king suleman
JF-Expert Member
- Jun 28, 2014
- 1,749
- 1,151
Wewe kama una mind vitu hivyo kuolewa hutaweza.....Kuna wanaume wanapenda u-mwinyi bwana, yaani anaamka anaenda kuoga wakati anaoga unatandika kitanda na kuweka mazingira ya chumba vizuri. Unakwenda jikoni kuandaa chai, anatoka bafuni na taulo kiunoni anatafuta atavaa boxer na kama atakumbuka mafuta basi itakuwa kwenye viganja vya mikono. Taulo atakuachia juu ya kitanda si tatizo lake tena.
Mezani umeandaa chai na vitafunio hata kama chumvi haisikiki mfano kwenye mayai atakuita ukamchukulie jikoni hapo ni baada ya kukuita umletee maji ya kunawa na tissue ya kujikaushia.
Yaani ameshindwa kabisa kwenda kunawa jikoni au bafuni au kwenda jikoni kuchukua chumvi. Na akimaliza kula hataondoa hata kijiko mezani anaacha kila kitu pale anakwenda kukaa kwenye sofa anaangalia mpira, kusoma gazeti au anachat kwenye simu. Hiyo ni weekend.
hayo ni sehemu ya Majibu yatokanayo na Mada.Hujaelewa mada.
Mkuu umemaliza kila Kitu.Tatizo Lenu Mkisaidiwa Leo Kutandika Kitanda Kesho Utaacha Makusudi Kesho Kutwa Utasema Naomba Nisaidie Kumuogesha Mtoto Nikimuogesha Mara Mbili Tatu Kuna Siku Utasema Mtoto Hajaoga Tu? Nikizoea Kumuogesha Utasema Na Hizo Nguo Mbili Za Mtoto Nifulie Povu Moja ,nikifua Utasema Sasa Hilo Povu Unamwaga Bure C Ufue Hata Zile Nguo Zako Apo Ndo M/ume Umeshaingizwa Kwenye Kaz Za Nyumban Kuna Cku Atakwambia Nimechoka Nisaidie Kupka Ukifanya Hvo Kuna Siku Atachelewa Kulud Akijua We Utapka Ucpo Pika Atakuuliza Yan Hujapika Tu,,, WITO KWA WANAUME WOTE USIMSAIDIE CHOCHOTE WF WAKO
Nishagundua una matatizo ya kupangilia nyumba yako
Niko meza ya chakula, toothpick, chumvi, tissue nk ndo mahala pake, sasa nisipoviona na hakuna maji ya kunawa nifanyeje? Niende kutafuta viliko? Na nikikuuliza unakunja mdomo na pua?
HAPANA labda uwe umenioa wewe
ushaingia geto la mwanaume ukaona mpangilio wake?Nature mbona mkiwa kwenye mageto yenu hamfanyi hivyo !?
Huwa inaboa sana mtu anasimama anavua nguo anaacha hapo hapo.
Taulo kitandani,upo unapika anakuita kamletee glass mara kidogo kaita umtafutie charger,
Hujarudi vizuri anaulizia remote,
Ukikaa ujiandae uepue unaitwa ukawashe ac/feni.
Mpaka ifike jioni unatamani aondoke tu walau upumzike !
Sasa kama sioni soks moja nivae hio moja miguu yote?Anakuja kukuita jikoni uko kati kati ya mapishi kisa haoni socks ya pili na anachelewa huko vaendako.