Wanaume msifanye hivi

Wanaume msifanye hivi

trudie

JF-Expert Member
Joined
Jan 15, 2014
Posts
4,444
Reaction score
10,790
Tukiwa tunaianza wikiendi tulivu kabisa nawasalimu wanajukwaa wote.
Kilio changu mimi ni kwa wanaume hasa waliooa, wanaoishi na wachumba au wapenzi wao iwe kwa kutoa mahari au kinyemela ila unaishi nae. Awe kakuzalia watoto au bado Mungu hajawajalia.

Jamani wanaume waheshimuni sana wenzi wenu maana huyo ndio anayekulelea watoto wako. Usimseme vibaya mwenzi wako kwa ndugu na marafiki zako mfichie madhaifu na mapungufu yake.

Unaposhiriki kumsema vibaya jua kwamba humuaibishi yeye tuu bali na wewe unajiabisha kwa hao watu.

Wanaume jamani kamwe usikubali watu wakamwongelea vibaya mwenzi wako mbele zako na wewe ukacheka tuu mtetee onyesha kwamba wewe hufurahii hicho kitendo hata mwongeaji awe mama au baba yako mzazi mwenzi wako ni wa thamani sana.

Jambo lingine jamani wanaume usimdhalilishe mwenzi wako mbele ya watu, usimtukane wala kumkaripia. Hata akikukosea kuna sehemu sahihi ya kumwambia kosa lake ila sio mbele za watu unamfanya akose raha na kukosa "confidence". Mheshimu sana mama watoto wako maana amejitoa sana kukuletea hao watoto alibeti kifo chake kuingia leba ili tuu uitwe baba.

Mwisho kabisa wanaume wakwe zako ndio waliokufanya upate mke nae atakuletea watoto wazuri jaribu kuwaheshimu na kuwajali. Kuwajali namaanisha hata kuwasalimia na kuwatembelea angalau wanaona mtoto wetu ameenda sehemu sahihi.

Ni hayo tuu kwa leo enyi wanaume. Nawatakia wikiendi njema.
 
Kiufupi wewe ni family politician,unaweza kuwa mkoloni wa familia kwa kujificha kwenye kivuli cha kuzaa watoto!!

Kwanza watoto si wa mwanaume,watoto ni wazazi wote,kusema umenizalia watoto mimi mwanaume huko ni kunizubaisha ili niwe fala kwako,mbona mwanamke alibakwa na akazaa hasemi kwa aliyembaka kuwa nimebeti kifo kuingia leba kukuzalia mtoto?

Mwanamke mwenye hekima hawezi kuongea haya maneno ya kibinafsi na kibaguzi,kwahiyo mmeo awakumbatie wazazi wako awaache wazazi wake au vipi,

Mi nadhani mwanamke na mwanaume wanatakiwa waishi vizuri bila kuegemea upande wowote,hakuna anayetakiwa kujiona ana anafaa zaidi kuliko mwenzake.

Mtoa mada acha siasa,
 
inaonekana mkuu wewe ni mmoja wa wanaoongelewa hapo juu...Hakuna sehemu inasema uwaache wazazi wako bali usifurahie wazazi wako wakamsema vibaya mwezi wako mbele yako maana madhaifu yake ni yako pia.
 
  • Thanks
Reactions: 365
Biblia haisemi tuwaheshimu wake zetu bali tuwapende....wake ndio wameaswa kutuheshimu na kututii sisi....Mungu anajua kabisa kuwa mwanamke akiheshimiwa huwa anabadilika na kuwa mbaya kuliko shetani...yy apendwe tu..ova
Ukimpenda mke wako hutamtangazia madhaifu yake yawe ya kweli au uongo kwa ndugu na marafiki zako...pia ukimpenda mke wako hutafurahia asemwe vibaya mbele yako. Kwa kifupi ukimpenda mke wako yote hayo hayatafanyika ni sawa na heshima tuu
 
Hujaona alivyozungumzia wakwe? Mi sijaoa bhana wewe,ila napenda haki
inaonekana mkuu wewe ni mmoja wa wanaoongelewa hapo juu...Hakuna sehemu inasema uwaache wazazi wako bali usifurahie wazazi wako wakamsema vibaya mwezi wako mbele yako maana madhaifu yake ni yako pia.
 
Tatizo mkiheshimiwa mnaleta jeuri unakuta mnatuona kama mabwege vile.
Kama unashindwa kumheshimu basi hata mdefend mkeo pale unapoona anaonewa. Beba madhaifu yake kama yako maana hata yeye ana yako mengi anakubebea
 
You may not be interested with that baby by then, but you may be enjoying .........
 
Hujaona alivyozungumzia wakwe? Mi sijaoa bhana wewe,ila napenda haki
Mkuu uzi unasema usifurahie mwenzi wako akisema vibaya hata kama na mama au baba yako. Upande wa pili unasema waheshimu na kuwajali kwa salamu wakwe zako sasa sijui wewe umesoma wapi
 
  • Thanks
Reactions: 365
Tatizo kuna mda mwanamke anakuwa anamdomo, anaropoka mbele ya watu utaacha kumgombeza au kumkaripia??

me mwanamke akinijibu hovyoo mbele za watu ntamkata hayoo maskio. tukiwa chumbani ajibu atakavyo ata atukane sawa tu.
 
Mwisho kabisa wanaume wakwe zako ndio waliokufanya upate mke nae atakuletea watoto wazuri jaribu kuwaheshimu na kuwajali. Kuwajali namaanisha hata kuwasalimia na kuwatembelea angalau wanaona mtoto wetu ameenda sehemu sahihi.

Mbona hujaongelea wakwe zako,

Kama wewe umeandika hujakopi hii story basi jua kabisa kua hauko fair,
Mkuu uzi unasema usifurahie mwenzi wako akisema vibaya hata kama na mama au baba yako. Upande wa pili unasema waheshimu na kuwajali kwa salamu wakwe zako sasa sijui wewe umesoma wapi
 
Ukimpenda mke wako hutamtangazia madhaifu yake yawe ya kweli au uongo kwa ndugu na marafiki zako...pia ukimpenda mke wako hutafurahia asemwe vibaya mbele yako. Kwa kifupi ukimpenda mke wako yote hayo hayatafanyika ni sawa na heshima tuu
Ni upendo.....kulingana na biblia takatifu....
 
Back
Top Bottom