King Jaja of Opobo
Member
- Aug 20, 2013
- 49
- 5
Imezoeleka kuwa wanawake ndiyo viumbe pekee wanaopata manyanyaso toka kwa wenza wao, jambo ambalo lilisababisha vita kali kuanza
vita ya kumtoa mwanamke katika manyanyaso, ukatili, udhalilishaji na kadhia zote zinazotajwa kusababishwa na maumbile yake.
Hata hivyo, ukifuatilia kwa karibu, pengine kusikiliza visa vingi vinavyotokea katika mitaa ya hapa nchini, utagundua kuwa wanaume nao, wananyanyasika kwa kiasi kikubwa kama wanawake wanavyonyanyasika bali wanaficha ukweli. Pengine wanaona ni fedheha, aibu au labda si jambo lililozoeleka katika jamii hasa za Kiafrika. Lakini huu ni wakati mwafaka wa kuuweka wazi ukweli kuhusu manyanyaso mnayoyapata. Umefika wakati wa kusema ukweli kuwa wanaume nao wanapata manyanyaso, ili kama ni vita kwa ajili yao, ianze tena kwa makali kama ile inayofanyika kwa ajili ya wanawake. Source Mwananchi 27 September 2013