Una maana gani!huyo shem wako mgonjwa
Una maana gani!
Mbona unamtuhumu mtu asiye na kosa?
Kosa lake ni kutomsechi bwanake mifukoni, au?
Duh huyo mwanaume ni balaa
Nyumba ya kupanga na bado anaambiwa apeleke milioni mbili na nusu
Ni matofali mangapi au ni mifuko mingapi ya cement au si anapata sehemu ya miguu ishirini kw aishirini nje kabisa ya mji wakati akisubiri amalizie bei ya manunuzi
Kweli akili ya kuambiwa changanya na ya kwako
Lakini kumbuka kuna theory inayosema usiweke mayai yako yote kwenye kapu moja. Nakumbuka niliambiwa na mwalimu wangu wa portfolio AnalysisHii sms jana mke wa ndugu yangu kaibamba kwenye simu ya mumewe ambaye alisevu jina la mtuma meseji kuwa anaitwa ' Mose fundi bomba':
'Mpenzi leo nimepita madukani Kariakoo.Bei ya vifaa ni hizi: Stima (500,000._), Draya(400,000.-), Stima ya fasho(200,000.-), viti (60,000.-) na sinki(600,000._). Fanya hima kesho (yaani leo) unipatie hizo pesa maana nasikia bei karibu zitapanda.Ukinipa milioni mbili na nusu zitanitosha na kununulia dawa za kuanzia.mmmmmwwwaaaa i love you,ikamalizia hiyo sms.
Wakuu timbwili linaendelea,na tatizo kubwa bi mkubwa mradi wake wa kuku umesimama mzee anasema hana hela na wanaishi nyumba ya kupanga. Kinababa haya mambo ya kuzima moto kwa jirani huku kwetu kunaungua matokeo yake ndo haya.
Nawasilisha.
hah maisha ndivo yalivo
Positive side ya stori: Abarikiwe mama kwa kuwa na mradi wa kuku.
Hapana, nilikuwa najaribu kuonesha umuhimu wa kinamama kujiandaa na situation kama hizi, sio unafuma meseji ya hawara hata pa kutokea huna, una makucha marefu mikononi tu na malipustiki ya India.Unataka kufunika kombe mwanaharamu apite au?