atapenda pua, kule sikio, kule macho n.k. Wanawake wamejaaliwa nguvu ya pekee ya kupenda mtu katika uzima wake hivyo ni vyema wangejifunza kuishi na hilo badala ya kuumizana."
Kimsingi naona mama Anna Mghwira ametuinua kinamna flani japo ChrisMauki alitupondea. Pia, kamaliza ule utata wa siku nyingi kuhusu wanaume kuwa haturidhiki na mke mmoja, jamani warembo sie tunapenda kipande flani tu kwa kila mwanamke na ndio maana tunahangaika kukamilisha mwili mzima. Mtuelewe tafadhali wala msipigane πππ