USHAURI: Simuelewi mume wangu

miss chuga

JF-Expert Member
Dec 25, 2019
296
623
Habari za majukumu?

Nambeni wenye ujuzi na mambo ya ndoa mnisaidie hapa maana nimewaza mpaka akili imechoka na majibu nimekosa.

Mume wangu amekuwa ni mtu ambaye kufanya tendo la ndoa ni mpaka mimi nimuanze ndiyo tunafanya. Ila na mimi siku nikijikausha tunaweza tukamaliza hata wiki 2 tusifanye wakati mwingine tunaweza maliza hata mwezi mama nisipomuanza.

Kinachonikera zaidi ni kwamba hata wakati mwingine nikimuanza mimi, anaweza kuniambia mke wangu leo nimechoka naomba tulale tutafanya siku nyingine. Hiki kitu kiukweli kinaniumiza sana akili, raha ya mapenzi kila mtu aoneshe ana hamu na mwenzake siyo kila siku mimi ndiyo nianze kuomba mapenzi.

Hapa nawaza ni kwamba atakuwa na matatizo ya nguvu za kiume au inawezekana ana michepuko anafanya huko akirudi nyumbani amechoka hana hamu na mimi, au inakuwaje au pengine kalogwa asiwe na hisia na mimi, ila bado nmekosa majibu!

NB: Nimejaribu hadi kubadilisha mazingira ya nyumba, nimepanga upya nyumba ni safi inavutia na akirudi anakuta nimeshaoga nimejipamba najitahidi kuvaa na vinguo vya kumtega lakini bwana huyu hata haoni, wakati mwingine mpaka navua nguo zote usiku namuomba anikumbatie kwa makusudi ili apate nyege lakini wapi, naye alivyo anaishia kunikumbatia bila kufanya chochote.

Nikisema nimuanzishie mimi mahaba anaishia kunambia mke wangu kuna joto usinishike tulale kwanza, yani napata hasira huwa natamani hata nipige ukunga.

Hivyo naombeni wataalamu wa mambo ya ndoa mnishauri tatizo ni nini au mimi nakosea wapi ili nijirekebishe ndoa yangu iwe na amani maana imefika hatua nimeshajikatia tamaa.

Pia soma:
MREJESHO: Simuelewi mume wangu
 

Glenn

JF-Expert Member
May 22, 2018
23,973
42,586
1. Hali yake kimaisha iko sawa au imeshuka....ukame huondoa nyege hasa uliyezoea kushika pesa ndefu.....naongea kwa uzoefu.

2. Biashara zimemnyookea?

3. Yuko busy na simu?

4. Anachelewa kurudi?

5. Unamkoromea? Au mnalumbanaga?
Ikiwa mnalumbana hili ni tatizo, mwanaume hapendi kabisa kutosikilizwa au kujibiwa vibaya na mwanamke.
Endapo utayafanya hayo atakosa hamu na wewe kabisa
 

Emushi

JF-Expert Member
Sep 20, 2022
2,088
4,335
Kuna ninayotaka kujua hapa
JamiiForums-1491704105.gif


Kwanza kabisa nature ya kazi yake pili kipato tatu mazingira ya wewe na yeye
 

Toxic Concotion

JF-Expert Member
Aug 5, 2015
4,483
13,903
Kuliko kumlazimisha kufanya tendo ambalo ni dhahiri hataki kulifanya ni bora ukamuweka chini ki upole na kumuuliza nini kinamsibu.

Desturi ya mwanaume ni sawa na kujivua nguo hadharani pale anapokiri kuwa kuna tatizo la nguvu za kiume.
Inawezekana asiwe na mapungufu ya nguvu za kiume lakini akawa na mambo yanayomzonga akili kiasi cha kuathiri utendaji wake.

Tiba ya kwanza daima ni kujua kiini cha tatizo. Na hilo hutolijua pasi kumuhoji. Ondoa dhana yeyote kuwa ana mchepuko maana hiyo itapelekea kuhalalisha hisia za wewe kutaka kuchepuka.

Mwisho na kubwa zaidi, linganisha utendaji wake wa kimapenzi wa toka mlipoanzana na wa hivi sasa. Isije ikawa toka mmekutana alikuwa si mpenzi wa tendo (kuashiria kuna tatizo) ukaanza kuhangaikia tiba ya tatizo sugu.
Kila la heri na Mungu akusimamieni katika ndoa yenu.
 

