Wana MMU,
Nimekuwa msomaji wa threads mara nyingi kuliko kuchangia kwa muda mrefu, ila leo naomba na mimi nichangie japo kidogo. Hoja yangu inahusu wanaume na mapenzi. Nimeona kuna wanaume mara kadhaa huweka post zinazoonyesha kusalitiwa na mwanamke aliyemuamini na kumpa moyo wake. Kwa mfano, ulimpenda, hakuwa na elimu sana, ukamsomesha alafu akakutenda. Au anafanya biashara ukampenda, ukampa mtaji lakini ukagundua kuwa ana mtu mwingine, wewe ukabaki unaumia moyo. Au hata kama ana hela zake na anakuzidi kipato au elimu, mkapendana, lakini ukagundua amekupenda kwa sababu ana interests zake fulani anataka kuziachieve kutoka kwako. Akizipata wewe si lolote na si chochote atakutupilia mbali kama C....m. Badala ya kubaki unaumia moyo na kulalamika na kulipiza visasi, nakushauri mambo yafuatayo.

- Usidhani kwa kumpa hela, kumsomesha au kumpa gari ndo atakupenda milele. Achana na hayo mawazo mapotofu. Ukijua hilo mapema, utajua kuwa kumfanyia hayo mambo siyo kumfanya akupende, ni zaidi ya hapo. Hivyo basi, fanya hayo ukijua kuna uwezekano kama hajakupenda kwa dhati bado atakuacha na kukusaliti.
- Ikishatokea umemgharimikia sana mwanamke na hatimaye ametoka kimaisha na akakuacha, usipoteze muda wako kujutia muda na gharama ulizotumia kumsaidia katika maisha yake. Anza maisha upya maana hujui ni kwa nini Mungu amekuepushia hilo. Pia, ukiendelea kuwa na msongo unajiharibia afya yako bure wakati mwenzako anapeta huyooo. Pia utakuwa umeshapata fundisho maishani.
- Acheni kutanguliza pesa kwenye mapenzi. Mpime huyo unayetaka kuanza naye mahusiano kabla, uone msimamo wake kimaisha. Kwa mfano, mmeshafahamiana, na kupeana ahadi lukuki za mahaba, ukishaona sms za kuomba vocha, hela ya saloon, kodi ya nyumba etc. wakati penzi lenu halina hata mwezi shtuka. Utaliwa.
- Katika hatua za mwanzo kabisa za mapenzi, angalia mwenzako ni mkweli kiasi gani, mpe hata jaribu dogo tuu, onyesha kama vile umepatwa na tatizo fulani na umekwama kabisa. Uone atakavyohandle tatizo lako, utajifunza kitu.