Wanaume tuache kujiendekeza

Ahsante kwa kuniombea MUNGU anitunze, nawe nakuombea kwa MUNGU azidi kukubariki, uje na mawazo mazuri zaidi ili tuzidi kupata elimu.
 
Sheikh Jurjan, umeandika kwa hasira na matokeo yake umechanganya mambo japo lengo lako ni zuri.

Ni hivi ukiona taasisi, kampuni, asasi au hata serikali inayumba au inafanya vuzuri angalia kiongozi mkuu aliyeko madarakani kisha chunguza mienendo yake kwa maana yeye (Kiongozi) ndiye anayeweza kuiwezesha serikali/taasisi yake kuwa na maendeleo mazuri au mabaya.

Vivyo hivyo katika taasisi ya ndoa/familia, Baba (Mwanaume) ndiye kiongozi na ndiye anayetegemewa kuongoza taasisi hiyo kuelekea katika mafanikio, sasa basi Baba akiwa imara na kuongoza kwa haki familia itasonga mbele na mafanikio yataonekana na hutosikia upumbavu wa haki sawa katika familia hiyo, Baba huyo huyo akiwa lege-lege (hasa kwenye utafutaji na maamuzi) ndipo manug'uniko, dharau, ujuaji (kwa ujumla uana harakati) huanza.

Najua changamoto za maisha zipo na zitaendelea kuwepo (maana hata mimi ninazo na ninazikabili ipasavyo) lakini kiukweli wanaume wengi hasa waliozaliwa kuanzia miaka ya 1990 wana tabia ya kujiliza-liza mbele ya wanawake ili kutafuta huruma kitu ambacho binafsi kinanikera (Mfano. MC Pilipili). Lengo la uzi huu ni kuwakumbusha wanaume wa aina hiyo kuwa wasitafute mtu wa kumbebesha mizigo ya lawama pale chombo kinapoenda mrama bali wajitafute ni wapi wamekosea na wajirekebishe ili chombo kirudi kwenye mstari.

Habari ya mapinduzi ya viwanda ipo zaidi kwenye Historia na Uchumi, wataalamu wa mambo hayo wapo jukwaa la uchumi na historia.

Karibu tena!!
 
Hv mtelezo n nn[emoji848]
Chief, Ahsante kwa swali lako zuri. Mtelezo ni neno la mpito (mengine ni kitonga, dezo nk) ikimaanisha mtu au watu wanopenda kupewa vya bure. mfano, kula chakula asichokitolea jasho (Hasa Wanaume)/ Kuwa omba omba wakati uwezo wa kufanya kazi anao.
 
Mbona hujaweka ""STATEMENT ABOUT BIKRA""

Jokajeusi njoo uone HII MBUZI

#YNWA
 
Kuna wanaume wanaudhalilisha sana uanaume wao.
 
"STATEMENT ABOUT BIKRA" ni mada inayojitegemea hata wewe unaweza kuiandaa siyo lazima awe Jokajeusi (Unatakiwa kujiamini). Hii mada inahusu wanaume wanaojiendekeza, halafu mimi ni Binadamu siyo mbuzi. Karibu uchangie.
Mbona hujaweka ""STATEMENT ABOUT BIKRA""

Jokajeusi njoo uone HII MBUZI

#YNWA
 
Reactions: Cyb
Siku ukitoka hapo kwa shemeji yako ukaanza kujitegemea utabadili kauli tuu
 
Siku ukitoka hapo kwa shemeji yako ukaanza kujitegemea utabadili kauli tuu
Uzuri na ubaya wa humu ni kuwa hatujuani. Mimi ni mzee nina wajukuu sasa na ninaishi nyumbani kwangu. Kuhusu Mashemeji nimeisha wasomesha na wanajitegemea kwa sasa.
 
Narudia pale pale wanavyosema wenzangu....imagine unaingia mjini kichwa kichwa unaoa mtu kama Mama Diamond, unafikiri mambo yakiwa mabaya huko mbeleni atakuambia nini kuhusu watoto wenu mliozaa na kuwalea?
 
Narudia pale pale wanavyosema wenzangu....imagine unaingia mjini kichwa kichwa unaoa mtu kama Mama Diamond, unafikiri mambo yakiwa mabaya huko mbeleni atakuambia nini kuhusu watoto wenu mliozaa na kuwalea?
.............Du! Huo ni mtihani japo waliyotangulia walitwambia kuwa kila mtihani una "heri" ndani yake, kuijua hiyo "heri" iliyopo ndani ni mpaka ufaulu mtihani husika.
 
Ukitaka kumjua mwanamke zijue tabia za Paka, wanawake wote duniani wana tabia kama za Paka, ndio Paka huyu huyu Nyau.

wewe kaa mchunguze Paka utazijua tabia za wanawake.
Adam mwenyewe hakumwelewa Hawa pindi Mungu alipomuuliza swali,, akajibu si huyu mwanamke uliyeniletea haaaaahaaaa.
 
Adam mwenyewe hakumwelewa Hawa pindi Mungu alipomuuliza swali,, akajibu si huyu mwanamke uliyeniletea haaaaahaaaa.
Adamu alishindwa kujitambua na kutambua nafasi yake, maagizo ya kutokula lile tunda la mti wa katikati alipewa yeye kabla ya Hawa, Sasa kwa kuwa alikuwepo kabla ni dhahiri alitakiwa kumuongoza Hawa. Lakini kwa kuwa hakujielewa yeye ni nani na nafasi yake kwa Hawa ni ipi hivyo alishawishiwa na akajikuta akipokea lile tunda na kulila.

MUNGU alipokuja kumuuliza, badala ya kukiri makosa na kuomba msamaha (toba), yeye akaanza kumlaumu Hawa. Kitendo cha yeye kumlaumu Hawa kwa upande mwingine kiliashiria kuwa MUNGU alikosea kumpa msaidizi (jambo ambalo siyo la kweli). HII INATUFUNDISHA KUWA TUNAPOKOSEA TUNATAKIWA KUKIRI MAKOSA YETU NA SIYO KUTAFUTA MTU WA KUMTWISHA LAWAMA.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…