Mad Max

JF-Expert Member
Oct 21, 2010
12,412
27,058
Mkuu Glenn kataja hapo juu, kwa kuongezea:

1. Unatabia ya kukaa naked sana mkiwa ndani wawili tu. Yaani unakua na chupi tu? Jitahidi uwe unavaa muda wote nguo mfano Tshirt kubwa, unaacha mapaja tu, khanga flani, dera, etc ila usishindie kyupi tu, anakinai.

2. Anzisha kitu taratibu. Mfano unamfanyia massage, unamnyoa nywele za kwenye sirini, unamkata kucha, unamuosha miguu, etc ivyo vitu vidogo vinaamsha hamasa.

3. Usisubiri mwende kitandani ndio umuanze. Na usisubiri ifike saa 4 usiku kila siku ndio muanze. Kua creative, unamwambia ukamuogeshe, amekaa kwenye kochi unaenda kulala kwenye mapaja yake, etc.

4. Mwangalie usoni. Aisee tunapenda sana kuangaliwa usoni sio mchezo.

Ngoja niishie hapo. Mstari wa chini ni nje ya Mada.

Vijana tusioe, tusubiri hali itulie.
 

Depal

JF-Expert Member
Nov 26, 2018
34,172
136,375
Mkuu Glenn kataja hapo juu, kwa kuongezea:

1. Unatabia ya kukaa naked sana mkiwa ndani wawili tu. Yaani unakua na chupi tu? Jitahidi uwe unavaa muda wote nguo mfano Tshirt kubwa, unaacha mapaja tu, khanga flani, dera, etc ila usishindie kyupi tu, anakinai.

2. Anzisha kitu taratibu. Mfano unamfanyia massage, unamnyoa nywele za kwenye sirini, unamkata kucha, unamuosha miguu, etc ivyo vitu vidogo vinaamsha hamasa.

3. Usisubiri mwende kitandani ndio umuanze. Na usisubiri ifike saa 4 usiku kila siku ndio muanze. Kua creative, unamwambia ukamuogeshe, amekaa kwenye kochi unaenda kulala kwenye mapaja yake, etc.

4. Mwangalie usoni. Aisee tunapenda sana kuangaliwa usoni sio mchezo.

Ngoja niishie hapo. Mstari wa chini ni nje ya Mada.

Vijana tusioe, tusubiri hali itulie.
Abee mdogo wangu 🙈
 

miss chuga

JF-Expert Member
Dec 25, 2019
296
623
1. Hali yake kimaisha iko sawa au imeshuka....ukame huondoa nyege hasa uliyezowa kushika pesa ndefu.....naongea kwa uzoefu.

2. Biashara zimemnyookea?

3. Yuko busy na simu?

4. Anachelewa kurudi?

5. Unamkoromea? Au mnalumbanaga?
Kwa upande wangu Mimi naona Hali ya kimaisha ipo sawa mpaka anapata na ela za kubetia kila siku na huwa simkoromei Wala hatuna malumbano ndani amani ipo Kama ni ela za matumizi anaacha kunipenda ananipenda sana tu tunacheka, tunapiga story yani hamna shida kabisa tatizo ni Hilo moja tu la kutokupewa haki yangu, na kinachoniumiza akili hivi hata Kama mwanaume ana michepuko jamani ndoasinimc mke wake hata kwa wiki tu japo Mara moja mpaka inafika wakati nawaza au kalogwa ili akose hisia na Mimi dah! Ukisikia ndoa ni ngumu ndo hii sasa
 

miss chuga

JF-Expert Member
Dec 25, 2019
296
623
Naona unapambania haki yako hutokei kujibu maswali...pambana upewe hata kimoja
Nipambane wapi hapa nimejiweka kimtego mtego Ila mwenzangu hata hategeki ndo kwanza yuko bze anacheza na mtoto natamani hata nikachukue maji ya baridi nimmwagie pengine akili itamkaa sawa inakera kwakweli hapa nawazaa kwanzia kesho nianze kulala na jinsi maana naona najitesa tu na baridi mwenzangu hana habari
 

Similar Discussions

40 Reactions
Reply
Top Bottom