Wanaume msifanye hivi

Wanaume msifanye hivi

Tatizo kuna mda mwanamke anakuwa anamdomo, anaropoka mbele ya watu utaacha kumgombeza au kumkaripia??

me mwanamke akinijibu hovyoo mbele za watu ntamkata hayoo maskio. tukiwa chumbani ajibu atakavyo ata atukane sawa tu.
Hahahahhaha
 
Kwa wazazi wetu mnasema
"Mwanaume ataacha wazazi wake na kuambatana na mkewe"ila wazazi wenu ndio tuwakumbuke na kuwatembelea.
Ujinga tu.
Kwani Mimi wazazi wangu hawakumletea yeye mtu wa maana duniani!?
 
Kwa wazazi wetu mnasema
"Mwanaume ataacha wazazi wake na kuambatana na mkewe"ila wazazi wenu ndio tuwakumbuke na kuwatembelea.
Ujinga tu.
Kwani Mimi wazazi wangu hawakumletea yeye mtu wa maana duniani!?
Mkambiwa ukweli hamtaki kukubali....wanaume waheshimu wenzi wenu ndio maana kichwa cha habari kinasema "wanaume" na sio "wanawake" acheni kupenda mashindano na ligi hizo. Wanaume msifanye hivyo
 
Ni bora kupendana tu.. upendo ule ulio na nguvu kuliko mauti. upendo unasitiri wingi wa dhambi...!!!
 
Mwanaume mwenzangu inawezekana neno UPENDO hukulisoma vzur ktk bible.. Hebu pitia hapa..

1 Wakorintho 13:4-8

4 Upendo huvumilia, hufadhili; upendo hauhusudu; upendo hautakabari; haujivuni;
5 haukosi kuwa na adabu; hautafuti mambo yake; hauoni uchungu; hauhesabu mabaya;
6 haufurahii udhalimu, bali hufurahi pamoja na kweli;
7 huvumilia yote; huamini yote; hutumaini yote; hustahimili yote.
8 Upendo haupungui neno wakati wo wote; bali ukiwapo unabii utabatilika; zikiwapo lugha, zitakoma; yakiwapo maarifa, yatabatilika.


Hapo mstari wa 5 maneno ya mwanzo kabisa... Au tuliambiwa tuwape upendo upi.. Nieleweshe ndg yangu huenda nami nikawa nakosea.
 
Tukiwa tunaianza wikiendi tulivu kabisa nawasalimu wanajukwaa wote.
Kilio changu mimi ni kwa wanaume hasa waliooa, wanaoishi na wachumba au wapenzi wao iwe kwa kutoa mahari au kinyemela ila unaishi nae. Awe kakuzalia watoto au bado Mungu hajawajalia.

Jamani wanaume waheshimuni sana wenzi wenu maana huyo ndio anayekulelea watoto wako. Usimseme vibaya mwenzi wako kwa ndugu na marafiki zako mfichie madhaifu na mapungufu yake.

Unaposhiriki kumsema vibaya jua kwamba humuaibishi yeye tuu bali na wewe unajiabisha kwa hao watu.

Wanaume jamani kamwe usikubali watu wakamwongelea vibaya mwenzi wako mbele zako na wewe ukacheka tuu mtetee onyesha kwamba wewe hufurahii hicho kitendo hata mwongeaji awe mama au baba yako mzazi mwenzi wako ni wa thamani sana.

Jambo lingine jamani wanaume usimdhalilishe mwenzi wako mbele ya watu, usimtukane wala kumkaripia. Hata akikukosea kuna sehemu sahihi ya kumwambia kosa lake ila sio mbele za watu unamfanya akose raha na kukosa "confidence". Mheshimu sana mama watoto wako maana amejitoa sana kukuletea hao watoto alibeti kifo chake kuingia leba ili tuu uitwe baba.

Mwisho kabisa wanaume wakwe zako ndio waliokufanya upate mke nae atakuletea watoto wazuri jaribu kuwaheshimu na kuwajali. Kuwajali namaanisha hata kuwasalimia na kuwatembelea angalau wanaona mtoto wetu ameenda sehemu sahihi.

Ni hayo tuu kwa leo enyi wanaume. Nawatakia wikiendi njema.
Kwenye avatar ni wew kiongozi?
 
mwanamke tumeumbiwa wanaume.........anaeanzaga kutoa ya ndani siku zote ni mwanamke.....bisha au kataa uwezavyo.....wanaume hatuongei sana ila tunatekeleza......na najua wapi pa kukamilisha utekelezaji......acha siasa
 
kama amenitia aibu mbele za watu ni makofi hapo hapo hakuna cha sijui nikamwambie pembeni
 
Tatizo kuna mda mwanamke anakuwa anamdomo, anaropoka mbele ya watu utaacha kumgombeza au kumkaripia??

me mwanamke akinijibu hovyoo mbele za watu ntamkata hayoo maskio. tukiwa chumbani ajibu atakavyo ata atukane sawa tu.
ni kumalizana nae hapo hapo
 
Back
Top Bottom