Wanaume tuache kujiendekeza

Kuna mtu anauliza hapa "Hawa wanawake wanaoongelewa hapa ni tofauti na wale wa makongamano ya ukombozi wa mwanamke na nyumba yakee?"

Comment isindikizwe na nyimbo ya Ghatto-Mamah!.
Chief Wanawake wanaozungumziwa ni hawa hawa wa kibinadamu, isipokuwa uzi wangu umewalenga zaidi baadhi ya wanaume wanaojiendekeza kwa kujiliza-liza na kutafuta huruma badala ya kuwajibika ipasavyo. Karibu uendelee kuchangia.
 
Ukitaka kumjua mwanamke zijue tabia za Paka, wanawake wote duniani wana tabia kama za Paka, ndio Paka huyu huyu Nyau.

wewe kaa mchunguze Paka utazijua tabia za wanawake.
Chief, Sijawahi kuwa na wazo la kumchunguza paka achilia mbali kumfuga. Naomba unijulishe tabia za Paka a.k.a Nyau ambazo zinashabihiana na za Mwanamke kama hutojali. Karibu.
 
Chief, Sijawahi kuwa na wazo la kumchunguza paka achilia mbali kumfuga. Naomba unijulishe tabia za Paka a.k.a Nyau ambazo zinashabihiana na za Mwanamke kama hutojali. Karibu.
Paka huyu huyu nyau au paka pori [emoji3]
 
Ukitaka kumjua mwanamke zijue tabia za Paka, wanawake wote duniani wana tabia kama za Paka, ndio Paka huyu huyu Nyau.

wewe kaa mchunguze Paka utazijua tabia za wanawake.
Nyau ni mstaarabu sema akinya hachambi anakalia mkia wake
 
Kama tutaacha kufuata mfumo mzima wa Dini unavyosema,tutarajia mambo tofauti na makubwa zaidi ya haya uliyoyaongea.
 
Kama tutaacha kufuata mfumo mzima wa Dini unavyosema,tutarajia mambo tofauti na makubwa zaidi ya haya uliyoyaongea.
Chief, naomba ufafanuzi yaani mambo makubwa kama yepi? Maana utaratibu wa Wanaume kuwa viongozi wa familia sisi Africa tulikuwa nao kabla ya hizi dini za mashariki ya kati kufika kwetu na mambo yalikwenda vizuri tu!! ndo maana mimi kwenye uzi wangu sikutaja dini bali nimetumia neno "Asili"

Lakini pia naona dini hizo zimekuja kushadidia na hazikupinga.
 
Kwanza unaandika vzr kwa mtiririko mzuri hakuna makosa ya kisarufi hongera sanaaa
 
Mkuu wanawake wenyewe wa Sasa hivi unawaonaje??

Siwezi kupoteza muda ku-act rijali kwa aina ya wanawake wa Sasa (walio wengi)

MIMI KUOA WATASUBIRI SAAANAAAAA!!!
 
Mkuu wanawake wenyewe wa Sasa hivi unawaonaje??

Siwezi kupoteza muda ku-act rijali kwa aina ya wanawake wa Sasa (walio wengi)

MIMI KUOA WATASUBIRI SAAANAAAAA!!!
Chief, Kuoa ni sunnah, hivyo hakuna anayeweza kukulazimisha (na akitokea atakuwa kinyume na sheria na kimaumbile). Hiyo aina ya sasa ya wanawake sisi ndo tumesababisha/pelekea wawe hivyo. Lakini yakupasa utambue kuwa katikati ya wengi wabaya, ndani yake kuna wachache wazuri, kazi ni kwako kuchambua, (Kila mtihani una heri ndani yake)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…