Wanaume naomba ushauri wenu make mume wangu simuelewi

Wanaume naomba ushauri wenu make mume wangu simuelewi

Dada sikiliza mume wako anatatizo moja tu ambalo ukiweza kulimudu atabadilika ,anasykology ya kuongoza hapendi kuongozwa wala kupingwa. Kwa hiyo wazo lolote akilitoa sema ok,likiharibika then its is your right chance to argue then fanya marekebisho. Usipofanya hivi atadhani dharau. Kumbuka mwanaume always ni mtoto kwa mwanamke ktk maswala ya mapenzi,jaribu kurudisha Yale matendo ambayo ulikuwa Unafanya wakati wa uchumba mfano ,dear Leo nikutayalishie nini,kuna juice unapenda nini? Vitu vidogo tu basi atachenji. Always kuwa smart in dressing,manukato,aproching face etc.Mimi nikirudi nyumbani lzm ninywe juice nimeweka wazi kwa wife nisipokuta lzm anipe sababu. Mume wako si muwazi kwa maswala haya jalibu kurivew maisha ya awali utajua tu. Mfano mwingine mke wng nikimuudhi naenda kununua nyama choma nikirudi anatafuna yameisha, unajua ni Kwanini enzi za uchumba kila out anapenda kwenda nyamachoma. Jitahidi dada akiwa juu wewe usipande Ndio sheria

yani ushauri huu dada yangu ndio ukweli mtupu juu ya tatizo la mumeo jaribu kuusoma kwa kuurudia rudia utapata point muhimu za kuweza ku solve hilo tatizo la mumeo,..japo sio mara zote useme ok.....sometime unaweza ku propose tofauti....
 
Pole sana mdogo wangu. Hapo kuna uwezekano tofauti. Kwanza anaweza kuwa anahitaji mtoto mwingine maana umesema mnaye mmoja wa 5yrs.Pili,labda anakuwa katoka kwa mwanamke mwingine.Tatu,labda ndugu/wazazi wanamweleza mabaya kukuhusu ww.Pia yaweza kuwa stress za kazini. Kikubwa subiri siku katulia.Pika chakula anachokipenda mle.Kama mnakunywa,kunyweni kidogo. Ongea naye kwa upole.Sight tukio la mwisho ili akumbuke.Kama hatakueleza,ataacha hiyo tabia.Mwombe sana MUNGU Atakusaidia.
 
Yasiyo wazika ni yapi hayo Dada?

Angalia tabia zako na uwezo wako katika kazi;
mahusiano yako na Jamii na aina ya marafiki ulionao;
tabia yako kabla ya ndoa;
sifa na mienendo yako kabla ya ndoa na sasa;
Je una msaada gani kwa mumeo?;
Uwezo wako wa uelewa hasa katika mambo ya kifamilia;
Unachangia nini katika familia yako au wewe kazi yako ni kuangalai TV tu! Kila kazi anafanya House maid?;
Elimu yako ni ya kiwango gani? na je unajiendeleza hata kwa njia ya mitandao na Posta?
Unajua kupika au ndio wale ambao mme ana kisukari lakini hata vyakula vya wagonjwa wa kisukari huvijui na hata hujui kuvipika!?;
Unajua mambo ambayo mmeo anavipenda? Au unajifanyia tu kila jambo bila uweledi wowote?

ni maoni yako na nninayapokea. kama nikupika mimi uwa nampikia mume wangu na mtoto wangu. kwa ujumla familia yangu .kazi ya dada nikuandaa kama kuchemsha maharage na nyama. na namshukuru mungu mume wangu ndo kaajiliwa mi ninauza kwenye h/dware yetu ambayo haipo mbali na nyumbani kwetu. kiufup kwa kumjali mume wangu nipo sawa. kuanzia jikoni, sita kwa sita hata kumsuprise kwa zawadi
 
Kupika ni elimu kubwa ambayo wanawake wengi wa kitanzania hawajui, wachache walio kubali kujiendeleza ndio nafuu. Angalia kila line ya maswali yangu kwa kweli wengine hawapendi kuongea hasa kurudia rudia kila siku jambo lile lile.

Katika zama hizi za haki sawa na fursa sawa wanawake wengi hawawezi na wengine wahajui kabisa majukumu ya unyumba.
 
akinuna na wewe endelea na shughuli zako kama huoni vile, wanaume dizaini hii hiyo ndo dawa yao. mie alikuwa akinuna napotea siku nzima na-catch up na shughuli zangu za hapa na pale. kama kuna shosti sijamwona siku nyingi naenda kumtembelea tunapuyanga weee! mbona kashika adabu mwenyewe

yan kweli wanaume wa kununanuna wanachosha na kukera sana sema wao hawajui tu,mm nlkuwa na boyfrnd yan kitu kidgo anakununia hata siku mbili na bado anatka yy ndo kakosea ila umuombe msamaha mimi nlishindwa kutokana na matendo yake nkaona kila mtu aendelee na maisha yake.
 
mwanaume mjinga huivunja ndoa yake kwa mikono yake yeye mwenyewe...

mshirikishe Mwenyezi MUNGU katika tatizo hili madam dagaa..
 
Last edited by a moderator:
  1. kuwa mpole
  2. endelea kumkarimu na kumfurahia
  3. kama hapigi simu/anapiga kwa dada, wewe mpigie, mjulie hali na mpe pole ya kazi!
  4. ikibidi mtumie sms nzuri bila kuchoka
  5. katika siku anazonuna, hakikisha unapendeza!
  6. mueleweshe kuwa unaumia kuona yeye ananuna!
 
tulia, mumeo anampango kando, huo Ndio ukweli.....
 
Baba yake rafiki yangu alikuwa akiwa hana hela muda wote alikuwa ananuna ili watoto na mke wake wamuogope wakose jinsi ya kumuomba hela.... fanya uchunguzi hilo
 
Pole sana mdogo wangu. Hapo kuna uwezekano tofauti. Kwanza anaweza kuwa anahitaji mtoto mwingine maana umesema mnaye mmoja wa 5yrs.Pili,labda anakuwa katoka kwa mwanamke mwingine.Tatu,labda ndugu/wazazi wanamweleza mabaya kukuhusu ww.Pia yaweza kuwa stress za kazini. Kikubwa subiri siku katulia.Pika chakula anachokipenda mle.Kama mnakunywa,kunyweni kidogo. Ongea naye kwa upole.Sight tukio la mwisho ili akumbuke.Kama hatakueleza,ataacha hiyo tabia.Mwombe sana MUNGU Atakusaidia.

hayo yote umeyatoa wapi ndugu umetengeneza majungu lengo lako uue ndoa ya watu so sad kama hujui kushauli kaa kimya kuliko kubuni ishu za maana
 
Kiukweli hiyo tabia inatokeaa hata kama nikiwa sina cash nakuwa hasira sana kwa hiyo inatokea kipindi akiwa amenuna ww jaribu kumfanyia vitu vizuri
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom